kiraia
JF-Expert Member
- Nov 20, 2007
- 1,716
- 1,006
Kwa kipindi cha Nyuma kumekuwa na tetesi za Shirika la umeme Tanzania kukata umeme siku za uchaguzi hasa kipindi cha jioni wakati kura zikihesabiwa na kuwapa nafasi wale wasio na huruma na nchi yetu kutekeleza azma zao. Hivyo basi tunaomba uongozi wa TANESCO kuwa wazalendo mwaka huu na kuacha nuru iwamulike wezi wa kura hasa yale maeneo yenye umeme. kwa yale maeneo yasiyokuwa na umeme hasa vijijini tunawaomba wapiga kura kuwa makini ili uchakachuaji usiweze kufanyika kwani tetesi za masunduku ya kura feki za mbeya bado zinatesa bongo zetu japo ndio hivyo wakubwa wameshakanusha.