Elius W Ndabila
JF-Expert Member
- Jul 17, 2019
- 324
- 649
Na Elius Ndabila.
0768239284
Taifa lolote duniani ili liweze kuendelea na wananchi wake kunufaika na maendeleo ya nchi yao inategemea sana uhusiano wa kimataifa.
Uhusiano wa Kimataifa unasimamiwa na sheria za kimataifa ambazo nchi mbali mbali duniani zilitia saini.
Lakini nchi hailazimishwi kuwa na uhusiano na nchi nyingine kwa kuwa tu imesaini mkataba huo, bali kila nchi inauhuru wa kuchagua nchi ya kuwa na mahusiano nayo.
Uhusiano huu msingi wake ni VIENA CONVENTION ON DIPLOMATIC RELATION 1961.
Kumekuwa na jambo moja ambalo watu wengi hawalijui ambalo ndilo limenisukuma niandike makala hii fupi. Ili uweze kuwa na uhalali wa kuwa nchi hii inauhusiano na nchi hii ni lazima kuwe na Ubalozi wan chi husika kwenye nchi nyingine.
Huwezi kusema nchi hii inauhusiano na nchii hii kama nchi hizimbili hazina Ubalozi kwenye nchi hizo. Lakini kumekuwa na ufahamu mdogo juu ya mahusiano haya.
Watu wengi inapotokea tatizo au mafanikio kati ya nchi na nchi basi watu wanaokuwa wanatambuliwa kwenye uzuri huu au ubaya huu ni Waziri wa Mambo ya Nje na Balozi wa nchi husika.
Lakini ukweli wa mambo kwenye Balozi kuna watu watatu ambao ni mhimu sana ukiondoa maafisa wengine mbalimbali waliopo balozini.
Mmoja akicheza vibaya katika hawa watatu nitakaowaongelea leo basi kunaweza kuvunjika kwa mahusiano au kushindwa kutumia mahusiano hayo kujiletea maendeleo.
Nitawataja kwenye aya zinazofuata.
Nchi ambazo zimeweza kutumia vizuri fursa hizi za kimahusiano uchumi wake hauteteleke. Uchumi wake unapaa, hii ni kwa kuwa ukitumia vizuri Balozi ni rahisi kutangaza fursa zilizopo nchini ambazo zinaweza kuvutia wawekezaji na wadau wengine wanaoweza kuleta fedha za kigeni. Kama munyororo wa haya mafiga matatu haujakaa vizuri mnaweza kutafta mchawi na msimpate.
Uhusiano wa kimataifa ili uwe na faida haumtegemei Waziri na Balozi tu, bali kuna mtu ambaye ingekuwa ni uwanjani ningesema anacheza nafasi ya kiungo mkabaji.
Huyu asipokuwa makini na mbunifu timu inaweza kufungwa. Yaani kwangu ninamuona huyu ndiye key maker. Ili timu iweze kufunga huyu ndiye mwenye nafasi ya kupoza mashambulizi au kuchochea mashambulizi.
Kwenye Nyanja ya Diplomatic huyu mtu anaitwa Consular. Huyu ni ofisa anayekuwa kwenye kila balozi nayeye ndiye huhusika na mambo ya diplomasia ya uchumi. Huyu ndiye anahakikisha nchi rafiki inanufaika na uchumi wa nchi yake.
Huyu ni sawa na Waziri wa Fedha ambaye yeye ndiye anajua uchumi. Kwa mfano leo Tanzania uchumi ukishuka huwezi kumsema Rais wa nchi, tutamsema Mh Mpango na jopo lake lote pale Wizarani.
Rais ana mambo mengi lakini Waziri wa Fedha yeye ana deal na uchumi tu. Nchi ikiteketea ujue waziri hakufaa na si Rais. Halikadharika unapoenda nje Balozi anakuwa kama Rais yani anakuwa na mambo mengi, lakini CONSULAR yeye kazi yake ni uchumi tu.
Ibara ya 5 ya VIENA CONVENTION ON CONSULAR RELATIONS inazungumza kazi za CONSULAR, moja anasema to furthering the development of commercial, economic, cultural and scientific relations between the sending state and the receiving state..
Kwa mfano, leo hii tunalaumu kuwa Tanzania haijafanya vizuri kwenye sekta ya utalii ukilinganisha na vivutio vilivyopo hapa nchini.
Wapo watu wanaolaumu kuwa Wizara ya Mambo ya Mje haijafanya vizuri kwenye kuvitangaza vivutio hivi au balazo zetu hazijafanya vizuri ukilinganisha na nchi nyingine.
Lakini ukweli wa mambo ni kuwa yupo mtu ambaye alipaswa asilale kutangaza haya nakwa kuangalia namna ya kuwavutia hawa watu. Mhusika mkubwa naye si mwingine ni huyu anayeshughulika na Diplomasia ya kiuchumi/Consular na timu yake.
Waziri yeye anangalia mahusiano ya nchi na nchi zote marafiki duniani. Balozi yeye anangalia uhusiano wanchi aliyopo na nchi anayotoka lakini Consular yeye anangalia mahusiano ya kiuchumi baina ya nchi hizi mbili. Hata Immunity za watu hawa wawili zinatofautiana.
Nchi kubwa duniani kwa sasa zinashindana kwenye diplomasia ya uchumi na si vinginevyo. Nchi nyingi za mataifa makubwa sasa wanalitegemea bara la Afrika kuendesha nchi zao.
Sisi bado hatujatumia vizuri hizi rasilimali kwa kujenga uchumi imara na kuvuna fedha za hawa wazungu ambao hata kwao hawana maeneo ya kulima zaidi ya rotation agriculture.
Tanzania tu tukitangaza vizuri vivutio tulivyonavyo yaani kila Consular akatimiza wajibu wake basi nchi inaweza ikajiendesha kwa utalii. Huyu ni mtu muhimu sana ambaye nimeona nimwongelee kwa kuwa amejificha haonekani.
Siku nyingine nitakuja kuzungumza utofauti unaokuwepo kwenye majukumu kati ya Balozi/Ambassador na Consular. Nitazungumza majukumu yao, kinga zao na mipika yao ya kazi.