Tunakoelekea sasa kunatisha...Ndoa za kulazimisha hizi mmh!


Mkuu kwa hiyo 2015 tumpe mwanamke asimamie nchi eeeeeh? Lakini hata mkuu wa kaya anatoa sana nafasi kwa wanawake kwenye uongozi..... watatunyonga hawaaaa....
 

Hiyo sentesi yako ya mwisho imeniacha natabasamu badala ya kusikitika
Ila mie ningeanza na huyu mwanaume ambae hamtaki mwanangu
 
mwanaume ndiye aliyetoa amri mtoto auawe?
watu8 nadhani mwanaume hakuwa anamuhitaji huyo mtoto na mama akaona dawa ni kumuua
wonders shall never end .....
 
Last edited by a moderator:
Sasa si angeenda hata kumuweka mtoto wake kwa ndugu yake watu wengine bana hawatumii akili kabisaa ndoa zenyewe za siku hizi mpaka unafikia hatua ya kuua.
 
Mwanaume aliyetoa sharti hilo hakuwa anampenda huyo mwanamke. Na huyo mwanamke ukimchunguza uelewa wake utakuwa una walakini, na nadhani ni mtu ambaye mtazamo wake utakuwa umejikita kuwa kuolewa ndiyo solution ya matatizo yote jambo ambalo ni uongo wa hali ya juu.
 

I can sense a lot of bitterness in you, l can say the same way about men unajua.

Twende polepole, aliyetoa mimba, aliyetupa mtoto n.k yuko wapi mwanamume ambaye wakati anataka kula tunda alimsifia na kumuassure kuwa she is the best thing that happened to him?

Sisupport hata kidogo uuaji aliofanya huyo mdada lakini kabla ya hapo nikifuata thinking yako aliyempa mimba in the first place yuko wapi? Si muuaji; imagine unaleta kiumbe duniani halafu unakitelekeza na kuenda kumwaga mbegu zingine kwa wadada wengine.

Please tuseme tu ubinadamu una mapungufu lakini si wanawake tu ndio wenye shida!
 
Mkuu kwa hiyo 2015 tumpe mwanamke asimamie nchi eeeeeh? Lakini hata mkuu wa kaya anatoa sana nafasi kwa wanawake kwenye uongozi..... watatunyonga hawaaaa....
Si unaona Liberia na Ujerumani zilivyoshika adabu? Mwanamke hana muda wa kumwangalia mtu machoni. Anakuua huku unamwangalia.
 
Hapo kuna wawili wameshiriki kutoa uhai wa mtoto huyo, hivyo lazima wote wawili wachukuliwe hatia ya kuwa wauwaji.
 
watu8 nadhani mwanaume hakuwa anamuhitaji huyo mtoto na mama akaona dawa ni kumuua
wonders shall never end .....
Hiyo ni akili finyu ya huyo mwanamama, angeweza kumpeleka huyo mtoto kwa ndugu zake.
 
Last edited by a moderator:


This is so typical of men.... kazi ni kujudge, kazi ni kulaumu.... Wanaume wangapi wanashtuka, guswa ama kukaa na kutafakari kuwa yeye kachukua nafasi ipi katika yale ambayo mwanamke kafanya? Wanaume wangapi wapo accountable and responsible in such matters? Hili ni tukio tu ambalo FL1 kawakilisha hapa, ila kumbuka kuna beyond that. Kuna influences... kuna circumtances ambazo zimepelekea huyo mwanamke kutenda ukatili huo. Either the way anaishi, either yale ambayo amepitia, either hali yake ya maisha na mengine meengi! (thou bado sio excuse).

Kutumia hili tukio na kujudge wanawake tuna roho mbaya ni makosa... kuna mengi wanawake tunafanya ambayo ni imani na powerful na ambayo katika hali ya kawaida mwanadamu mwingine kama mwanaume hawezi elewa wala kufikia hicho kiwango... Akina mama wote hawa walo kuzunguka and have so much love for their kids hawatoshi kukutambusha kuwa wanawake ni extra-ordinary creatures? Lukolo taratibu kaka.....
 
Last edited by a moderator:
Hapo kuna wawili wameshiriki kutoa uhai wa mtoto huyo, hivyo lazima wote wawili wachukuliwe hatia ya kuwa wauwaji.

Sidhani kama mwanamume alimwambia amuue mwanae; yeye alitoa msimamo wake kuwa hawezi oa mtu mwenye mtoto kama ambavyo wengi wamekiri kuwa hawawezi kuoa mwanamke ambaye ameachika akiwa na watoto.

Hiyo kesi ni ya huyo mdada muuaji ambaye kwa upuuzi wake anaona thamani ya mume ni kubwa kuliko kiumbe alichokileta duniani. Na hii dhana ya kuolewa ni heshima ndio ya kulaumiwa kwa asilimia ndogo sana; 90% ni upuuzi wa huyo dada, she deserve a life sentence!
 
Loh. . huyo mama anaweza akawa ana matatizo ya akili kwa kiasi fulani. Siwezi kuua mtoto wangu kwa lolote lile, achilia mbali ndoa ambayo naweza ipata kwa mwanaume mwingine kama naitaka sana.
 
Wanawake walio wengi hawana tena huruma wala utu, wanatoa sana mimba sasa, mitaani na makazini wanaongoza ugomvi wanauwa watoto, mwingine jana anakubari binti wa miaka 3 aingiliwe na boyfriend wake alafu anamtete kwa ndugu na polisi source leo tena clouds fm jana. Kweli mwanamke ufalme wake ni duniani, mwanaume ufalme wake mbinguni.
 
Wote wawili hamnazo...nani kawadanganya wakishau ndio maisha yao yatakuwa murua? Kwanini tunapenda kukimbia majukumu siku hizi?
 
Kwani asingeolewa ndio ingekua mwisho wa maisha??hivi kweli mtu anathamini ndoa kuliko mwanae??kweli binadamu tunatofautiana..
 
trust me, she will never HAVE PEACE kwenye maisha yake. hiyo roho ya huyo mtoto daima itamuandama!
 
nijibuni jamani hivi kuna nini soo special kwenye kuolewa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…