Tunaomba mrejesho greenhouse agriculture

Tunaomba mrejesho greenhouse agriculture

michepuko

JF-Expert Member
Joined
Apr 22, 2014
Posts
1,192
Reaction score
345
Wakuu ni miezi iliyopita iliyopita tuliona threads za kutosha kuhusiana na kilimo cha greenhouse,Ningependa wale members ambao walijaribu kilimo hiki watupe mrejesho walipofikia ila na sisi members mengine tujue wapi pa kuanzi,Ahsanteni.Kilimo kwa kwanza.
 
Mkuu kweli tunahitaji wachache wenye uzoefu tupate changamoto walizopitia tusijepita humo tena kwa mfano nikiangalia mazao yanayo limwa humo mengi yanahitaji maji, dawa na mbolea nyingi changamoto kama hizi walizikabili vipi wakiwa wageni n.k.

kilimo barazani kwangu, hii itanipunguzia michepuko maana sintokwenda kwa mama chausiku huko uzaramuni.
 
Mkuu kweli tunahitaji wachache wenye uzoefu tupate changamoto walizopitia tusijepita humo tena kwa mfano nikiangalia mazao yanayo limwa humo mengi yanahitaji maji, dawa na mbolea nyingi changamoto kama hizi walizikabili vipi wakiwa wageni n.k.kilimo barazani kwangu, hii itanipunguzia michepuko maana sintokwenda kwa mama chausiku huko uzaramuni.
Mkuu inamanaa JF yote hakuna member aliye jaribu hii kitu? inabidi tupate mrejesho wa hili,maana zile mil 3 za ku install greenhouse si ndogo ati.
 
Mkuu inamanaa JF yote hakuna member aliye jaribu hii kitu? inabidi tupate mrejesho wa hili,maana zile mil 3 za ku install greenhouse si ndogo ati.

Mtu kama GEBA2013 anakuambia kuliko atupe 3mil yake kwenye Greenhouse ya 15m x 8m, bora akalime zake matikiti, yatamtoa tu.

Wajua hawa jamaa hua sometimes wanachukua picha za Mashamba ya nje na kuja kutudanganyishia wabongo.

Mtu anakuambia anatengeneza Greenhouse ya mirunda halafu akikuonyesha picha za ndani ya shamba, unashangaa kuna kench za Chuma!!
 
Last edited by a moderator:
Mtu kama GEBA2013 anakuambia kuliko atupe 3mil yake kwenye Greenhouse ya 15m x 8m, bora akalime zake matikiti, yatamtoa tu.Wajua hawa jamaa hua sometimes wanachukua picha za Mashamba ya nje na kuja kutudanganyishia wabongo.Mtu anakuambia anatengeneza Greenhouse ya mirunda halafu akikuonyesha picha za ndani ya shamba, unashangaa kuna kench za Chuma!!
Natamani sana nipate ushuhuda wa mmoja aliyejaribu hii kitu from scratch,anipe mafaniko yake na changamoto zake,maana haiwezekani kitu kikawa productive halafu kisi sambae kwa kasi,hapo ndio nina doubt.
 
Last edited by a moderator:
Aliesema milioni tatu ni nani? Greenhouse si chini ya milioni tano..
 
Mimi binafsi nimetembelea kilimo cha green house kilichopo kijiji cha Nsola wilaya mpya ya Busega mkoani Simiyu. kilimo kina maendeleo mazuri sana. nawashaulini hata nyinyi mtembelee kilimo hicho mpate kujifunza. Wageni wengi wanatembelea hapo. Tupo pamoja kujenga nchi.
 
Hiki kilimo kilikuja kwa kasi sijui nini kimetokea mpaka kukawa na kimya kikubwa hivi.
 
Hiki kilimo cha greenhouse Kenya wanakipiga kwelikweli...ila TZ tunapewa information ambazo katika utekelezaji inakuwa shida sana.Na hao wanaosema ni expert kimsingi sio, mana nimewatembelea greenhouse zao ila huwezi pata motisha ya kuwekeza ... mana wana "underperformace cultivation". Labda ufauatiliaji wa hali ya juu ufanyike kabla hatujaanza michakato kama hii.
 
Aliesema milioni tatu ni nani? Greenhouse si chini ya milioni tano..

Lakin kuna kipindi huwa kinarushwa kwenye TV sijui ni TBC nilifanikiwa kukikuta katikati kikiongelea jambo hili.
Mwendeshaji wa kipindi aliitwa Sactus Mtsimbe na alikuwa na hojiana na mhasibu wa TIA ambaye alikiri kufanya aina hii ya kilimo nafkiri.

kwa mujibu wa maneno ya mgeni alianza kwa sh mil moja lkn tayri alikuwa na jengo sasa hapa ndipo tuanze kupeana uzoefu.
 
huo mjengo pekee tu ni ml tano kisha kuna mbegu mbolea etc labda ndo hiyo ml moja yake. Tofauti na kenya na uganda imeshakuwa common kwaiyo wanaoagiza material wengi na bei zimeshuka hapa material ni bei kubwa sana mtu unawaza endapo haitazalisha ni hasara
 
Wakuu ni miezi iliyopita iliyopita tuliona threads za kutosha kuhusiana na kilimo cha greenhouse,Ningependa wale members ambao walijaribu kilimo hiki watupe mrejesho walipofikia ila na sisi members mengine tujue wapi pa kuanzi,Ahsanteni.Kilimo kwa kwanza.

