Tunahitaji nini kutoka kwa Vyama mbadala?

Tunahitaji nini kutoka kwa Vyama mbadala?

mwaimu Jt

JF-Expert Member
Joined
May 7, 2017
Posts
878
Reaction score
429
Ndugu wanabodi salaam,

Kama tujuavyo kwa sasa tuko katika Msimu wa Siasa za Uchaguzi, lakini nimekuwa nafuatilia sana baadhi ya mikutano ya kampeni inayofanywa na wagombea mbali mbali waliotia nia kugombea hasa nafasi ya Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, naomba kuweka wazi mikutano mingi nilivyofuatilia ni ya hawa wagombea wa vyama vinavyoonekana kuwa na wafuasi wengi ndani na nje ya nchi.

Kilichonisukuma kuja kwenu ni tafakari niliyobaki nayo na ambayo imenipelekea kuwa na maswali, Je tunachohitaji Watanzania ni mgombea atakayekuwa na dhamira ya dhati ya kuondoa matatizo na changamoto tulizokuwa nazo katika jamii na nchi yetu kwa ujumla au tunahihitaji mgombea mwenye dhamira ya kutaka kupambana tu na Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli?

Wasalaam
 
Hakuna jambo jema kipindi hiki kama kuondokana na huyu nduli amefanya unyama mkubwa sana kwa watu.
 
Tatizo upinzani haujajiandaa kushika nchi
Lisu huko bitter na Magufuli as a person anasahau kuwa uchaguzi nini ni kukipigania Chama kishike dola sio kujipigania mwenyewe
Yeye vita yake ni na Magufuli hivi haimsaidii sababu Magufuli kabebwa na Chama na wanachama personal attack zake hazimuongezei kuwa

Alizoea siasa za personal attack za enzi za Kikwete sasa hivi kumebadilika watanzania sio wale wa kutukana mtu halafu wanakupigia makofi!!
 
Raisi: Tundu Lisu

Makamu : Salumu mwalimu

Waziri mkuu : Mbowe

Waziri wa miundombinu: Mnyika

Waziri wa michezo : Sugu

Waziri wa fedha : Lema


Kwa safu hiyo si dhani kama hi nchi itakuwa salama

Na Mbowe atataka yeye ndio awe final say
 
Watanzania wanataka maendeleo sio kulia lia ili upate huruma ulipe kisasi , tunataka sera sio matusi.
 
Back
Top Bottom