Masokotz
JF-Expert Member
- Nov 26, 2018
- 3,713
- 6,121
Hiki ni kipindi cha siasa na kama kawaida huwa napenda sana kupita katika vijiwe vya kahawa kujadili kuhusu uelekeo wa siasa zetu na maendeleo yetu.
Katika vijiwe vyote nilivyopita pembeni ya kukuta watanzania wengi wakiwa bado na ile mitazamo ya ajabu ajabu kuhusu siasa na maendeleo kuna mambo manne ambayo yanajitokeza mara kwa mara ikiwamo. Ukosefu wa ajira,Ugumu wa maisha,hali Umaskini na hali ngumu ya uchumi.
Ukipita mjini na kuangalia idadi ya biashara ambazo zimefungwa unaweza kupata kihoro kwani ni kama vile tumegeuka TAIFA la WAMACHINGA na MAMA LISHE.mbaya zaidi wamachinga wengi wanauza bidhaa zile zile kutoka nchi zile zile.Kuanzia Posta,kariako,Tegeta,Sinza,etc.Hali ni ile ile.
Ukirudi mitaani huku idadi ya madalali imeongezeka,wa viwanja,nyumba etc na wanunuzi ni wachache.
Suala la kujiuliza ni Je kama TAIFA tufanye nini ili kubadilisha hali ya TAIFA letu?Tuanze na nini?