Mkuu inamanaa JF yote hakuna member aliye jaribu hii kitu? inabidi tupate mrejesho wa hili,maana zile mil 3 za ku install greenhouse si ndogo ati.Mkuu kweli tunahitaji wachache wenye uzoefu tupate changamoto walizopitia tusijepita humo tena kwa mfano nikiangalia mazao yanayo limwa humo mengi yanahitaji maji, dawa na mbolea nyingi changamoto kama hizi walizikabili vipi wakiwa wageni n.k.kilimo barazani kwangu, hii itanipunguzia michepuko maana sintokwenda kwa mama chausiku huko uzaramuni.
Mkuu inamanaa JF yote hakuna member aliye jaribu hii kitu? inabidi tupate mrejesho wa hili,maana zile mil 3 za ku install greenhouse si ndogo ati.
Natamani sana nipate ushuhuda wa mmoja aliyejaribu hii kitu from scratch,anipe mafaniko yake na changamoto zake,maana haiwezekani kitu kikawa productive halafu kisi sambae kwa kasi,hapo ndio nina doubt.Mtu kama GEBA2013 anakuambia kuliko atupe 3mil yake kwenye Greenhouse ya 15m x 8m, bora akalime zake matikiti, yatamtoa tu.Wajua hawa jamaa hua sometimes wanachukua picha za Mashamba ya nje na kuja kutudanganyishia wabongo.Mtu anakuambia anatengeneza Greenhouse ya mirunda halafu akikuonyesha picha za ndani ya shamba, unashangaa kuna kench za Chuma!!
Aliesema milioni tatu ni nani? Greenhouse si chini ya milioni tano..
Lakin kuna kipindi huwa kinarushwa kwenye TV sijui ni TBC nilifanikiwa kukikuta katikati kikiongelea jambo hili.
Mwendeshaji wa kipindi aliitwa Sactus Mtsimbe na alikuwa na hojiana na mhasibu wa TIA ambaye alikiri kufanya aina hii ya kilimo nafkiri.
kwa mujibu wa maneno ya mgeni alianza kwa sh mil moja lkn tayri alikuwa na jengo sasa hapa ndipo tuanze kupeana uzoefu.
Wakuu ni miezi iliyopita iliyopita tuliona threads za kutosha kuhusiana na kilimo cha greenhouse,Ningependa wale members ambao walijaribu kilimo hiki watupe mrejesho walipofikia ila na sisi members mengine tujue wapi pa kuanzi,Ahsanteni.Kilimo kwa kwanza.
Kilimo cha greenhouse ni kizuri lakini kina challenges kama agri-business/business nyingine. Tatizo tulilo nalo Tanzania ni watu kutaka mafanikio/pesa ndani ya muda mfupi kuliko ilivyo practical. Wanaosema kwamba ni expert wa kilimo hiki wanakuza mafanikio yanayoweza kupatikana. Ni marketing ili kupata wateja wengi na kutoka haraka. Binafsi nimetembelea baadhi ya hizi demo greenhouses. Mavuno hayapo mengi kama wanavyotangaza. Na sio rahisi wao kukupeleka kwa mtu ambaye wamemjengea ukitaka kupata uzoefu. Watu wengi Uganda na kenya walivamia kilimo hiki na wameacha hizo structure zinaozeana. Kilimo hiki ni
1.Expensive (Initial Capital)
2.Kinahitaji ujuzi na uangalizi wa karibu sana ili kupata mavuno bora tofauti na watu wengi wanavyodhania
3.Unahitaji mtu mwaminifu kupata material zinazohitajika especially polythene. Hii sio nylon ya kawaida na watu wengi hudanganya hapa
Kwa mtu ambae yupo serious ni vema kumtembelea mkulima halisi wa greenhouse kabla ya kuanza kilimo hiki.Arusha wapo wengi kidogo!