Tunampataje mwalimu bora tanzania?

Mbelwa Germano

JF-Expert Member
Joined
May 7, 2011
Posts
789
Reaction score
289
Nimekuwa nikifuatilia harambee ya kuchangia tuzo ya Mwalimu bora kutoka kituo cha television cha ITV na baaada ya muda nilijiuliza swali moja: JE MWALIMU BORA TANZANIA ANAPATIKANAJE? Swali hili limezingatia ule ukweli kamili kwamba ni vigumu kufanya ufuatiliaji (monitoring) wa nchi nzima.

Nawakilisha.
 
uko sahihi. mazingira ya ualimu nk ni ngumu sana kumpata mwalimu bora. ni tofauti na soka. ingawa vijijini kuna wachezaji wazuri zaidi ya hawa tunaowaona, ila wanakosa exposure n akuonekana. kwa nchi kama tz ambayo haina updates M&E data ni ngumu, tena especially kwa asasi binafis kuja kusema huyu ni mwalimu bora kuliko wote.
 

Ni kweli kabisa mkuu,hili suala naona kama limekaa kimtego zaidi, nadhani kuna mtaji unatafutwa.
 
walimu bora unamjua wewe au unaongea tu? una muda mchafu wa kuchangia mambo ya kise##. nch so yako hii wewe, acha kuwa goigoi kiasi hicho. au kama vip kawe mwalimu bora wewe.
 
Wengi mtakubali hii nayo ni BONGO STAR SEARCH MPYA inayolalamikiwa kila siku. Haki itatendekaje kumpata mwl bora? Kuna makanjanja wachache wanataka kuwashika watu masikio,hii ni karata tatu mchana kweupe. Naona harufu ya DECI.
 
walimu bora unamjua wewe au unaongea tu? una muda mchafu wa kuchangia mambo ya kise##. nch so yako hii wewe, acha kuwa goigoi kiasi hicho. au kama vip kawe mwalimu bora wewe.

Kaka act wise kidogo, hapa tunahoji ni kwa jinsi gani waandaji wa tuzo za walimu wanaweza kumpata Mwalimu bora Tanzania kulingana na mazingira ya elimu nchini kwetu, binafsi napata tabu kidogo kuona mantiki ya waandaaji, sasa ukinishambulia unakuwa umekosea, kwa sababu umetoka nje ya mantiki ya hoja kwasababu sijataja yupi na nani ni mwalimu bora, ni vyema unapochangia uelewe content ya hoja yenyewe si kukurupuka.

Hili ni jukwaa la GT na ni jukwaa la majadiliano, we unataka nikachangie wapi?
 
Hawa nadhani itakuwa rahisi kuwapata

Hivi kwa mazingira haya ya watoto 150 class moja, vitabu hamna, vifaa vya kujifunzia na kufundishia havipo mwanafunzi amekata tamaa mwalimu ndo usiseme utapata mwalimu bora? IDARA ya UKAGUZI is almost dead nani anaweza kumbaini mwalimu bora? Ni miaka Sasa walimu wa serikali hawaandai scheme wala lesson plan, mwalimu bora atoke wapi? Wangetafuta bora walimu tuko wengi saaaaaaana!
 
Nadhani tukianza kusaka walimu wanaongoza kwa kuwapa mimba wanafunzi tutawapata kiurahisi,ilkiwepo na kinara wao.
 
walimu bora unamjua wewe au unaongea tu? una muda mchafu wa kuchangia mambo ya kise##. nch so yako hii wewe, acha kuwa goigoi kiasi hicho. au kama vip kawe mwalimu bora wewe.

sidhan kama hii adhabu inamstahili coz sijaona kibaya alichoandika
 
Nia ya ile Asasi ni njema ila naona mapungufu jinsi wanavyo tegemea kuendesha hili zoezi,hawakua wazi katika vigezo watavyotumia kupata Mwalimu Bora.Pia watu walioalikwa kwenye ile harambee walipwaya kama shuguli inahusu taifa zima!!
 

hapo mwalimu anausika vipi mkuu maana kama ni vitcu haoa sidhani kama mwalimu ndo anatakiwa avinunue
 
hii ni kupeana tu
wanaangalia sana wake za watu fulani hasa viongoz kisha wanatoa tuzo au
kwa upande wa wanaume ni kujuana tu na ulimsaidia vp kiongoz kwenye kampeni na uchaguz kisha unapewa tuzo
 
Mjadala huu ni mzuri sana japo kuna watu wachache wanaodhani kila mahali ni sehemu inayofaa kutoa kauli za matusi,tuwabeze na tuendelee na mjadala wetu. Mwalimu bora halisi hawezi kupatikana kwa mazingira ya Tz,coz any appraisal should be accompanied with a provision of instruments for performance of a givn task on which an appraisal wil be set.Sasa hawa wenzetu wametangulia kufanya appraising kabla hawajaweka mazingira yanayomfanya mwl afanye kazi yake,na wapate kumpima kwa haki.
 
Nia ya ile Asasi ni njema ila naona mapungufu jinsi wanavyo tegemea kuendesha hili zoezi,hawakua wazi katika vigezo watavyotumia kupata Mwalimu Bora.Pia watu walioalikwa kwenye ile harambee walipwaya kama shuguli inahusu taifa zima!!

Natumaini wangeweka vigezo wangeweza kujenga imani kwa wadau...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…