Tunahitaji mfumo mpya wa kijasusi?

Mkuu hakuna mpepelezi anayeongoza kama akina Jack Baur na kina Wily Gamba, Joram Kiango n.k.
Ila kunakuwa na Unit flan ndani ya agencyambayo ndio inakuwa inategemewa sana lakini sio mtu individual.
 
Mimi nina swali kwa intelijens kabisa, ni kweli eti kuwa hizi harakati za Miamsho ya Kiislamu Zanzibar yenye nia ya kuvunja Muungano na kuunda Jamhuri ya Kiislamu, eti harakati zote zinafanyika Iran ili zanzibar pahala bila uchafu wa kimagharibi kama Utalii, Ulevi, nk, kweli?
 
Naomba nitoe angalizo.
Naona watu wanatolea mifano kwa kuitaja sana CIA. Kwa taharifa yenu Intelligence agency ambayo ni high efficiency na kiwango zaidi Duniani ni ile ya Pakistan, ISI.

Chanzo ni Hollywood.
 
Duh kweli sisi ni kama tunatembea bila nguo kwa huo ulinzi wetu, tunadepend jeshini tu!!!
 
Kama serikali haina mpango wa kuimarisha usalama wa nchi, na sisi tunaona kabisa usalama wetu uko mashakani suluhisho ni nini? tulalamikie nini ili wafanye nini? je? ni rahisi kiasi gani kutenganisha siasa na usama wa nchi?

Mkuu Mpingauonevu, maswali yako yameibu maswali mengi kichwan mwangu hasa juu ya uwezekano wa kuwa na utawala wa sheria/intelijensia isiyo na chembe ya siasa katika dunia yetu hii ya tatu hasa Tanganyika tulio fundishwa kuishi kindugu, kusaidiana na kuhurumiana, tuliofundishwa misemo na methali za kuvutia(zimwi likujualo halikuli likakwisha, heri shetani uliyemzoea kuliko malaika usiyemjua nk.). Itanipa shida kukuweka kwenye kitengo wewe nisiyekufaham usije ukaniharibia mipango yangu. Kama ina wezekana, inawezekanaje kufanya tofauti na matakwa ya aliyekuweka katika kitengo ikiwa sote twajua kuwa mkuu wa kitengo cha upekuzi/ujasusi/intelijensia (whatever you call it) hupointiwa? Aina ya demokrasia tuliyonayo sisi wa dunia ya3, pia inanipa shida kuamini kuwa hii kitu inawezekana kwa sasa hapa kwetu.
 
Wadau ivi hapa kwetu tz kuna kipaumbele cha kuwatumia watalaamu wetu hususani vijana kwa manufaa ya taifa la kesho kuweza kutumia teknolojia ya kwa manufaa ya taifa siyo tu kukaa na utamaduni wa zamaaaaaaaaani wa kusikiliza watu wanaongea nn? sawa hauwezi kuacha ila dunia imebadilika kila nyanja leo ujasusi wa wenzetu uko ktk uchumi na tekn zaidi sijui hawa UWT.....? ukienda ubalozi wa japan DSM watakwambia ni magari mangai yameingia $$$ ila upande wa pili sijui hata kama wana dalili yeyote ile
 

hivi haiwezekani kitengo cha intelijensia kuwa kinajitegemea na ajira zikawa ni za kuomba? nasikia (sina uhakika) kwamba CIA ni kitengo (taasisi) kwa hiyo unapoomba kazi unatoa vielelezo vyote. Kwa nini na sisi kwetu isiwe hivyo ili tuondokane na huu usalama wa ndugu na tupate usalama wa taifa wa kikweli? je? hili la usalama wa taifa linajadilika kikatiba?

 

wapi? ulikosomea masters Rukwa? walikueleza reference za net hazifai?? inaonekana bado haukumuelewa mwalimu wako mkuu........muulize tena!!! wengine tunafundisha vyuo vikuu humu!
 
