Tunakosea tunapoacha kuwashirikisha watoto wetu mafanikio yetu mapema

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
Katika miradi na vitega uchumi tunavyoanzisha, wengi hatuwashirikishi watoto wetu mapema.

Siku ukipata ajali, ugonjwa au kifo ndipo mke/mume au mtoto mkubwa anapokabidhiwa biashara au mradi ambao hajui ataanzia wapi kuuendesha.

Unakuta ulianzisha mradi wa ng’ombe wa maziwa, washirikishe watoto na familia kulisha na kukamua maziwa. Hata bwana mifugo akija kukaguwa wawepo na hata magonjwa ya kawaida wape kazi ya ziada kuyafanyia research huko shuleni kwao.

Hata biashara vya M-pesa, kama umeajiri kijana wa kukusaidia mpe off Jumamosi watoto uwafundishe kuendesha biashara kidogo kidogo.

Jitahidi kubalance muda wa home work na kusaidia biashara. Ile dhana vya kuwa hakuna cha bure inalipa, walipe watoto ujira mdogo kwa muda wanaosaidia.
 
Yeah uko sahihi nadhani ukiwashirikisha mapema utawaepusha na kutaabika maishani ilhali umewaachia vitega uchumi bt km hawajui namna ya kuviendeleza na mwishowe kufa halafu unaibuka ule msemo wa kimasikini eti mwenye mali kaondoka na mali yake kumbe baba au mama ndiye uliyesababisha.
 
Legacy yote uliyoianzisha inapotea na mali zinafilisika
 
Yaani mi Mungu akinijalia mtoto inshaallah lazima ajue kila kitu ninavyokifanya as long sifanyi biashara haramu mpaka anafika age ya 15yrs awe expert ikiwezekana km mm.
 
Yaani mi Mungu akinijalia mtoto inshaallah lazima ajue kila kitu ninavyokifanya as long sifanyi biashara haramu mpaka anafika age ya 15yrs awe expert ikiwezekana km mm.
Hii pia inasaidia kuwaepusha na magenge mabaya kwa ni wanakuwa busy
 
watoto wa siku hizi vichwa maji.
ukisha muonesha tu ni kosa.
kusoma hata soma tena
atakosa umakin katika vitu vya msingi kwa kutegemea vya baba vipo
 
Hayo mambo tuwaachie Wahindi ndo wanayaweza. Sisi tuwakomalishe watoto na shule tu.

Mtu ni mfanya biashara tena ana msisitizia mtoto wake asome aje kupata kazi nzuri.

Ndo maana wafanya biashara wengi wa kibongo utakuta watoto wake wameajiriwa some where na yeye ndo anaendesha biashara wengi sana.

Wahindi hakuna kitu kama hicho.
 
watoto wa siku hizi vichwa maji.
ukisha muonesha tu ni kosa.
kusoma hata soma tena
atakosa umakin katika vitu vya msingi kwa kutegemea vya baba vipo
Kwani lazima asome? Akisha jua kusoma na kuandika inatosha. Wale Wachina pale Kariakoo unazani wamesoma sana? Au unazani hawakuwa na pesa za kusoma?

Hahahaa Hizi elimu za Wakoloni ni shida sana zinatufanya tuamini kwenye kusoma tu then tukitoka hapo tukatumikiswe
 


aiseee
umepitwa na mengi.
hivi hujui elimu ndo ufunguo wa kukiendeleza hicho mzazi alicho anzisha???
hakuna mtaji, kiwanda au duka linalo weza kuongozwa na kukua bola maarifa ya darasaa has a katika kitu husika.
poleee Sana mkuuu
 
Ni utaratibu mzuri ila unaitaji umakini wa hali ya juu hasa kwenye vitu kama biashara bora kilimo na ufugaji au ata ujenzi na useremala ila hapo kwa duka au biashara ya pesa kwa pesa/bidhaa aise ni pagumu sababu patampa mtoto maarifa ya pesa ataitambua pesa ni nini sasa akiisha itambua swala la kujua namna ya kuitumikia ni lingine

Ila kwenye shuhuli za vitendo vya mwili sana sana utamfanya mtoto ajue pesa inatafutwa vipi pia utamjengea imani ya kuwa pesa haipatikani kirahisi bali ni kwa kupambana na pia utamfanya aamini kuwa viungo vya mwili wake amepewa na Mungu ili vimsaidie kupata kipato cha kuishi

Nadhani hii ya pili ndio nzuri zaidi kwa jamii yetu ya watu weusi. Inatufaa sana kutokana na asili yetu.

-wepesi kuwa wavivu
-wepesi kukata tamaa
-wepesi kuzulumu
-wepesi kuzulumiwa
-wepesi kudanganya na kudanganywa

Nadhani watoto wetu tuwaepushe na hii asili yetu ka kuwapa ujuzi na maarifa ya vitendo

Jumapili njema nyote.
 
Akisoma anaweza kuipeleka biashara to the next level kama ana maarifa
 
Uzi wa msingi sana huu hasa kwa wazazi
 
Hili tatizo linachangiwa na kukosekana kitu kama hicho juu cha mleta uzi. Mtoto au watoto ni matokeo ya malezi ya mzazi,shule na watu wengine wanaomzunguka. Siungi mkono hoja yako kwamba tuwakomalie na shule tu kwani kuna maisha baada ya shule na hayo ndio marefu sana zaid ya maisha ya shule,hivyo ni vyema kwa mzaz au wazazi kuwashirikisha watoto ili ifike sehemu wajue na kuamin hakuna maisha nje ya kujiajiri kama baba au mama anavyofanya. Kwa hapa kwetu walioweza hii kitu na wakinga na wachaga ambao wengi hata watoto wao wakisoma wengi wanarudi kufanya anachofanya mzazi
 
watoto wa siku hizi vichwa maji.
ukisha muonesha tu ni kosa.
kusoma hata soma tena
atakosa umakin katika vitu vya msingi kwa kutegemea vya baba vipo
Kuna namna ya kumuonyesha. Mamdogo aliwaonyesha wanae hati za nyumba zenye majina yao. Watoto aakajiona matajiri wakapata 4:49 shuleni huko.

Malezi ya majivuno pia yalichangia
 
Pia mkuu si watoto wote wana uwezo wa kufaulu mitihani na kufika mbali. Kama uke nurture vizuri ukimpa mtaji Kama matokeobya shule hayakuwa mazuri itamsaidia.
Hata akiendelea, malecturer wanaongoza Kwa Kuwa na maduka ya hardware ni njia ya kuongeza kipato
 
Well said
 
Daaah hiyo itasaidia sana hata kuepusha makundi ya vijana waliokata tamaa na kuanza kushawishika kuingia kwenye makundi ya kuharibu amani ya nchi yetu eti oooh maisha magumu, tunaitisha mgomo juu ya serikali so parents should teach their young to depend on themselves
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…