Tunaishi kwa Kuamini Baleke ni Mwanasimba au Mayele ni Mwanayanga

bryan2

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2016
Posts
3,323
Reaction score
4,679
Mashabiki wa Tanzania [emoji1241] hakika ni watu wa maajabu bado tupo kwenye zile zama za kuamini Mayele ni mwanayanga au Baleke ni mwanasimba huu ni mfano mdogo.

Tunashindwa kutambua hawa ni waajiriwa kama waajiriwa wengine, hawa ni wafanyakazi wenye mikataba yao na wanalipwa hawapo pale kwa mapenzi yao.

Tumekua na kasumba ya kuamini mchezaji akishakuja Yanga au Simba basi huyo ni mwanachama la hasha tunakosea sana ndio maana mchezaji huyohuyo akitaka kwenda timu nyingine tunaanza kuumia au kumchukia mchezaji mwenyewe naye anatafuta malisho mazuri.

Ni Sawa na wewe leo upo Kampuni X ukipata dau kubwa unaenda Kampuni Y japo napo huku kuna baadhi ya mabosi hawapendi hasa kama ulikua productive, ni Sawa na mchezaji ukishindwa kufika terms zake na timu nyingine ikaja na terms nzuri zaidi ni haki yule mchezaji kwenda.

Mapenzi tumeyaona kwa Kina Steve Jerald wamechezea timu moja mpaka kustaafu au Giggs, Beckham David pamoja na Kuwa mpenzi wa Man utd bado alitoka na kwenda kutafuta malisho mazuri zaidi.

Sio ajabu leo Baleke akienda Azam au Yanga kwa imani zetu chafu hizi wapo wanaoweza kwenda hata wa waganga kumloga japo siamini katika haya.

Sidhani kama pale DRC [emoji1078] ukichezea Mazembe wewe ni mwanamazembe means huna ruhusa ya kusajili timu nyingine yoyote ile.
 
Mbona hueleweki? Au unataka ubalance story? Si useme tuu mashabiki wa Yanga hawaamini kama Mayele anaondoka wakidhani ni mwanaYanga mwenzao. Unazunvukazunguka mara baleke ya nini?
 
Mbona hueleweki? Au unataka ubalance story? Si useme tuu mashabiki wa Yanga hawaamini kama Mayele anaondoka wakidhani ni mwanaYanga mwenzao. Unazunvukazunguka mara baleke ya nini?
Ungeanzisha Uzi wako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…