Tunaokwerwa na SMS za Promo tukutane hapa tafadhali!

DrLove69

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2018
Posts
3,112
Reaction score
3,491
Rejea kwenye kichwa cha Uzi hapo juu.
Binafsi nimekuwa nikipata usumbufu sana kutoka kwa haya Makampuni ya mitandao ya simu kwa kutumiwa SMS za kipumbavu.
Kutwa napokea SMS za;
Vodacom Ofa
Boom pesa
Pesa ni mpesa
Tigo SMS
Magic
15670 SOKA

Na nyingine nyingi ambazo sizikumbuki kichwani. Hii kwangu imekuwa ikineletea usumbufu mkubwa sana.
Mimi kama mteja wa Makampuni ya simu nina Haki ya kukubali au kukataa kutumiwa hizo SMS za Promos.
Simu yangu sio bango la matangazo ya biashara. Simu yangu ni kwa matumizi yangu binafsi. Nikitaka huduma za ziada nitafika katika Ofisi husika na kuomba maelekezo ya zaidi.
Wito kwa TCRA kuna Watanzania tumevimbewa na hizi tabia za haya Makampuni ya simu. Kwa niaba naomba mlitafakari na kuliangalia kwa kina hili suala la wateja kutumiwa SMS za Kipumbavu na Kusababisha usumbufu mkubwa.
 
Nilijua nakereka peke'angu...sipendi mm mameseji yao jamaniii yananijazia sanduku langu tuu la ujumbe mfupi,..aahg!!!
Hauko peke yako mkuu! Ni kero zaidi ya kero. Muda mwingine unakuta uko mbali na simu na unategemea msgs za muhimu...mara unasikia msgs zinaingia dabodabo, unaamka na kuwahi simu unakutana na upuuzi wa promos. Aaaaaargh :-(
 
Waache bhana uchochezi,.
 
me nkiziona uwa nafurah sana mana sina mtu wa kuchat nae hvy nkiziona huwa nachat nao wanipe more details khs promo hy husika
 
me nkiziona uwa nafurah sana mana sina mtu wa kuchat nae hvy nkiziona huwa nachat nao wanipe more details khs promo hy husika
Ni Haki yako ya kimsingi. Na ndio maana huduma kama hizo ilifaa zizingatie vigezo na masharti vya mteja. Kwa wateja wa aina yako ni sahihi kupokea hizo SMS, ila kwa sisi wengine ambao hatuna uhitaji nazo wangetafuta njia bora ya kutuepusha na huo usumbufu.
 
Mi huwa zinanikera zinapokuwa zinajirudia yaani tangazo moja wanarudia kama vile umalazimisha kutumia huduma hiyo
 
Mi huwa zinanikera zinapokuwa zinajirudia yaani tangazo moja wanarudia kama vile umalazimisha kutumia huduma hiyo
Acha tu mkuu! Unakuta unapata SMS kama tano hivi kwa mkupuo na zote zimefanana kimaudhui!
 
Hauko peke yako mkuu! Ni kero zaidi ya kero. Muda mwingine unakuta uko mbali na simu na unategemea msgs za muhimu...mara unasikia msgs zinaingia dabodabo, unaamka na kuwahi simu unakutana na upuuzi wa promos. Aaaaaargh :-(
Download App inaitwa True caller inablock matangazo ya kampuni za simu, yaani tangazo likiingia kwa mara ya kwanza mfano toka tigo bima, ukiliblock hutaliona tena, likija linaingia mojakwamoja kwenye dustbin hulioni hadi siku utembelee huko kwenye blocked sms hii ni baada ya kuifanya true caller kuwa default Sms app. App hii pia inakuwezesha kuonesha jina la akupigiaye au kutuma sms hata kama ni namba ngeni
 
Spam reports
 
Ninayo hiyo app kwa simu kitambo mkuu. Lakini siku hizi haya Makampuni ya simu yamekuja na ujanja wa aina tofauti ambao ukiblock namba it's Invalid number. Sijui kama umenipata hapo mkuu!?
Nadhani wametumia codes tofauti kwenye digits.
 
Wanakwepa kodi ya kuweka matangazo barabarani,itabidi TCRA walivalie njuga hili suala. Kampuni zote ziashe kuwatumia wateja wao promo SMS na badala yake waweke matangazo ili serikali ipate kodi ya matangazo[emoji4]
 
na sms za halotel ukishaweka salio zinavyomiminika
Afadhali hatotel,tigo ndo pasua kichwa. Ikitokea umetuma SMS huku ukiwa hujui kama bando limeisha utatumiwa SMS za salio halitoshi kama hamsini hivi kwa mkupuo[emoji4] [emoji4]
 
Wanakwepa kodi ya kuweka matangazo barabarani,itabidi TCRA walivalie njuga hili suala. Kampuni zote ziashe kuwatumia wateja wao promo SMS na badala yake waweke matangazo ili serikali ipate kodi ya matangazo[emoji4]
Umegusa jambo la msingi sana mkuu.
 
Ndugu Mteja,umebakiwa na Dk 0.00 Tigo-Tigo.Piga *102*00# kuangalia salio au *147*00# kununua kifurushi kingine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…