BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,165
Tunahitaji vyombo jasiri vya habari - Sitta
Mwandishi Wetu Disemba 10, 2008
Raia Mwema~Muungwana ni vitendo
SPIKA wa Bunge, Samuel Sitta, hivi karibuni alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa Mfuko wa Vyombo vya Habari Tanzania, katika ukumbi wa Karimjee, Dar es Salaam, shughuli iliyohudhuriwa na wadau mbalimbali wa habari nchini. Pamoja na mambo mengine alizungumzia hali ya nchi ilivyo kwa sasa na alianza kwa kusema;
MWAKA jana mwanahabari wa Ulaya aliyebobea Winters Negbenebor, katika makala yake: Globalization, Independent Media and Development in Africa: Theatre of the strong and the mighty; aliandika yafuatayo kuhusu vyombo vya habari katika Afrika:At this point, it is very evident that Africa needs nothing more than a better and more democratic media system for its growth and development. Only an African press genuinely committed to the freedom of the media, respect for human rights, respect for peoples welfare and development can bridge the gap and sail Africa to the much desired promised land. A Better Media. A Better Africa.
Maneno haya yanatukumbusha ukweli mzito kwamba kwa kwetu Afrika taaluma ya uanahabari haina budi kuzingatia safari yetu ndefu na ngumu ya kuleta maendeleo ya kweli kwa watu wetu. Kwa hiyo, naushukuru uongozi wa Mfuko wa Vyombo vya Habari Tanzania kwa kunialika kujumuika nanyi katika tukio hili muhimu kwa nchi yetu la kuzindua Mfuko wa Vyombo vya Habari.
Nawashukuru pia kwa heshima mliyonipa ya kuwa Mgeni Rasmi kwenye hafla ya uzinduzi wa Mfuko huo ambao una lengo la kuimarisha sekta muhimu ya habari hapa nchini Tanzania.
Sekta ya habari nchini imekua kwa kasi katika kipindi cha miaka 10 iliyopita. Nimearifiwa kuwa hivi sasa kuna vituo vya redio 45 kote nchini, vituo vya televisheni 27 na magazeti 60. Hata kijijini kwangu Urambo tuna vituo viwili vyaCable television! Bado hapo hujahesabu blogs kama vile Jamii Forums, Michuzi blog nk.
Kupanuka huko kwa sekta ya habari kunaifanya Tanzania kuwa miongoni mwa nchi chache za Afrika zenye kiwango cha juu cha ukuaji wa sekta ya habari. Kwa baadhi yetu ambao ni wasomaji makini wa magazeti, hivi sasa, ukipenda kufanya hivyo unahitaji zaidi ya saa tatu kuyapitia magazeti yote.
Katika hafla hii nimeona vema nizungumze nanyi masuala manne yafuatayo: -
Sekta ya habari na Maendeleo ya Nchi;
Uandishi bora wa habari na unaozingatia maslahi ya nchi;
Serikali na Vyombo vya Habari;
Changamoto mbalimbali.
Sekta ya Habari na Maendeleo ya Nchi:
Sekta ya habari ina mchango mkubwa sana katika maendeleo ya nchi hususan nchi masikini kama Tanzania. Mbali na kuelimisha jamii kuhusu masuala mbalimbali, vyombo vya habari husaidia kufichua vitendo vinavyokwamisha maendeleo ya nchi kama vile ufisadi, rushwa katika utawala, matumizi mabaya ya madaraka, huduma mbovu kwa wananchi, ubadhirifu wa mali ya umma nk.
Tunayo mifano mingi nchini ambapo vyombo vya habari kwa ujasiri na bila woga vimekuwa mstari wa mbele katika kufichua maovu. Nawapongeza kwa dhati kutokana na mchango wenu wanahabari wa kupambana na maovu nchini kwa ujasiri mkubwa.
Aidha, vyombo vya habari pia huchangia kuwepo uwazi na uwajibikaji (transparency and accountability) katika utawala ambavyo ni msingi muhimu wa utawala bora. Ni dhahiri kuwa kuna uhusiano wa moja kwa moja baina ya maendeleo ya nchi na uimara wa sekta ya habari katika nchi husika. Nchi nyingi masikini, hususan katika Afrika, zina mifumo na sheria ambayo inagandamiza uhuru wa vyombo vya habari.
Kwa mfano hapa kwetu Tanzania kwa yeyote mwenye mtazamo chanya atabaini kwamba Sheria ya Magazeti (1976) imepitwa na wakati. Natoa wito kwa Serikali kuharakisha kufikisha bungeni Muswada wa Sheria mpya ya Habari itakayolingana na hali ya sasa.
