Tunamshauri na kumuonya Msajili wa Vyama vya Siasa aache sarakasi za maneno

BAK

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2007
Posts
124,790
Reaction score
288,165
WARAKA WA KICHUNGAJI (PASTORAL LETTER) WA MAONYO KWA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA NA JESHI LA POLISI NCHINI TANZANIA.

Mheshimiwa Jaji Francis Mutungi na Inspekta Generali Simon Sirro!

Pokeeni salaam za upendo kutoka kwetu sisi Askofu! Jana tuliwanyoshea kidole Ofisi Msajili wa Vyama vya Siasa na Jeshi la Polisi kupitia ukurasa huu tukiwaonya ninyi nyote kuacha kufanya vitendo vinavyofinya haki na hivyo kuchochea vurugu nchini. Tuliamini kuwa maonyo yale yangeliweza kuzingatiwa na wahusika wangeweza kuonyeka.

Lakini barua ya ufafanuzi iliyotolewa na Msajili wa Vyama vya Siasa, haionyeshi kama Msajili amepokea maonyo yetu na kama anakusudia kusitisha matendo yake. Tunapenda watu watambue kuwa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa sio moja ya taasisi kongwe katika michakato ya haki za msingi za watu duniani; bali Uhuru wa Kujieleza, Uhuru wa Kutoa Maoni, Uhuru wa Kujumuika, na Uhuru wa Kuamua ndizo taasisi kongwe zaidi zilizoasisiwa na kuumbwa pamoja na binadamu (rejea Maandiko Matakatifu). Ni kwa misingi hiyo, ndio maana katiba nyingi duniani ikiwemo Katiba ya Tanzania zimekwepa kuzifinya Taasisi hizo.

Katiba zinazoongoza taifa lo lote duniani, hazijawahi kusimamishwa na mamlaka ye yote ile isipokuwa pale nchi husika inapokuwa katika hali ya hatari au Jeshi linapopindua Serikali au wakati wa vita ya wenyewe kwa wenyewe. Tukiachia hayo, hakuna taasisi ye yote iliyo na mamlaka ya kuisitisha Katiba kwa sehemu au yote kutenda kazi isipokuwa katika mazingira ya vita. Hata Rais wa nchi amenyimwa mamlaka hayo isipokuwa pale ambapo nchi inapokuwa katika hali ya hatari, ndipo Rais anaweza kulitangazia Taifa kuwa nchi ipo katika hali ya hatari. Katika mazingira hayo, kuna mambo ya kikatiba yanaweza kukoma yenyewe au yanaweza kukomeshwa na mamlaka iliyotangaza hali ya hatari!

Utetezi wa Msajili wa Vyama vya Siasa kuwa hakusitisha mikutano ya siasa bali alishauri kusitishwa kwake hauna mashiko. Kama nia ilikuwa ni njema, Msajili angelikutana na wadau na kukubaliana nao kwanza ili kushauriana kwa pamoja kabla ya kuutangazia umma kama alivyofanya ambapo sasa ni dhahiri amejikuta akitoa kauli za kuvunja Katiba. Kimsingi, kushauri kusitisha mikutano ya kisiasa na mambo yanayofanana na hayo, ni kusitisha kufanya kazi sehemu ya Katiba, mamlaka ambayo Ofisi ya Msajili haina na haijawahi kupewa! Kitendo alichofanya Msajili wa Vyama vya Siasa ni jaribio la uvunjaji wa Katiba au kusimamishwa kwa Katiba (suspending the Constitution) mchana kweupe! Hayo mambo ndiyo yanayoleta vurugu nchini.

Sisi Askofu tunasikitika kuona Ofisi ya Msajili ikijiruhusu kutumika au kutumiwa kufanya matendo yanayoweza kupelekea vurugu (anarchy) nchini na kuhatarisha amani ya nchi. Kwa sababu hiyo, sisi Askofu Mwamakula, tunaosimama katika zamu yetu katika zamani hizi, tunamuonya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini kuacha mara moja kufanya mambo yanayoweza kupelekea vurugu nchini. Ni dhahiri kuwa Vyama vya Siasa, vikipuuza 'maelekezo' au 'ushauri' wa Msajili, Jeshi la Polisi litaingia kutaka kuizuia mikutano hiyo kwa nguvu. Vyama vya Siasa na wafuasi wao wanaweza wasikubali udhalimu huo wa Jeshi la Polisi, na hapo ndio nchi itakuwa imetumbukia katika vurugu!