Huwezi kuimarisha ulinzi wakati watu wanaingia nchini kiholela ati kwa sababu tu ni member wa EAC. Subirini matokeo yanakuja very soon.

Ongezea..........Wanaingia kiholela na kuchukua passport yetu kama njugu vile............we are so lousy kwenye suala la immigration.........na tunadharaulika sana Kimataifa kwenye hili suala la immigration...............
 
mkuu ni utaratibu gani unaotumika kuwapata hao majasusi?

 

TISS yetu ya TZ inafanya kazi kwa maslahi ya:
1. Wawekezaji walioko na wanaotaka kuiba mali za watanzania
2. Wanasiasa wanaofanya kazi kwa maslahi yao.
3. CCM na Wezi wengine nchi hii, Ndiyo Maana kina Kombe waliuawa
 
Mbona wamerakani walienda kumchukua Osama Bin Laden na kumuua bila ya wao kujua??? Je CIA taarifa walizipata wapi? Hebu jifunze kuunganisha dots bana!

UNA UHAKIKA GANI KUWA HAWAKUJUA MKUU! Wao ndo walikuwa wanamlea na ndo wao walowapatia wamarekani kwa makubaliano kuwa wahakikishe anauwawa.
 
wapi? ulikosomea masters Rukwa? walikueleza reference za net hazifai?? inaonekana bado haukumuelewa mwalimu wako mkuu........muulize tena!!! wengine tunafundisha vyuo vikuu humu!

Rukwa? Nina MBA kaangalie chuo cha 4 africa kwa ubora kwa MBA na cha kwanza Tanzania ndiko nilikosomea mimi....
 
mkuu ni utaratibu gani unaotumika kuwapata hao majasusi?

Big up man. Kinachoendelea sasa ni kwamba vijana wengi wanaohudumia idara yetu nyeti wanapoteza maadili kidogo but they are doing good job. Watu wanalaumu tu lakini lazima wajue bila hiki kikosi tusingekua tuonaongea hapa kwani uslama wetu usikingekuwepo kutokana na maadui wa nje na ndani ya nchi yetu. Wakati wa Mwalimu na mpaka sasa jukumu la usalama wa nchi yetu ni wetu sote na si kusema eti idara ya usalama haifanyi kazi.

Ukiona usalama wanchi unayumba basi ujue sisi wananchi(raia) hatufanyi kazi ya kulinda nchi yetu. Usama wa awali juu ya maadui zetu ni wewe mwananchi, ukiona mtu anaihujumu nchi yetu na wewe hutoi taarifa kwa vyombo vya usalama, then wewe mwananchi umehusika kuingamiza nchi yetu japo utailaumu idara husika.

Ushauri wangu wananchi wezangu sote tuilinde nchi yetu kwa kushirikiana na vyombo husika. Sote tupo kwenye meli moja waliochini wakiamua kutoboa meli wasifikirie ikizama utawalaumu watoboaji, maana yake ni kwamba ukiona mtu anatishia usalama wa raia mwenzako au wa nchi yetu aidha kwa tamaa zake au kutokujua na usitoe taarifa basi jua hata wewe umehusika kuliangamiza taifa. Tuwe wazalendo wa nchi yetu, tuache kulaumiana.
Mungu ibariki Tanzania.
 
wapi? ulikosomea masters Rukwa? walikueleza reference za net hazifai?? inaonekana bado haukumuelewa mwalimu wako mkuu........muulize tena!!! wengine tunafundisha vyuo vikuu humu!

Hakika hakumwelewa. Hata mimi ukiniletea references za google.com au wikipedia.com,nitakutimulia mbali.
 
hii iko conc sana hebu tuone wadau wanasemaje?japo naweza amini kwani niiliwahi kuwa kule kipindi cha uchaguzi walisema hawana nia na muungano kwani hata nyanya walikua wanapata za kopo toka arabuni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…