Tunaofuatilia Squid Game 3 tukutane hapa. Ni mchezo gani kwenye Season 3 unajua kabisa usingetoka salama?

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
2,536
Reaction score
7,194
Wakuu,

Binafsi nimetoka kuangalia na kumalizia Series maarufu duniani ya Squid Game muda sio mrefu.

Kwa kweli I'm still traumatized na zile games pamoja na storyline nzima hasa kifo cha starring Gi Hun ambaye alijitoa maisha yake ili kuokoa maisha ya yule mtoto.

Lakini pia the fact kwamba mtoto mchanga ndo alishinda zile hela zote bado kinanichekesha. Yaani dogo alizaliwa kwenye eneo hatari sana lakini mwisho wa siku akawa Bilionea kwa urahisi tu

Alafu kuna zile games pia. Game ambayo binafsi ilinisikitsha ni ile hide and seek, yaani kombolela. Hakuna kitu kilinisikitisha kama yule mwamba ambaye alikuwa anamsaidia yule bibi na yule binti namba 222 ambaye alikuwa mjamzito kufariki.

Kiukweli that game nisingetoboa kabisa!

Maana ili uweze kushinda ni lazima na wewe ule mtu kichwa. Binafsi nadhani kwa upande wa Storyline Season 2 iko vizuri zaidi ila kwenye Season 3 michezo imekuwa interesting zaidi



Vipi nyie wenzangu, ni games gani ambazo unajua kabisa msingetoboa?
 
Mimi ndio yule dogo muoga muoga lakini nikafika hadi final game,

Game zote ningekuwa kama yule dogo, uoga ni akili muda mwingine
 
Jamani mimi mpka saivi sijapata hii movie,,natamani niipate lakini kila nikienda movie room wananipa ambazo zipo translated na mimi sitaki movie ambazo zipo transalated ,,,
NAOMBA MWENYE LINK YA MOVIE HII AU HATA TELEGRAM MOVIES ANISAIDIE
 
Jamani mimi mpka saivi sijapata hii movie,,natamani niipate lakini kila nikienda movie room wananipa ambazo zipo translated na mimi sitaki movie ambazo zipo transalated ,,,
NAOMBA MWENYE LINK YA MOVIE HII AU HATA TELEGRAM MOVIES ANISAIDIE
Onstream apk
 
Nenda google search nkiri.com


Au awafim kisha ingia humo search squid game utaipata

Naomba unipe link au njia yoyote ile unitumie bado sijaipata
 
Ile game ya funguo na kisu ile game ngumu sana kwangu naona
 
Nafikiri huu mchezo wa rock, paper, scissors hasa ukihusisha kuuliwa ni mchezo mgumu sana
 
WAcha niifuatilie hii
 
Games za season 3 hazikua ngumu sana zilihitaji kujiamini zaidi.

Hide & seek mi ningeombea nipewe bisu ila sio kujificha aisee.
Bisu ni chap namtoboa mtu napita.

Game ya mwisho kilichowaua ni tamaa na kutoaminiana.
 
Season 1 ndo ilikuwa moto zaidi, then inafuata hii 3. Season 2 ilini-disappoint
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…