Tunahitaji Raisi kama Traore wa Burkinafaso sio madikiteta

Mzalendo2015

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2012
Posts
7,225
Reaction score
9,830

View: https://youtu.be/vtxezmGOgQI?si=MUyi4Mzqdi4Mnb-v
Sikiliza kilichotokea kwenye kikao cha Viongozi wa AU kule Addis Abeba. Rais kijana mwanapinduzi bila kupepesa macho wala unafiki alimlipua Rais Rutto wa Kenya kuhusu mauaji ya Gen Z huko Kenya.

Aliiungwa mkono na Cyril Ramaphosa wa A. Kusini ukumbi ukabaki unazizima. Tanzania iliwakilishwa na Mhe. Mpango akabakia kukodoa mimacho tu.Nilitamani sana aizungumzie Tanzania kwa ukandamizaji wa Demokrasia, Haki za binadamu kwa utekezaji na mauaji ya wapinzani.
 
Wananchi tutafurahi sana tukimpata rais wa aina hiyo... Uchumi wetu utainuka speed sana
 
Tuwatoe CCM kwanza tusije kusingizia wengine tatizo ni sheria mbovu
Kila Mtz amemsikia Polepole ambacho CCM wamekuwa wanakifanya kubakia madarakani. Ni wakti wa Watz kuondoa tongotongo na ujinga tulonao. NO REFORMS NO ELECTION SIYO UHAINI TENA BAALI NI UHALISIA.
 
Tuwatoe CCM kwanza tusije kusingizia wengine tatizo ni sheria mbovu
na katiba ikarabatiwe. Pia kiukweli Kenya walijaribu kuifuata serikali ya ccm, ambayo inatumia vitisho kama kuua katika kutekelea matakwa ya wahuni. Mfano kutupa watu virobani au maporini
 
Kwenye madaraka akiingia yeyote atataka ajaze tumbo lake na wa karibu yake. Weka kumbukumbu huu ujumbe wangu utaukumbuka siku moja
 
na katiba ikarabatiwe. Pia kiukweli Kenya walijaribu kuifuata serikali ya ccm, ambayo inatumia vitisho kama kuua katika kutekelea matakwa ya wahuni. Mfano kutupa watu virobani au maporini
Baada ya Bomu la Polepole bila shaka Watz wataelewa sasa maana pale CHADEMA wanaposema NO REFORMS NO ELECTION.
 
Kwenye madaraka akiingia yeyote atataka ajaze tumbo lake na wa karibu yake. Weka kumbukumbu huu ujumbe wangu utaukumbuka siku moja
Kaka usifkiiri hii nji kila mtu ni FISADI kama madikiteta wa CCM!! Ndo maana hawa madikteta wameamua kuunda mifumo ya KUBAKI MADARAKANI ili kuficha maovu yao. Wanajua siku wakitolewa Ikulu kitanuka!!
 
Kwenye madaraka akiingia yeyote atataka ajaze tumbo lake na wa karibu yake. Weka kumbukumbu huu ujumbe wangu utaukumbuka siku moja
Hii ni miongoni mwa zile jumbe za kipu.mbavu zinazolenga kuwakatisha watu tamaa wanapopigania mabadiliko! Kama ishu ni kujaza matumbo sasa si wapewe na wengine wajaze ya kwao kwa nini wawe ni walewale kana kwamba nchi ni mali yao!
 
Kaka usifkiiri hii nji kila mtu ni FISADI kama madikiteta wa CCM!! Ndo maana hawa madikteta wameamua kuunda mifumo ya KUBAKI MADARAKANI ili kuficha maovu yao. Wanajua siku wakitolewa Ikulu kitanuka!!
Sawa mkuu
 
Hii ni miongoni mwa zile jumbe za kipu.mbavu zinazolenga kuwakatisha watu tamaa wanapopigania mabadiliko! Kama ishu ni kujaza matumbo sasa si wapewe na wengine wajaze ya kwao kwa nini wawe ni walewale kana kwamba nchi ni mali yao!
Sawa mkuu
Ila tupunguze mihemuko
 
Hivi ni ukilewa usichati au ukichati usilewe?

Kwamba Traore sio dikteta? alipigiwa kura na nani?
 
2Hivi ni ukilewa usichati au ukichati usilewe?

Kwamba Traore sio dikteta? alipigiwa kura na nani?
Unajua maana ya dikteta ww au unapayuka?
Kama Watawala wa kiraia wamepoka madaraka kwa Raia na hawataki kusikia habari ya demokrasia, uhuru na haki kwa Wananchi,ni bora Watu km kina Traore watwae madaraka ili wawanyooshe wanasiasa uchwara.
 
Hivi ni ukilewa usichati au ukichati usilewe?

Kwamba Traore sio dikteta? alipigiwa kura na nani?
Haya na wewe tuambie CCM na Mafisadi wake wanapigiwa kura na nani?? Unless hujamwelewa Polepole au hujamsikiliza. Pole sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…