Tunaomba mrejesho ujenzi wa barabara za Kitunda

Tunaomba mrejesho ujenzi wa barabara za Kitunda

Gloriamagret

Member
Joined
Jun 12, 2023
Posts
47
Reaction score
155
Tunaomba mrejesho kuhusu ujenzi wa barabara za kata ya kitunda kama tulivyoahidiwa kutoka Banana kwenda Kitunda, Magole, Kivule, Hospitali ya wilaya kivule, Magole, Mwanagati, Msongola nk.

Tuliahidiwa ujenzi wa barabara hizo kujengwa kwa kiwango cha lami kwa mfuko wa DMDP awamu ya pili.

Mwenye taarifa atujuze ujenzi unaanza lini? Tenda inatangazwa lini? Nini kinaendelea kwa sasa nk.

Tunaomba kupewa mrejesho

Raia Mwama.
 
Mmeshapigwa na kitu kizito. Walaghai walitanda ila 2025 tutawatandua na jimbo letu la Ukonga litakuwa na 'steady flow' ya maendeleo. Mpaka kufika 2030 jimbo la Ukonga litakuwa ni jimbo lenye maendeleo kuliko majimbo yote ya Dar nikifanikiwa kuwa mbunge wenu 🤗🤗🤗
 
Hiyo inawatosha, nyie hamna mchango mkubwa kwa taifa haaaaah haaaah,huko mpo wafuga kuku tu tuwaletee barabara ya nini
 
Wakazi wa hicho kipande mjitafakari mnaowachagua , mi nimepita majuzi nilijua barabara itakuwa mkeka kumbe mambi niliyoyaona kipindi cha waitara ni yaleyale.
 
Back
Top Bottom