Shayu
Platinum Member
- May 24, 2011
- 608
- 1,655
Elimu ya uzalishaji mali na utoaji huduma ni sehemu ndogo sana ya maarifa lakini maarifa yaliyo makubwa ni jinsi gani watu wetu watakuwa na uwezo wa kuishi kwa pamoja na kujenga mahusiano yaliyo mema miongoni mwao kwa kufanya hivi taifa letu litakuwa na uwezo wa kubaki muda mrefu na kukua kwasababu bila kutengeneza elimu itakayojenga mahusiano yetu kama watu wa taifa moja hatutaweza kufika popote.
Ni Elimu hii ambayo itatujenga kuwa na mwelekeo mmoja kama taifa badala ya kuwa watu wa taifa moja wenye mielekeo tofauti. Ni lazima kuwe na kitu kilichotuunganisha kama Taifa na kutufanya tuwe na mwelekeo mmoja na elimu tunayoitoa iwe yenye msaada kwa huko tunakotaka kwenda kama taifa kwakuwa kama elimu yetu haitaelekezwa katika mkondo fulani bali tukawa tunazalisha tu watu na kuwaacha, elimu hii haitasaidia kitu. Ni lazima tutengeneze mkondo na tuzalishe watu ili wafuate mkondo huo na sio kuzalisha watu na kuwatupa hii ni sawa sawa na kupanda mbegu bila mpangilio mzuri shambani.
Elimu yetu isiwe tu kwaajili ya kufanya watu wapate ajira na kupata mlo wa kila siku bali iwe ni sehemu ya mkakati wa kulifikisha Taifa hili sehemu fulani. Kwasababu sisi kama watanzania kuna sehemu fulani lazima tufike kwa pamoja, kuna sehemu tunataka kwenda na hatutafika kama muundo wa elimu tunayoitoa utakuwa haujapangiliwa kutufikisha huko.
Sisi kama Taifa ni lazima tuwe na mwelekeo hili haliepukiki ni lazima tuwe na sehemu miongoni mwa Mataifa. Haiwezekani tukawa tunatengeneza wasomi na elimu yenye mlengo wa manufaa binafsi badala ya ukombozi wa Taifa hili si sahihi na hatutakuwa na mwelekeo kama taifa kama tutakuwa na aina hii ya mawazo. Tunahitaji ukombozi mpya wa fikra utakao tuweka huru na kujitambua kuhusu utaifa wetu na umoja wetu. Tunahitaji mwelekeo na dira Sasa!