Kilimo cha greenhouse ni kizuri lakini kina challenges kama agri-business/business nyingine. Tatizo tulilo nalo Tanzania ni watu kutaka mafanikio/pesa ndani ya muda mfupi kuliko ilivyo practical. Wanaosema kwamba ni expert wa kilimo hiki wanakuza mafanikio yanayoweza kupatikana. Ni marketing ili kupata wateja wengi na kutoka haraka. Binafsi nimetembelea baadhi ya hizi demo greenhouses. Mavuno hayapo mengi kama wanavyotangaza. Na sio rahisi wao kukupeleka kwa mtu ambaye wamemjengea ukitaka kupata uzoefu. Watu wengi Uganda na kenya walivamia kilimo hiki na wameacha hizo structure zinaozeana. Kilimo hiki ni
1.Expensive (Initial Capital)
2.Kinahitaji ujuzi na uangalizi wa karibu sana ili kupata mavuno bora tofauti na watu wengi wanavyodhania
3.Unahitaji mtu mwaminifu kupata material zinazohitajika especially polythene. Hii sio nylon ya kawaida na watu wengi hudanganya hapa

Kwa mtu ambae yupo serious ni vema kumtembelea mkulima halisi wa greenhouse kabla ya kuanza kilimo hiki.Arusha wapo wengi kidogo!
 
Shwari mkuu,hapo kwenye kukuza mafanikio ili wapate biashara ni kweli,kwasababu wengi wamejaribu wakaacha,nadhani itakua inachangamoto nyingi na ngumu kidogo.
Kuhusu Arusha nadhani hali ya hewa nayo ina wa favour sana tofauti na maeneo mengi ya joto kali.
 
Kilimo cha greenhouse ni kizuri lakini kina challenges kama agri-business/business nyingine. Tatizo tulilo nalo Tanzania ni watu kutaka mafanikio/pesa ndani ya muda mfupi kuliko ilivyo practical. Wanaosema kwamba ni expert wa kilimo hiki wanakuza mafanikio yanayoweza kupatikana. Ni marketing ili kupata wateja wengi na kutoka haraka. Binafsi nimetembelea baadhi ya hizi demo greenhouses. Mavuno hayapo mengi kama wanavyotangaza. Na sio rahisi wao kukupeleka kwa mtu ambaye wamemjengea ukitaka kupata uzoefu. Watu wengi Uganda na kenya walivamia kilimo hiki na wameacha hizo structure zinaozeana. Kilimo hiki ni
1.Expensive (Initial Capital)
2.Kinahitaji ujuzi na uangalizi wa karibu sana ili kupata mavuno bora tofauti na watu wengi wanavyodhania
3.Unahitaji mtu mwaminifu kupata material zinazohitajika especially polythene. Hii sio nylon ya kawaida na watu wengi hudanganya hapa

Kwa mtu ambae yupo serious ni vema kumtembelea mkulima halisi wa greenhouse kabla ya kuanza kilimo hiki.Arusha wapo wengi kidogo!

Nimesikia VETA wameanza kujenga green house, walionyesha kwenye maonyesho ya sabasaba ya mwaka huu.
 
Kilimo cha green house sio kibaya Kama wengi wetu wanavyofikiri ila kilichopo hapa ni wengi wetu hii techinolog mpya kwetu, Kinachoonekana hapa wengi wetu hatujaamua kufanya Kama kazi! Ila ni Kweli kina changamoto zake hasa mambo ya Agrossupport ndio changamoto pia hizi green house zinatofautiana kulingana na kampuni inayokuwekea, kuna kampuni moja sitaitaja ipo mikoa ya kaskazin ,walitumia furusa hiyo kuwadanganya sana wakulima kwani tunnel/green house zao zilitengenezwa kwa matumizi ya ulaya ambazo ni nchi za baridi wao wakawa wanaziuza hapa na ni fupi! Kwa ushauri na green house zinazoendana nchi ya Tanzania nitafute 0655404047
 
Mwenye swale unaweza kuniuliza juu ya green house!
 
Attachments

  • ImageUploadedByJamiiForums1422552109.008704.jpg
    ImageUploadedByJamiiForums1422552109.008704.jpg
    16.2 KB · Views: 222
  • ImageUploadedByJamiiForums1422552327.074143.jpg
    ImageUploadedByJamiiForums1422552327.074143.jpg
    7.4 KB · Views: 202
  • ImageUploadedByJamiiForums1422552386.221186.jpg
    ImageUploadedByJamiiForums1422552386.221186.jpg
    9.6 KB · Views: 199
Back
Top Bottom