Tunajali pesa show popote hata chooni - Patcho

Tunajali pesa show popote hata chooni - Patcho

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Msanii wa filamu nchini na Rais mpya wa FM Academia, Patcho Mwamba amefunguka kwa kusema haoni tatizo kwa bendi za muziki kutumbuiza katika kumbi za baa kwa kiingilio cha vinywaji kwa kuwa wanachoangalia ni pesa wanazolipwa.

pacho%201.jpg

Pacho ameeleza hayo kwenye eNewz ya EATV baada ya kuwepo na dhana kwa kipindi kirefu kuwa bendi zikiwa zinatumbuiza ni kujishusha hadhi kwa kuwa kiingilio chake kinakuwa ni kidogo mno huku wengine huweka vinywaji kama kiingilio getini.

"Nakwambiaje bendi ni kama daladala, tunahitaji mtu yeyote apande haijalishi ni mwehu, jini, mchawi, kinachoangaliwa ni nauli yetu tu"alisema Patcho.

Pamoja na hayo, Patcho aliendelea kwa kusema "Tumetoka juzi kwenye mbio za mwenge hakukuwa na kiingilio tulilipwa chetu tukaenda kwenye kukimbiza mwenge, kampeni zikifika watu wanaendaga bila ya kulipia kiingilio. Brand haiwezi kuuliwa kwa masuala ya vinywaji ni upotofu, sisi tukishakodiwa na tukipewa pesa yetu tunaenda kupiga hata kama chooni tutapiga si tumeshalipwa" alisisitiza Patcho.

Chanzo; EATV
 
Walishaambiwa atakayebaki mpaka mwezi wa kumi na mbili huko jijini basi yeye mwanaume!
 
Huyu jamaa alibebwa sana na marehemu Kanumba kama Kanumba angekuwa bado yuko mzima huwenda jamaa nae angekuwa mbali.
 
Muziki wa bendi hasa hizi zenye mahadhi ya kikongo aseee wana hali mbaya sana
 
Jamaa anahali mbaya, bendi zimebuma muvi zimebuma sa akimbilie wapi?
 
Patcho unachofanya sio billionea papa lemutuz hamumtaji kwenye nyimbo zenu au hatoi kitu
 
Msanii wa filamu nchini na Rais mpya wa FM Academia, Patcho Mwamba amefunguka kwa kusema haoni tatizo kwa bendi za muziki kutumbuiza katika kumbi za baa kwa kiingilio cha vinywaji kwa kuwa wanachoangalia ni pesa wanazolipwa.

pacho%201.jpg

Pacho ameeleza hayo kwenye eNewz ya EATV baada ya kuwepo na dhana kwa kipindi kirefu kuwa bendi zikiwa zinatumbuiza ni kujishusha hadhi kwa kuwa kiingilio chake kinakuwa ni kidogo mno huku wengine huweka vinywaji kama kiingilio getini.

"Nakwambiaje bendi ni kama daladala, tunahitaji mtu yeyote apande haijalishi ni mwehu, jini, mchawi, kinachoangaliwa ni nauli yetu tu"alisema Patcho.

Pamoja na hayo, Patcho aliendelea kwa kusema "Tumetoka juzi kwenye mbio za mwenge hakukuwa na kiingilio tulilipwa chetu tukaenda kwenye kukimbiza mwenge, kampeni zikifika watu wanaendaga bila ya kulipia kiingilio. Brand haiwezi kuuliwa kwa masuala ya vinywaji ni upotofu, sisi tukishakodiwa na tukipewa pesa yetu tunaenda kupiga hata kama chooni tutapiga si tumeshalipwa" alisisitiza Patcho.
Kusema kweli Patcho si mwanamuziki wala mcheza filamu ,hizi fani analazimisha tu sababu ya kuganga njaa na amshukuru marehemu Kanumba aliyekuwa anambeba tu,na kwenye muziki kazi yake akipanda jukwaani ni kutaja tu majina ya mapedeshee ili adakishwe kitu kidogo,hakuna cha muziki wala filamu hapo.

Chanzo; EATV
 
Patcho si mwanamuziki wala hajui hata kucheza filamu ni mtu anayelazimisha tu fani kwa muziki kazi yake ni kupanda jukwaani na kuanza kuwapaisha mapedeshee wa mujini ili apate kitu kidogo,na kwenye filamu bado anasafiria nyota ya Kanumba
 
Shikamoo Magu
Hawa wasanii nilikua nawaona kwenye tv ila kwa hali inavyoelekea ntakutana nao kwa mama muuza mihogo.
Wengine ntakutana nao banda la kuangalia mechi za mpira, nikilipa jero naangalia mechi na live band[emoji23] [emoji23]
Kuna wakati napenda uwepo wa mzee wa Makinikia
 
Back
Top Bottom