Tunahofia nini kurudia uchaguzi wa mabaraza?

Tunahofia nini kurudia uchaguzi wa mabaraza?

Dingswayo

JF-Expert Member
Joined
May 26, 2009
Posts
4,019
Reaction score
2,925

TANZANIA ipo kwenye mchakato wa kupata Katiba mpya inayotarajiwa kuwa suluhu ya upungufu wa Katiba ya sasa iliyotuongoza kwa miaka 51 baada ya uhuru. Mchakato wa kupata Katiba mpya umepita kwenye hatua mbalimbali ikiwemo kukusanya maoni ya wananchi, viongozi na raia wa kada na rika mbalimbali.

Hatua iliyopo sasa ni uundaji wa mabaraza ya Katiba ngazi ya kata nchi nzima. Mchakato wa kuwapata watakaounda mabaraza hayo umeingia dosari ambayo tusipoipatia ufumbuzi wa haraka tutakuwa kwenye hatari ya kupata bora Katiba badala ya Katiba bora.

Tunasema hivyo baada ya Mwenyekiti wa Tume ya Kukusanya Maoni ya Katiba Mpya, Jaji Mstaafu Joseph Warioba, kukiri kwamba utaratibu wa kuyapata mabaraza ya kata uligubikwa na rushwa, udini, siasa na mamluki.

Jaji Warioba alikiri kusikia malalamiko na kasoro zilizojitokeza kwenye kata karibu zote zilizofanya uchaguzi ule, lakini alisisitiza kwamba hayuko tayari kurudia, tume yake itaendelea na mchakato ule kama walivyojipangia.
"Hilo la rushwa lilikuwepo na hata mamluki kule kwenye uchaguzi, nilistaajabu kusikia watu wanahonga ili wachaguliwe kuingia kwenye mabaraza haya.

Licha ya kufahamu uwepo wa kasoro hizo, Jaji Warioba amegoma kurudia uchaguzi huo, amesisitiza kwamba tume inaandaa rasimu ya Katiba na kwamba inatekeleza wajibu wake kwa weledi mkubwa.

Kama Warioba anakiri kasoro kwenye mchakato huo, anakimbilia wapi kukamilisha Katiba mpya itakayokuwa na makosa?

Tunamshauri Jaji Warioba asiogope kuchelewa kupatikana kwa Katiba mpya, akubali kurudia uchaguzi wa mabara ya Katiba, safari hii kuwe na usimamizi wa kutosha ili kudhibiti matendo ya rushwa na uchochezi yanayofanywa na baadhi ya watu kwa maslahi binafsi au za vikundi au vyama vyao vya siasa.

Tunaamini kwamba Katiba tunayokwenda kuitengeneza itawaongoza Watanzania wote bila kujali tofauti zao hivyo tunahitaji kitu bora kwa faida ya wote wala si kukimbia kumaliza ili mradi iwepo Katiba hata kama ni ya hovyo.

Katiba bora itaandikwa na Watanzania wote, hivyo basi tuwakemee wanaopandikiza mamluki kwenye mabaraza ya Katiba ambao wamebeba mawazo ya wengine na kuzuia fikra pevu za wananchi wa kawaida kushiriki kwenye mchakato huo.

Katiba mpya ya Tanzania inatarajiwa kuwa tayari Aprili 26, 2014 wakati tunaadhimisha miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Lakini hiyo si hoja ya kutufunga kukimbilia kuhitimisha mchakato kwa tarehe hiyo kwani hata wenzetu waliotutangulia katika suala kama hili walitumia muda mrefu zaidi, sasa kwetu kuna nini kinakimbiliwa?
 
Mimi ni mwanaccm halisi,
hofu iliopo ni kwamba ccm tunaweza tusipate wawakilishi wengi kama mwanzo na hili linaweza kuwa pigo kwetu na kushindwa kupitisha mambo yetu kwani sasa hivi watu walishagundua kosa walolifanya. Nafikiri mmeelewa ahsante!
 
Kwani hao waliopita ni Wakenya msifanye katba ni ya Chadema.Katiba ni ya Watanzania hakuna upuuzi wa kurudia ili kukidhi matakwa ya Chadema.
 
Back
Top Bottom