Bongolander
JF-Expert Member
- Jul 10, 2007
- 5,067
- 2,210
Kwa mara nyingine tena katika historia ya michezo Tanzania, limerudi tena jambo la ajabu na la kijinga, la watu wasio na utaalamu wowote na soka kuongelea soka bila kujua hasa ni nini wanaongelea. Hali hii imekuwa inajirudia na kujirudia kila timu yetu inapokuwa kwenye michezo ya kimataifa.
Kuna baadhi ya watu, kwa sababu tu ya kuwa karibu na michezo kwa njia moja au nyingine, iwe ni utangazaji wa mechi za soka, iwe ni uongozi fulani kwenye michezo, au hata uandishi wa habari za michezo, wanajifanya wajuaji kiasi hata cha kudiriki kukosoa mambo ya kiufundi kana kwamba wanayajua … lakini ukweli ni kwamba hata elimu ya msingi ya ufundi wa soka hawana, mbali ya hata kutowahi kuchezea timu ya shule.
Juzi nilimsikia mtu mmoja akimponda Kocha Emmanuel Amunike kuwa hana kiwango (Kama huko nyuma alivyokuwa akimponda kocha kutoka Brazil). Vigezo alivyotumia kukosoa ni vyepesi ambavyo mtu mwenye akili hawezi kuvikubali (eti kuwa hata mtu mmoja wa Nigeria alisema Amunike hafai). Alikuwa wapi kusema haya huko nyuma na akasubiri hadi stars ifungwe ndio aseme? Lengo hasa ni nini?
Sababu ya pili aliyotaja ni kuwa pesa wanayopewa vijana wa taifa stars $100 ni ndogo sana ikilinganishwa na bajeti ya dola milioni 13 waliyowekewa Senegal. Sijui kama alikuwa anamaanisha ukiwa na hela nyingi ndio utashinda na ukiwa na kidogo utashindwa. Nakubali kuwa $100 ni kichele, ingekuwa vizuri vijana wetu wakilipwa zaidi. Lakini kama hukujipanga kiufundi toka zamani hata ikiwa $1000 au $10,000 kwa siku, itakuwa nguvu ya soda tu. Pesa ni sababu moja tu kati ya sababu mtambuka. Marekani, China, Japan wana hela sana na bajeti zao kwenye soka ni kubwa sana, mbona wanatandikwa na timu ambazo bajeti zao ni ndogo? Sijui hili anaweza kulieleza vipi.
Amekosoa uchangiaji wa harambee uliofanywa na wabunge. Kwa maoni yangu ni kuwa wabunge wameonyesha uzalendo, tunatakiwa kuwapongeza. Pesa za timu ya taifa zinatakiwa kutolewa na serikali, sio wabunge, lakini wabunge kujitolea pesa mfukoni ni uzalendo mkubwa unaotakiwa kupongezwa na sio kubezwa. Huyu jamaa ni mbunge sasa sijui ni kwanini huko bungeni hakusimamia suala la kutenga fedha kwa ajili ya timu ya taifa, na kuamua kukosa harambee.
Spika wa bunge letu aliongea vizuri sana kuhusu physique ya wachezaji wetu. Kuna kitu kimoja alisema kuwa vijana watu wanatakiwa kuimarika, yaani wajengwe hata kwenye maswala ya lishe ili waweze kushindana vizuri. Ukiangalia mara ya mwisho timu yetu iliyokuwa kwenye fainali za Kombe la mataifa huru ya Afrika na ya sasa, jaribu kuangalia tofauti ya average height, weight, speed, endurance and physique, then you will understand what he meant. Ingawa na yeye sio mtaalamu wa soka, alichosema tulikiona kwenye luninga zetu. Hakukosoa alishauri na kupendekeza.
Lakini ingekuwa ni vizuri sana kama watanzania tungekuwa na japo watu wawili ambao ni authority kwenye soka, ili wakiongea kuhusu soka tuwaelewe. Kwa sasa kuna ombwe kwenye eneo hilo.