Huu ndio ufukunyuku ninaoukataa toka kwa waajiri. Jitu linasokomoka huko na kuagiza mtu aliyesoma OXFORD. Sasa kuna degree ya Mweka ambayo vyuo vingine hawatoi? Unataka competence au Jina la Mweka?
Haya basi kama haitoshi, unataka tu mtu aliyesoma Mweka, kusoma nini? Pale kuna kozi nyingi? Kwa jinsi ulivyoandika huu ufwanyaya hapa, mtu mwenye akili zake atajua unataka mtu aliyesoma mweka labda umuulize kitu kuhusu mazingira ya pale au kuna demu ulimwacha akiwa mfagiaji kwa hiyo unataka kujua hali yake.
Tayari mpk hapo SITUMI. Kama mambo mengine yako blah blah namna hii mshahara utapatikana kwa wakati kweli? Kuna kazi au tunaenda kukaa kwenye meza tukipiga story? Hakyanani sina ajira lkn ya kufanya na watu wa namna yenu hapana.