SoC01 Tunahitaji miundombinu bora ili kujikwamua kiuchumi

SoC01 Tunahitaji miundombinu bora ili kujikwamua kiuchumi

Stories of Change - 2021 Competition

ItsMi

Member
Joined
Sep 13, 2021
Posts
66
Reaction score
31
Miundombinu ni daraja la maendeleo.

kama tunavyoelewa kwamba Miundombinu Ni jumla ya nyenzo kuu ambazo zinaleta maendeleo katika jamii nzima tunapizungumzia miundombinu tunagusia vitu mbalimbali ikiwemo mawasiliano, maji, barabara, hospitali, majengo, usafiri, umeme, shule, madaraja na vinginevyo vingi Hivyo kwa ujumla wake ni msingi wa maendeleo ya taifa.

Lakini hasa mada yetu ya leo inalenga moja kwa moja miundombinu ya barabara katika namna fulani ya kuinua pato la nchi na kuchochea maendeleo kiujumla, Sasa kumekuwa na changamoto kubwa kwa barabara ndani ya nchi yetu ambapo barabara zinajengwa kwa kiwango cha chini na wakati mwingine hata yawezekana zisijengwe swala ambalo linarudisha nyuma maendeleo ya taifa.

Tatizo jingine ni kwamba barabara hizohizo zilizojengwa kwa kiwango cha chini unakuta mara baada ya miezi mitatu au minne barabara inaanza kulika na kubaki na mashimo njia nzima Jambo ambalo linakuwa kero hasa kwa usafirishaji na wasafiri kwa maana inachochea uharibifu wa vyombo vya moto kiujumla japokuwa kumewekwa taratibu kwa wizara husika kwamba zinatakiwa kuhahakikisha kwamba mashimo yanayojitokeza barabarani yaweze kuzibwa kwa muda mfupi lakini haipo hivyo kama ilivyopangwa kwa kuwa unaweza kuona mashimo hayo yamekaa takribani hata kipindi cha wiki kadhaa katika mwezi hivyo hii ni changamoto kubwa.

Pia upungufu wa barabara katika maeneo mbalimbali... na pia swala ambalo linapelekea foleni kubwa katika maeneo ya miji mikubwa hivyo pia tunaiomba serikali ijaribu kulitazama hili swala kwa ukaribu zaidi.

Pia wengi tujuavyo ni kwamba Usafirishaji ndio mhimili mkuu na nguzo imara kwa maendeleo kwa nchi nyingi zilizoendelea kwa sababu uwepo wa usafirishaji utaruhusu Marighafi kutolewa mashambani na kupelekwa viwandani kwa lengo la uchakatwaji kuchochea uzarishaji wa bidhaa na hatimae kuzisambaza bidhaa hizo ndani na nje ya nchi yaani (exporting) swala litalopelea ongezeko la pesa za kigeni halafu pia Kuchochea maendeleo ya nchi na kujitangaza kimataifa kupitia bidhaa hizo na kujiongezea mapato mbalimbali.

Miundombinu nzuri za barabara na mawasiliano zitasaidia kuimarisha mahusiano kati ya nchi yetu na nchi zingine pia miundombinu nzuri itaweza kuruhusu kiwango kikubwa cha uzalishaji wa bidhaa na hatimaye kujiimarisha zaidi kwenye maswala mazima ya kiuchumi.

Kwa hivyo mara baada ya kuyajua hayo mambo yanayoweza kusaidia kuinua uchumi wa nchi yetu, Sasa ningeliomba serikali yetu inayoongozwa na mheshimiwa mama samia suluhu hassan. Kwamba iweze kulitazama jambo hili kwa makini na kulipa kipaombele kwa hakika mara baada ya hapo tutasonga mbele na kuweza kuwaacha nyuma wale wote walionekana kuwa mbele yetu. Na ndiyo sababu siku zote ili kujikwamua kiuchumi tunahitaji miundombinu bora.

Nitumaini langu kwamba Jambo hili litawezekana lakini pia tukimtanguliza mungu wetu mbele kabla ya jambo lingine lolote.

Asante kwa muda wako kwa kuifuatilia mada hii,uwe na usomaji mwema
 
Upvote 1
Back
Top Bottom