Tunahitaji kuwekeza kwenye engineering knowledge ili tupige hatua zaidi

eddy

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2007
Posts
16,054
Reaction score
11,568
Ukikaa na kijana wa kiyahudi (Israeli) anachowaza ni kuvumbua, mtoto analelewa tangu mtoto kuwa yeye anaakili sana na anapaswa kuzitumia kuvumbua.

Tuje kwetu kijana anahitimu degree hajaenda field na hajui atafanya kazi gani baada ya kuhitimu na hata ukimwajiri tofauti yake na form four ni ngumu kuitenganisha.

Leo hii charger ya simu ikigaribika unatupa hakuna fundi, mafundi ujenzi wetu bado wanatumia kabilo ya kamba, wakati wenzetu wanatumia infra red beams, 80% ya wahitimu wetu ni walimu wa Geography na history. Na historia yetu ni ileile ya kinjeketile.

Mie ningependekeza yafuatayo, katika fedha za mikopo ya elimu ya juu tutenge 100bn kila mwaka kusomesha engineer's katika nchi za kimkakati kama Japan Germany China USA Canada. Na katika taaluma za kimkakati.

Prof Muhongo alipeleka vijana kusoma mafuta na gas wala sijui walifikia wapi nasukia wengine walivyorudi waliambia baba yenu alishaondoka wizarani.

Pia tunao best students katika shule za primary secondary hawa napendekeza wapewe 100% government sponsorship hizi ndio cream za kuendesha nchi yetu badae.

Lakini pia tunao best graduates katika vyuo vyetu napendekeza wapewe ajira moja kwa moja serikalini na kwenye mashirika ya kimkakati, mfano kijana atakaepata GPA ya 4.5 and above aajiriwe direct.

Tuondoe utaratibu wa best student kubaki TA badala yake wakurugenzi wenye umri wa miaka 50 and above na wana vigezo vya kuwa wahadhiri wahamishiwe kwenye vyuo na wafundishe hadi watakapokuwa na umri wa miaka 70 badala ya kustaafu wakiwa na umri wa miaka 60.
 
Lipumba ana bonge la GPA Ila Ni utopolo,Mwigulu ana 1st class nae ni uto fc.

By the way JK alipata Gentleman na akawa rais.

GPA Ni ujinga tu.
Sidhani kama Lipumba anavurunda kwenye taaluma yake,
 
Engineers wapo, tatizo kubwa ni namna ya kuwatumia hao vijana.
Serikali masikini huelekeza zaidi nguvu kwenye udhibiti badala ya kuwezesha uzalishaji.
Legeza udhibiti, wezesha vijana waendeleze miradi binafsi miaka mitano tu uone.
China wanaendelea baada ya kupunguzwa udhibiti kwenye ubunifu na uzalishaji.
Fikra kizamani za serikali kudhibiti kila kitu ni kurudisha nyuma kasi ya maendeleo.
 
Hapana tuwekeze zaidi kwenye watu wenye vipaji kama Haji Manara, Curpian Musiba na Baba levo, na Mwijaku🤣🤸‍♂️🐒
 
Ukikaa na kijana wa kiyahudi (Israeli) anachowaza ni kuvumbua, mtoto analelewa tangu mtoto kuwa yeye anaakili sana na anapaswa kuzitumia kuvumbua.

Tuje kwetu kijana anahitimu degree hajaenda field na hajui atafanya kazi gani baada ya kuhitimu na hata ukimwajiri tofauti yake na form four ni ngumu kuitenganisha.

Leo hii charger ya simu ikigaribika unatupa hakuna fundi, mafundi ujenzi wetu bado wanatumia kabilo ya kamba, wakati wenzetu wanatumia infra red beams, 80% ya wahitimu wetu ni walimu wa Geography na history. Na historia yetu ni ileile ya kinjeketile.

Mie ningependekeza yafuatayo, katika fedha za mikopo ya elimu ya juu tutenge 100bn kila mwaka kusomesha engineer's katika nchi za kimkakati kama Japan Germany China USA Canada. Na katika taaluma za kimkakati.

Prof Muhongo alipeleka vijana kusoma mafuta na gas wala sijui walifikia wapi nasukia wengine walivyorudi waliambia baba yenu alishaondoka wizarani.

