Waziri2025
Senior Member
- Sep 2, 2019
- 148
- 379
MTANGAMANO wa kikanda kwa nchi za afrika kupitia mashirika ya posta umesaidia kutoa huduma jumuishi na sahihi za kifedhana posta kwa watoa huduma zingine mbalimbali na hivyo kusaidia kuwafikia wananchi wengi kwa gharama nafuu na muda mfupi.
Hayo yameelezwa January 17 na Waziri wa Ujenzi,Mawasiliano na Uchukuzi Mhandis Isack Kamwele, kwenye maadhimisho ya miaka 40 ya Umoja wa huduma za posta barani Arika na kuongeza kuwa pato la taifa hasa kwenye nchi zinazoendelea yaliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano ya kimataifa (AICC.) Arusha
Amesema faida hiyo inasaidia kutolewa kwa huduma Jumuishi za kifedha na posta sehemu ambazo hazifikiwi kwa urahisi hasa maeneo ya vijijini ambako miundo mbinu yake haijawa rafiki kufikika kwa urahisi na kwamba serikali inaendelea kuboresha miundo mbinu lengo ni posta nchini kuwa na teknolojia yake ili kusaidia kurahisisha utolewaji wa huduma .
Kamwele,amesema swala la Nishati bado ni changamoto kwa baadhi ya maeneo nchini lakini serikali inasaidia kuboresha na haitachukua muda mrefu nchi yetu itakuwa na miundo mbinu mizuri kwa kuwa huduma hizo za posta zina uwezo mkubwa wa kuchangia mtangamano wa kiuchumi na kikanda na raslimali zigeuzwe kuwa uchumi.
Mradi wa huo PAPU aliousisi na Meya Mstaafu Kalisti Lazaro Wa Jiji la Arusha kwa kupambania kiwanja hicho kurudi serikalini Mara baadae ya kuporwa na mwekezaji sasa umeaanza kutelekelezwa ujenzi Wa Gorofa la kisasa la ofisi ya Papu
Mwaka Jana 2019 kalisti Lazaro pamoja na viongozi Wa papu walifikia ujenzi kuanza ambapo serikali ilitoa baraka zote na kusema kwamba iko tayari kuanza ujenzi Wa ofisi
Waziri Amesema kabla ya mwaka 1980 afrika ilikuwa haijaunganishwa na dunia katika mawasiliano hivyo kuanzishwa kwake kuna mambo mengi yamefanyika na kuhakikisha zinatolewa huduma bora zaidi
Kwa upande wake Mkurugenzi mkuu wa Umoja wa posta Ulimwenguni (UPU), Bishar Hussein, amesema maeneo ya Vijiji kwa muda mrefu yamekuwa na changamoto ya kufikiwa na huduma za posta hivyo kuna kila sababu kwa nchi wanachama kuboresha miundo mbinu ya mashirika ya posta katika nchi zao .
Amesema kuwa ipo haja kwa nchi wanachama kuboresha huduma za kifedha kwa wananchi na miradi hiyo itasaidia kukuza biashara ya mitandao na kuanzishwa kwa vituo ni kweli katika mtangamano huo huduma jumuishi za kifedha zimekuwa zikikabiliwa na changamoto mbalimbali hasa maeneo ya vijijini ambazo ni ngumu kufikika.
Awali Katibu muuu wa PAPU, Younouss Djibriene, amesema anazishukuru serikali zote za nchi wanachama kwa kusaidia kutekelezwa kwa mafanikio na shirikisho hilo la posta barani afrika ambalo limetimiza miaka 4o tangia lianzishwe mjini Arusha Tanzania mwaka 1980.
Amesema utengamano wa kikanda umesaidia kuimarisha mahusiano ya kibiashara na hivyo Papu, inapenbda kupitia umoja huo kuwepo na soko moja la biashara kupitia mitandao.
Ameongeza kuwa asilimia 80% ya huduma zinazotolewa zinasaidia kupunguza umaskini kwenye maeneo ya vijijini .
MWISHO.
Sent using Jamii Forums mobile app