Tunamshauri na kumuonya Msajili wa Vyama vya Siasa aacha sarakasi za maneno kuhusu jambo ambalo halina mikanganyiko wo wote kikatiba. Ole wao viongozi ambao kwa ulafi wao wa madaraka na vyeo wanafanya vitendo vya kutaka kuvuruga na kuvunja Katiba ya Nchi. Hao mnaowapigania kwa kutaka hata kuvunja Katiba hawewezi kubaki madarakani kama Mungu ataamua kuondoa kibari cha wao kuendelea kutawala. Mungu na awakemee wale wote wanaofanya hila (Yuda 1:9).

Wasipojitafakari na kuacha uovu huu, Mungu atawafedhehesha wao, familia zao pamoja na vizazi vyao. Maonyo yetu tuliyotoa jana kwa Msajili wa Vyama vya Siasa na Jeshi la Polisi yanaendelea kubakia pale pale kama maonyo ya Askofu kwa watu walio ndani ya Taasisi husika; hivyo hata maonyo haya tunayotoa leo ni msisitizo tu wa yale tuliyotoa jana ili dunia ijue kuwa kulitokea watumishi wa Mungu katika nchi hii ambao hawakuogopa kuwaonya viongozi na watawala (Ezekieli 33:1-20)

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Mkuu Emmaus Bandekile Mwamakula

B27A2D7C-ED95-45F8-A452-444FD4403332.jpeg
 
Wanaonekaga wanaofaidika na utawala wa CCM ,hawachoki kukingia ubavu kila madai dhidi ya serikali na chama cha MAPINDUZI ( Sasa ndio kipo kazini kiufasaha kabisa kinapindua matokeo ya Uchaguzi ) .nasema uongo ndugu zangu ?
 
Maneno mazito na dhahiri haya toka kwa mtumishi wa Mungu:

"Tukiachia hayo, hakuna taasisi ye yote iliyo na mamlaka ya kuisitisha Katiba kwa sehemu au yote kutenda kazi isipokuwa katika mazingira ya vita."

Hata Rais wa nchi amenyimwa mamlaka hayo isipokuwa kwenye mazingira ya vita.
 
Huyu Mwamakula ana msongo wa mawazo, ndio maana siku zinavyozidi kwenda anazidi kukauka na kuchakaa! Mnafiki mkubwa
 
WARAKA WA KICHUNGAJI (PASTORAL LETTER) WA MAONYO KWA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA NA JESHI LA POLISI NCHINI TANZANIA.

Mheshimiwa Jaji Francis Mutungi na Inspekta Generali Simon Sirro!

Pokeeni salaam za upendo kutoka kwetu sisi Askofu! Jana tuliwanyoshea kidole Ofisi Msajili wa Vyama vya Siasa na Jeshi la Polisi kupitia ukurasa huu tukiwaonya ninyi nyote kuacha kufanya vitendo vinavyofinya haki na hivyo kuchochea vurugu nchini. Tuliamini kuwa maonyo yale yangeliweza kuzingatiwa na wahusika wangeweza kuonyeka.

Lakini barua ya ufafanuzi iliyotolewa na Msajili wa Vyama vya Siasa, haionyeshi kama Msajili amepokea maonyo yetu na kama anakusudia kusitisha matendo yake. Tunapenda watu watambue kuwa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa sio moja ya taasisi kongwe katika michakato ya haki za msingi za watu duniani; bali Uhuru wa Kujieleza, Uhuru wa Kutoa Maoni, Uhuru wa Kujumuika, na Uhuru wa Kuamua ndizo taasisi kongwe zaidi zilizoasisiwa na kuumbwa pamoja na binadamu (rejea Maandiko Matakatifu). Ni kwa misingi hiyo, ndio maana katiba nyingi duniani ikiwemo Katiba ya Tanzania zimekwepa kuzifinya Taasisi hizo.

