SoC03 Tunahitaji Taasisi maalumu itakayojihusisha na tafiti zinazofanyika vyuoni

SoC03 Tunahitaji Taasisi maalumu itakayojihusisha na tafiti zinazofanyika vyuoni

Stories of Change - 2023 Competition
Joined
Apr 19, 2023
Posts
77
Reaction score
124
Maadui wa Tanzania ni ujinga. Umaskini, na maradhi; kama ilivyosemwa na hayati Mwalimu J.K. Nyerere.
Serikali wakati wote inafanya kila namna ili kupambana na hawa maadui watatu.

Elimu ni nguzo kuu, tena nguzo namba moja katika kupambana na hawa maadui watatu wa taifa la Tanzania. Ni wazi kuwa, lengo kuu la elimu ni kumsaidia aliyeipata kuweza kuyamudu mazingira yaliyomzunguka Pamoja na kupambana na changamoto zilizozunguka mazingira hayo.

Na hii ndio sababu tunawaajiri walio na elimu katika suala husika kwani wana maarifa ya kuleta matokeo tunayoyahitaji Pamoja na kuzitatua changamoto zinazoambatana na suala husika.

Lakini Zaidi sana hii ndio sababu katika ngazi ya elimu ya juu yaani ngazi ya chuo kikuu, wanafunzi hufanya tafiti katika mambo yanayohusiana na programu anayosoma hapo chuoni. Mfano anayesoma uchumi atafanya utafiti katika jambo lolote linalohusiana na uchumi.

Tafiti hizi huwa zimelenga kuibua changamoto zilizopo katika jamii katika Nyanja husika ambayo mwanafunzi anasoma na mwisho mwanafunzi atakuja na suluhisho la tatizo husika ambalo amelifanyia utafiti. Na hii inakuwa ni sehemu ya matokeo yake katika kupata shahada yake.

Kama mwanafunzi ameshindwa kuona changamoto hata moja katika changamoto zote zilizopo tatika jamii yake na kutafiti njia ya kuitatua changamoto hiyo, basi hakuna kitu elimu yake imemsaidia na hii ndio sababu atashindwa kupata hiyo shahada yake.

Kila chuo kilichosajiliwa na serikali huahikikishwa ubora wake katika utendaji kazi na ndio maana kitaendelea kutoa elimu. Hivyo utafiti wowote ambao chuo kimesimamia na kimeidhinisha kuwa huu ni utafiti sahihi kwani umelenga kweli kutatua changamoto inayoikabili jamii husika, na umetoa majibu sahihi basi utafiti huo unaweza kutumika katika jamii husika kwa ajili ya kutatua changamoto hiyo.

Vyuoni kuna idadi kubwa sana ya tafiti ambazo zimefanyika, kwani kila mwaka tafiti hizi hufanyika na kuidhinishwa na chuo husika na watu hupewa shahada zao.

Sasa kama tafiti zinalenga kuibua changamoto zilizozunguka jamii na kuziletea suluhisho, hii ni kumaanisha kuwa kuna changamoto nyingi sana Pamoja na suluhisho ambazo zimefungiwa ndani ya makabati kule vyuoni katika vile vitabu vya tafiti vilivyoko humo.

Na hapo lengo halisi la kuwepo elimu linakuwa limekufa kama matatizo yamebainika na suluhisho la hayo matatizo likapatikana pia lakini bado vyote viwili vikatunzwa mahali bila kufuatia utekelezaji.

Kuna wachache ambao tafiti zao huja kutumiwa na baadhi ya makampuni binafsi au serikali kwa ajili ya kutatua changamoto husika, lakini bado kuna namba kubwa ya tafiti huachwa vyuoni na kutunzwa makabatini bila utekelezaji wowote.

USHAURI WANGU;
Serikali ingeanzisha moja kwa moja taasisi maalumu itakayojihusisha na masuala ya tafiti vyuoni au iongezee majukumu taasisi fulani kwa ajili ya kujihusisha na hizi tafiti za vyuo, ambapo taasisi hiyo itajihusisha na kuchukua tafiti zilizokuwa bora kwa mwaka na kwa kila chuo na kuhakikisha zimefikishwa sehemu husika kwa ajili ya kutendewa kazi.

Na kwa sababu tafiti ni mali ya chuo, serikali kupitia tasisi husika itapaswa kufanya mazungumzo ya namna ya kuliweka hilo sawa ambapo kila mmoja atanufaika kwa namna yake; serikali, chuo Pamoja na mwanafunzi.

Sio sawa kuwa na mrundikano wa tafiti nzuri zilizobaini matatizo/ changamoto za watanzania Pamoja na suluhisho kwa changamoto hizo makabatini huko vyuoni ili hali bado tuko katika janga la hawa maadui watatu wa taifa

Taasisi itajihusisha na yafuatayo;

1.Kuchukua tafiti hizi na kuzipeleka wizara au idara husika katika serikali kwa ajili ya utekelezaji wake. Kila mwaka inapitia katika vyuo vikuu vyote Tanzania na kuangalia tafiti ambazo zilikuwa bora kwa huo mwaka na zinatatua moja kwa moja matatizo/ changamoto za mtanzania. Na kila mwaka itapaswa kutoa taarifa ya idadi ya tafiti zilizochukuliwa kwa kila chuo na ni tafiti zipi hizo.

2.Kufuatilia utekelezaji wa tafiti hizo na kutoa taarifa kila mwaka

3.Itashirikiana na taasisi zinazohusika na mambo ya utafiti kama COSTECH ili kutimiza vyema majukumu yake maana hii yenyewe itahusika na tafiti za vyuoni tu.

Hii itasaidia yafuatayo

1.Lengo la kila utafiti kupeleka majibu sehemu husika litakuwa limetimizwa

2.Itatia hamasa kwa wanafunzi kufanya tafiti zilizo bora Zaidi kwani wana uhakika wa hatima ya tafiti zao.

3.Uhakika wa nafasi ya ajira kwa mwenye utafiti husika, kwani atahitajika ili kukamilisha kile alichokianzisha

MUHIMU: 1 Utaratibu huu wa serikali kuchukua hizi tafiti usikibane chuo kuruhusu hizi tafiti kwa wawekezaji wengine binafsi au vyovyote endapo chuo kitaona kinamaslahi na hilo au kuwa na maslahi Zaidi kwa mwanafunzi kwani lengo ni tafiti kuleta majibu kwa jamii kama ilivyokusudiwa na linakuwa limetimia.

MUHIMU: 2 Taasisi hii sio kwa ajili ya tafiti za kisayansi tu bali ni katika Nyanja zote; uchumi, siasa, Sanaa, michezo, burudani, n.k
 
Upvote 0
Back
Top Bottom