GUSSIE
JF-Expert Member
- Dec 2, 2014
- 3,880
- 11,134
Wanabodi,
Ni jambo lisilopingika watu ambao tunafurahi na kucheka kimaisha wakati wa JPM tupo wengi sana sana humu jamvini
Gharama za maisha zimeshuka sana. Leo hii kila kitu bei rahisi kuanzia chakula,Viwanja mpaka nyumba zinauzwa bei rahisi sana. Wakati wa Kikwete bei zilikuwa juu sana kutokana na mafisadi kushikilia uchumi hewa usio na mizizi
Gharama za kusomesha watoto zimeshuka sana. Leo shule binafsi unaweza kaa nao kuongea ada utalipa wakati gani na zimekuwa ni ada zinazoendana na vipato vya watu wengi sana. Mafisadi walijenga shule za academy uchwara kwa lengo la kuumiza wananchi wakati wa JK
Turudi kwenye kichwa cha uzi
Mimi binafsi nimebahatika kutembea nchi za nje zaidi ya 30 wakati huu wa JPM na hii imetokana na serikali kudhibiti mapato na kusimamia matumizi kwa miaka mitano. Kwa miaka kumi ya JK nilisafiri nchi 10 tu
Kipindi hiki cha JPM nimeweza kuwa na muda wa kutosha kuongea na familia yangu zaidi ukilinganisha na awamu iliyopita muda mwingi nilishinda kwa madalali na mafisadi kuweka mambo yangu sawa. Maofisa wa serikali wengi ilikuwa mpaka utoe rushwa ili mambo yako yakae sawa lakini JPM amejenga heshima
Kuna mambo mengi kwa watu smart ambayo JPM ameyafanya kwa Taifa hili.
Wezi, mafisadi na wapiga dili ndio walioumia. Sisi wa kuheshimu utu na haki JPM ni shujaa