Tunajenga Madarasa 8000 halafu Nyumba za Walimu 0, hapa kuna shida mahali...

Tunajenga Madarasa 8000 halafu Nyumba za Walimu 0, hapa kuna shida mahali...

CK Allan

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2013
Posts
2,781
Reaction score
6,139
SERIKALI imetoa Sh bilioni 160 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa 8,000 vitakavyopokea ziada ya wanafunzi zaidi ya 400,000 wa Kidato cha Kwanza mwakani ambao ni zao la elimumsingi bila ada.

Aidha, Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Tamisemi, Dk Charles Msonde ameelekezwa kufanyia kazi malalamiko ya baadhi ya walimu walioajiriwa hivi karibuni ya kutolipwa posho ya kujikimu.

Haya yameelezwa jijini hapa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Innocent Bashungwa alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya kuwapokea wanafunzi wa kidato cha kwanza mwaka 2023.

Bashungwa alisema fedha hizo tayari zimeshaingia kwenye akaunti za shule za sekondari 2,439 zilizoainishwa kuwa na upungufu wa vyumba vya madarasa kwa ajili ya Kidato cha Kwanza mwakani.

Hii ni taarifa niliyochukua kutoka gazeti la habari Leo, yaani tunaongeza Idadi hiyo ya madarasa lakini Walimu ambao Ndio nguzo na msaada wa kukaa Karibu na hao wanafunzi Bado hatuwaweki kwenye bajeti!

Niwaambie tu faida za Walimu kukaa shuleni ni nyingi sana kuliko mnavyodhani!

Madarasa 8000 Nyumba za Walimu 0!

Lord have mercy
 
Nini cha muhimu zaidi, kwani kila mtumishi wa serikali anajengewa nyumba, watapanga tu, you cant do everything at ounce
 
Nini cha muhimu zaidi, kwani kila mtumishi wa serikali anajengewa nyumba, watapanga tu, you cant do everything at ounce
Kuna nyanja zinahitaji kuangaliwa kwa jicho na mtazamo tofauti ili kuleta matokeo chanya kwa upana !! Sekta ya Elimu sekta ya ikiwa ni mojawapo mbali ya sekta ya Afya.
 
Back
Top Bottom