bryan2
JF-Expert Member
- Jun 8, 2016
- 3,323
- 4,679
Juzi wakati mheshima Rais anahutubia jeshi la Magereza kuna kauli moja alisema kwa upande wa walinda Amani wetu I mean vyombo vyote vya Ulinzi 'MSIWEKEZE SANA KWENYE MIRADI YA UZALISHAJI MKASAHAU KAZI ZENU ZA KIMEDANI AKIMAANISHA ULINZI WA NCHI NA MIPAKA YETU' hapa rais aliona mbali.
Tanzania ni wahanga kwa yale yanayoendelea Ukraine tumeshawahi onja sulubu ya vita kumbuka vita vya Uganda pia scenario yetu sio tofauti sana na Ukraine kwani nasi ishu ya mipaka ilihusika baada ya kiongozi flani wa Uganda kudai sehemu ya nchi ya Tanzania pia Tunaona Urusi akidai baadhi ya sehemu za Ukraine kama vile Crimea, Donetsk na Donbas ni kweli inauma sehemu ya nchi kuchukuliwa mfano hai leo tu mtu akipunguza hata robo hatua ya ardhi yako lazima pachimbike.
Twende kwenye mada yetu sasa tunajifunza nini kama taifa kwa yanayoendelea Ukraine kwenye baadhi ya Nyanja mbalimbali kuanzia wananchi, Viongozi mpaka vyombo vyetu vya Ulinzi.
Wananchi
Tunaona Ukraine mpaka sasa wananchi wameamua kusimama na nchi yao na viongozi wao japo hawawezi kuwa wote na hili ndio limefanya vita iwe ndefu baada ya wananchi kukataa kwenda upande wa Mrusi, Mrusi alitegemea akiingia Ukraine atapokelewa kwa Shwangwe na Vifijo ila hali imekua tofauti mwisho wa Siku kakutana na chupa za Molotov na wakulima pamoja na matrekta yao kuiba Vifaru vyake. Je, kwa nchi yetu tuna Umoja huu?
Propaganda
Siku hizi Propaganda ni kati ya silaha za kivita kwa hili Ukraine wamefanikiwa kwa asilimia kubwa nahisi kuna watu maalumu kwa ajili ya hizi kazi. Je, kwa upande wetu kama nchi tumejiandaa vipi kwa hili?
Medani/Mbinu za Kivita
Hakuna mtu alitegemea hii vita itaenda kumaliza mwezi kutokana na ubora wa jeshi la Urusi ila kwa Ground mambo yamekua kinyume hapa kuna ishu nyingi za kujadili ila siwezi kuingia ndani kifupi nimegundua jeshi la watu wengi na vifaa vingi sio ishu kubwa ishu kubwa ni umoja na mbinu za kivita kumbuka vita ya Vietnam, Vietcong walikua dhaifu kwa vifaa ila umoja wao na mbinu zao ziliwasaidia.
Nchi marafiki wakati wa Shida
Leo tunaona kuna nchi zimeamua kubwa upande wa Urusi bila kificho na nyingine zimeamua kuwa upande wa Ukraine bila kificho Je sisi kama nchi tunawajua marafiki wetu wa kweli ambao watasimama nasi wakati wa shida.
Uchumi
Vita ni gharama kubwa, je kama nchi tumejipangaje kwa hili bajeti yetu kwenye Ulinzi inatosha
Angalizo Vita ni hatua ya mwisho kabisa endapo njia zote za upatanisho zitashindikana sipendi vita na siombei vita ila hii dunia imejaa watu wa kila aina unaweza kujifungia ndani na bado wakaja kukuchokoza sio mbaya nawe ukajiandaa kwa lolote.