Pia tunao best students katika shule za primary secondary hawa napendekeza wapewe 100% government sponsorship hizi ndio cream za kuendesha nchi yetu badae.

Lakini pia tunao best graduates katika vyuo vyetu napendekeza wapewe ajira moja kwa moja serikalini na kwenye mashirika ya kimkakati, mfano kijana atakaepata GPA ya 4.5 and above aajiriwe direct.

Tuondoe utaratibu wa best student kubaki TA badala yake wakurugenzi wenye umri wa miaka 50 and above na wana vigezo vya kuwa wahadhiri wahamishiwe kwenye vyuo na wafundishe hadi watakapokuwa na umri wa miaka 70 badala ya kustaafu wakiwa na umri wa miaka 60.
Tunachoweza si ni kuwekeza katika siasa,tena siasa zile za kitanzania, huko kwenye maengineering tuwaachee walioamua kutopoteza muda kwenye siasa chafu.
 
Lipumba ana bonge la GPA Ila Ni utopolo,Mwigulu ana 1st class nae ni uto fc.

By the way JK alipata Gentleman na akawa rais.

GPA Ni ujinga tu.
Haya ndio madhara ya mfumo wa elimu uliopo sasa, huyu anaona jambo la msingi sana ambalo mtu anaweza akalifanya kwa faida ya jamii yake ni kupata madaraka.

ukimsumbua sana na maswali mtu wa namna hii atakuambia namna ambavyo matajiri wa kikinga kariakoo hawajaenda shule. Yaani hii nchi inahitaji watu kama mbowe, ukisema unaangalia wananchi wanataka nini lazima usimame, solution ni kufanya kile unacho amini.

Hivyo basi narudisha swali kwako mleta mada, wewe mwenyewe, unachukua hatua gani sasa kuwa mvumbuzi au kuwa engineer?
 
Tukitaka tupige hatua. Inabidi tuwekeze kwenye vitu viwili.
1.Elimu
2. Research and Development(utafiti)

Tanzania elimu yetu inajifia iko ICU. Na msingi mkuu wa elimu uko kwenye elimu ya msingi, tukishaharibu huko, hata tuwekeze vipi kwenye elimu ya sekondari, ufundi na chuo, bado mambo yatakuwa ni bila bila. Kila mwaka tunasoma ripoti kuwa wanafunzi wanamaliza darasa la saba ila hawajui kusoma, kuandika wala kuhesabu. Miundombinu hakuna, walimu wenyewe haba. Viongozi wapo tu wanachekelea. Hatuko serious na elimu yetu.

Kwenye utafiti ndo kabisa, innovation/uvumbuzi ndo unafanya nchi ipige hatua. Nchi zote zilizoendelea zinawekeza sana kwenye research and development. Ujerumani, Israel, South Korea n.k sisi hata kuwekeza tu asilimia moja ya pato la taifa, sawa na kama dola milioni mia sita, kwenye utafiti hatuna muda. Ila hela zinapatikana za kununua ndege kwa Cash, kununulia viongozi magari ya bei mbaya, kuwalipa marupurupu ya kila aina, na kubuni miradi ya upigaji isiyo na tija.

Hapo ndo utajua vipaumbele vya viongozi sio maendeleo, bali ni kujinufaisha wao na familia zao na kula vinono vya nchi.
 
Namkumbuka makonda aliwahi sema nchi hii wapuuzi kama konki liquid ndio hupewa promo kuliko wataalamu
Hapana tuwekeze zaidi kwenye watu wenye vipaji kama Haji Manara, Curpian Musiba na Baba levo, na Mwijaku🤣🤸‍♂️🐒
 
Namkumbuka makonda aliwahi sema nchi hii wapuuzi kama konki liquid ndio hupewa promo kuliko wataalamu

Wakati huo Makonda akiwa na utaalamu gani tofauti na Likwidi?

Hoja yako ni nzuri, ila umeinajisi hapo kwenye GPA zako.
 
Hivi wewe umesoma chuo kikuu chochote ukaona hao first class ni wadesaji wa kutupwa.

Na kwa udesaji wao wakifika kwenye field ni mambumbumbu wa kutupwa, kwa sababu waliishua kudesa chuoni.

Back
Top Bottom