Bashir Yakub
Member
- May 27, 2013
- 96
- 1,745
TUNAKUSHUKURU WAMBURA, LAKINI UPELELEZI/UCHUNGUZI URUDIWE.
Bashir Yakub, WAKILI
+255714047241.
Sina utaratibu wa kutoa pongezi kwa mtu anayetekeleza majukumu yake lakini IGP Wambura nikupongeze walau kwa hatua za haraka ulizomchukulia RPC wa Dodoma kwa kauli yake ya hovyo na ya shibe.
Nikupongeza pia kwa kusoma alama za nyakati, kwani usingefanya ulichofanya kwa THEOPISTA basi hichihicho kingefanyika kwako na huenda kufikia kesho mida kama hii ungekuwa tayari umekuwa balozi wa Tanzania nchini Vietnam.
Kwa uzoefu wangu kama Wakili jeshi la Polisi ndio wahifadhi wa ushahidi na vilelezo.
Wasiwasi wetu ni kama THEOPISTA anaweza kutoa kauli kama hii usalama wa vielelezo vya kesi hii vilivyo mikononi mwake kama mhifadhi ukoje.
Niseme tu kuwa uchunguzi wa tukio hili unatakiwa kurudiwa chini ya Kamanda mwingine. Huyu THEOPISTA tayari ameonesha upande wake katika hili.
Kauli yake inasadifu kile alichochunguza na hata bila kuisoma hiyo ripoti tunaweza kujua kuna nini kwenye ripoti kupitia maneno yake yenye kutia kichefuchefu na ukakasi mwingi.
Nukta nyingine ya muhimu sana ni hii. THEOPISTA anasema wale vijana hawakutumwa na mtu. Ni wazi THEOPISTA anamsaidia mtuhumiwa muhimu sana kukwepa mkono wa sheria katika hili tukio.
Sehemu ya mazungumzo kwenye video inasema hivi :-
.......................
VIJANA WAHALIFU: umetoka sehemu gani
BINTI: Dar
VIJANA WAHALIFU: Dar sehemu gani
BINTI: yombo
VIJANA WAHALIFU: yombo sehem gani .
BINTI: yombo dovya.
VIJANA WAHALIFU: dovya sehemu gani
BINTI : pale shuleni
VIJANA WAHALIFU: leo ume....au ume...
BINTI: Nime........na ku.....
VIJANA WAHALIFU: kwa kosa gani, la kutembea na mme wa mtu, sio.
BINTI : ndio
VIJANA WAHALIFU: muombe msamaha AFANDE.
BINTI🙁akiwa amelazimishwa kutizama kamera)afande nisamehe sirudii tena, naomba sirudii tena
VIJANA WAHALIFU: onesha Chu...kwa ushahidi
BINTI : (binti anaonesha)
.....................
Kwahiyo kwa mazungumzo haya na kwa weledi wa upelelezi wa jeshi letu pendwa la Polisi hakuna mtu mwingine
aliyekuwa anarejewa hapo au THEOPISTA na wenzake mnataka kutueleza nini.
Hivi ingekuwa ni watu wamemshambulia Waziri halafu wamejirekodi wakisema ILE KAZI ULIYOTUTUMA TUMEIMALIZA AFANDE na hao watu wakakamatwa na polisi wangeishia hapo wakasema hawakutumwa na mtu.
Haya ndo mambo ambayo huwatia doa jeshi la polisi. Haya ndo huwafanya mpoteze imani kwa watu. Haya ndo mambo huwafanya raia wasiwe karibu na nyie kuibua uhalifu. Haya ndo mambo hutufanya kuhoji weledi wenu.
Maneno yawe machache, hawa vijana walitumwa na AFANDE na walikuwa wakijirekodi ili kumthibitishia AFANDE kwamba kazi imefanyika vizuri na kwa ufanisi. Hii haihitaji mafunzo ya upelelezi.
AFANDE ni nani na kwanini analindwa kwa kiwango hiki. Ni lazima AFANDE aungenishwe kwenye hii kesi ili haki si tu itendeke, bali ionekane kuwa imetendeka.
Hatutakubali mpaka AFANDE aungenishwe kwenye kesi pamoja na vijana aliowatuma.
Kuna jambo hamjalijua kuhusu hii kesi. Hii kesi ni ya UMMA sio tena ya huyo muathirika. Msipokuwa makini itawaondoa wengi madarakani, tuache mzaha hili jambo sio jepesi kama mnavyofikiria.