Katiba zinazoongoza taifa lo lote duniani, hazijawahi kusimamishwa na mamlaka ye yote ile isipokuwa pale nchi husika inapokuwa katika hali ya hatari au Jeshi linapopindua Serikali au wakati wa vita ya wenyewe kwa wenyewe. Tukiachia hayo, hakuna taasisi ye yote iliyo na mamlaka ya kuisitisha Katiba kwa sehemu au yote kutenda kazi isipokuwa katika mazingira ya vita. Hata Rais wa nchi amenyimwa mamlaka hayo isipokuwa pale ambapo nchi inapokuwa katika hali ya hatari, ndipo Rais anaweza kulitangazia Taifa kuwa nchi ipo katika hali ya hatari. Katika mazingira hayo, kuna mambo ya kikatiba yanaweza kukoma yenyewe au yanaweza kukomeshwa na mamlaka iliyotangaza hali ya hatari!

Utetezi wa Msajili wa Vyama vya Siasa kuwa hakusitisha mikutano ya siasa bali alishauri kusitishwa kwake hauna mashiko. Kama nia ilikuwa ni njema, Msajili angelikutana na wadau na kukubaliana nao kwanza ili kushauriana kwa pamoja kabla ya kuutangazia umma kama alivyofanya ambapo sasa ni dhahiri amejikuta akitoa kauli za kuvunja Katiba. Kimsingi, kushauri kusitisha mikutano ya kisiasa na mambo yanayofanana na hayo, ni kusitisha kufanya kazi sehemu ya Katiba, mamlaka ambayo Ofisi ya Msajili haina na haijawahi kupewa! Kitendo alichofanya Msajili wa Vyama vya Siasa ni jaribio la uvunjaji wa Katiba au kusimamishwa kwa Katiba (suspending the Constitution) mchana kweupe! Hayo mambo ndiyo yanayoleta vurugu nchini.

Sisi Askofu tunasikitika kuona Ofisi ya Msajili ikijiruhusu kutumika au kutumiwa kufanya matendo yanayoweza kupelekea vurugu (anarchy) nchini na kuhatarisha amani ya nchi. Kwa sababu hiyo, sisi Askofu Mwamakula, tunaosimama katika zamu yetu katika zamani hizi, tunamuonya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini kuacha mara moja kufanya mambo yanayoweza kupelekea vurugu nchini. Ni dhahiri kuwa Vyama vya Siasa, vikipuuza 'maelekezo' au 'ushauri' wa Msajili, Jeshi la Polisi litaingia kutaka kuizuia mikutano hiyo kwa nguvu. Vyama vya Siasa na wafuasi wao wanaweza wasikubali udhalimu huo wa Jeshi la Polisi, na hapo ndio nchi itakuwa imetumbukia katika vurugu!

Tunamshauri na kumuonya Msajili wa Vyama vya Siasa aacha sarakasi za maneno kuhusu jambo ambalo halina mikanganyiko wo wote kikatiba. Ole wao viongozi ambao kwa ulafi wao wa madaraka na vyeo wanafanya vitendo vya kutaka kuvuruga na kuvunja Katiba ya Nchi. Hao mnaowapigania kwa kutaka hata kuvunja Katiba hawewezi kubaki madarakani kama Mungu ataamua kuondoa kibari cha wao kuendelea kutawala. Mungu na awakemee wale wote wanaofanya hila (Yuda 1:9).

Wasipojitafakari na kuacha uovu huu, Mungu atawafedhehesha wao, familia zao pamoja na vizazi vyao. Maonyo yetu tuliyotoa jana kwa Msajili wa Vyama vya Siasa na Jeshi la Polisi yanaendelea kubakia pale pale kama maonyo ya Askofu kwa watu walio ndani ya Taasisi husika; hivyo hata maonyo haya tunayotoa leo ni msisitizo tu wa yale tuliyotoa jana ili dunia ijue kuwa kulitokea watumishi wa Mungu katika nchi hii ambao hawakuogopa kuwaonya viongozi na watawala (Ezekieli 33:1-20)

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Mkuu Emmaus Bandekile Mwamakula

tumpuuze tu
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Back
Top Bottom