Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,843
- 31,057
Mwanzoni mwa mwezi wa tatu mwaka huu, tulimwona Kamanda wa Polisi wa kanda maalum ya Dar, Lazaro Mambosasa, akiongea na waandishi wa habari, akielezea tukio la kulazwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili, kwa Makamu Mwenyekiti wa CCM Taifa, Mzee Mangula.
Katika taarifa yake hiyo alitutueleza kuwa Mzee Mangula alianguka ghafla baada ya kumaliza kikao cha Kamati Kuu ya CCM, iliyoketi katika ofisi yao ndogo iliyopo Mtaa wa Lumumba jijini Dar-es-salaam, iliyokuwa ikiwajadili wanachama wa chama hiko akina Bernard Membe, Abdrahman Kinana na Mzee Yusuph Makamba, kwa kile kilichoelezwa na chama hiko kuwa ni utovu wa nidhamu wa wanachama hao
Katika taarifa yake hiyo, alitueleza wananchi kuwa kwa taarifa walizozipata kutoka katika hospitali alikolazwa huyo Mzee Mangula ni kuwa amegundulika kuwa alinyweshwa sumu.
Kwa hiyo Kamanda Mambosasa, alijiapiza kwa nguvu zake zote kuwa watawasaka popote pale walipo ndani ya nchi na hata nje nchi, wote waliohusika katika njama za kupanga na wale waliotekeleza uovu huo, ambao ni dhahiri ulikuwa ni mpango mahsusi wa kutaka kuyaondoa maisha ya kiongozi wetu wa juu wa CCM
Akaendelea kusisitiza kuwa Jeshi lake halitajali kama watu hao watatoka CCM au chama kingine cha siasa na akasema kuwa watawaburuza mahakamani wahalifu hao mara tu watakapokamilisha upelelezi wao
Tunafahamu kuwa kwa kutekeleza jukumu hilo, Jeshi letu la Polisi nchini litakuwa linahakikisha linatekeleza wajibu wao namba moja katika majukumu yao, ambayo ni kuhakikisha usalama wa raia wake na mali zao
Tokea wakati huo Mzee Mangula amekuwa kimya sana na kuzua hofu miongoni ya wananchi kujiuliza yuko wapi mkongwe huyu wa siasa hapa nchini?
Hata hivyo kitendawili hicho kimetenguliwa siku ya Jana baada ya kuonekana akiibuka ghafla Ikulu ya Chamwino Dodoma, akiambatana na Rais wa Zanzibar, Dkt Mohamed Shein wakiwa na mwenyeji wao Rais Magufuli.
Sasa swali ninalomuuluza Kamanda Lazaro Mambosasa ni je baada ya tambo zake zote zile, je uchunguzi wa waliomnywesha sumu Mzee Mangula umefikia wapi?
Kwa kuwa hivi sasa ni takribani miezi minne tokea atoe tambo hizo na hatujasikia maendeleo yoyote kuhusu upelelezi huo