madeinmusoma
JF-Expert Member
- Jan 7, 2014
- 324
- 387
Tunaishi kwenye dunia ambayo kila mtu anataka aonekane msafi na mtakatifu machoni mwa watu, hata kama usafi huo utagharimu furaha na Maisha ya wengine.
Kila mtu amekuwa na mamlaka na msemaji wa maisha ya wengine bila kujali na kujua kwamba ni kujibebesha mizigo mizito isiyo na faida kwake, lakini wanasahau majukumu yao kwa kuwa sasa wamekuwa busy na mambo ya wengine.
Watu aina hii hujiona wao ni wakubwa sana na wanajua mno kuliko wengine, Wao wanatamani washauri ila hawapo tayari kushauriwa. Wanatamani Dunia iwaze wanavyo waza wao bila kujua kwamba hata theluthi ya mambo ya Dunia wao hawayajui [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Nakushauri shusha hiyo mizigo ipunguze baki na mambo yako ndio mizigo inayokuhusu, Bahati mbaya sana hata mizigo yako unashindwa kushughulika nayo kwa kuwa macho yako yanawatazama wengine kupitia wewe, Hebu hiyo mingine waachie wenyewe
Kimsingi watu wameumbwa tofauti na kwa umaalum tofauti na kila mmoja yupo kwa mpango maalumu shusha hiyo mizigo.