Nachukua fursa hii kuupongeza uongozi wa Mfuko wa Vyombo vya Habari kwa kubuni wazo la kuanzisha chombo hiki. Aidha, nawashukuru wahisani kwa kujitolea kugharamia Mfuko huu kwa kipindi cha miaka mitatu ya mwanzo.
Uandishi bora wa Habari na unaozingatia Maslahi ya Nchi:
Kila nchi ina maslahi yake (national interests) ambayo hufafanuliwa kwenye Sera ya Mambo ya Nje ya nchi husika. Ni maslahi haya ambayo huitofautisha nchi au jamii moja na nchi nyingine. Ni kwa msingi huo, Tanzania ya Nyerere ilijengwa katika misingi inayozingatia usawa, udugu, uadilifu, kuwajali wanyonge na kutowabagua watu kwa misingi ya rangi ya mtu, dini yake, kabila lake, eneo analotoka au jinsia yake.
Ni misingi hii ambayo imetufanya tuendelee kuwapo kama Taifa moja lenye umoja na mshikamamo katika kipindi cha miaka 47 ya Uhuru wetu. Ni misingi hii ambayo imejenga taswira ya Watanzania kuwa ni watu waungwana, wamoja na wenye utamaduni wa ushirikiano na ukarimu.
Hata hivyo, katika miaka ya hivi karibuni kumekuwapo vitendo, kauli, mitazamo ya baadhi yetu kuashiria mwelekeo wenye nia ya kuibomoa misingi hii kupitia kwenye vyombo vya habari. Vyombo vya habari ni mojawapo ya nyenzo inayotumiwa na watu hawa.
Si kazi ngumu kuvitambua vyombo hivi vichache vya habari kwani vinajidhihirisha waziwazi kwa kuandika habari za uchonganishi, uzushi na kueneza hisia za chuki na utabaka. Mfano mmoja wa habari za uchonganishi ni pale ambapo mwandishi anapotosha hoja au taarifa kwa makusudi na anaamua kujenga hoja juu ya msingi huo alioupotosha!
Hii ni tabia moja mbovu mbovu ambayo hutumiwa na waandishi wasio waadilifu kwa lengo la upotoshaji yaani kupotosha nukuu ama unavyomnukuu kiongozi na kisha kujenga hoja juu ya upotoshaji ulioufanya mwenyewe.
Kwa mfano, Agosti mwaka huu nilipotamka kule bungeni kwamba mizania ya haki za binadamu hapa nchini imeegemea kuwalinda zaidi wahujumu uchumi wakubwa, mwandishi wa gazeti moja lenye mwelekeo wa kutetea mafisadi alipotosha kuwa mimi ni mwanasheria nisiyejali haki za binadamu.
Nilichosema ni kwamba, haki za binadamu za mtu mmoja mmoja ambaye kwa vitendo vyake anahujumu mamilioni haziwezi kutazamwa bila kuzingatia haki za hao mamilioni. Ni wajibu wa nchi yoyote, na hasa nchi masikini, kuangalia kuwa haki za binadamu hazitoi mwanya:
Kujenga tabaka la watu maalumu ambao utaratibu wa kuwashughulikia unakuwa tofauti na watu wengine;
Wala rushwa wakubwa wanaohujumu uchumi wa Taifa kujisikia wana uhuru mpana wa kuendeleza maovu yao huku hali ya wengi ikididimia.
Hali hii isipodhibitiwa mapema itauvunja umoja na utengamano wetu na kutuingiza kwenye migawanyiko, machafuko na hatimaye hata vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Hatuna budi kuviimarisha vyombo vya habari makini vyenye nia njema na nchi yetu dhidi ya vichache vinavyotumiwa na waovu. Kwa hiyo, nimefurahi kusikia kuwa, lengo la Mfuko huu ni kuvijengea uwezo vyombo vya habari na wanahabari ili kuandika na kutangaza habari za kina, za ukweli, zilizofanyiwa utafiti na zinazoweka mbele maslahi ya nchi.
Kwa maneno mengine, Mfuko huu unaanzishwa ili kuijenga taaluma ya habari katika misingi ya uadilifu, kujali taaluma na ukweli. Nawashukuru na kuwapongeza wote waliofanikisha kuasisiwa kwa Mfuko huu ambao ni dhahiri utaipandisha juu zaidi fani ya habari nchini.