Tunaomba tufahamishwe gharama za matunzo ya ndege za ATCL za kila mwezi na hasara tuliyopata tangu zipaki kwa ajili ya matatizo ya Corona duniani

Tunaomba tufahamishwe gharama za matunzo ya ndege za ATCL za kila mwezi na hasara tuliyopata tangu zipaki kwa ajili ya matatizo ya Corona duniani

Synthesizer

Platinum Member
Joined
Feb 15, 2010
Posts
12,699
Reaction score
22,598
Kwa wale wanaojua masuala ya uhandisi wa ndege pamoja na kuzitunza, wataelewa kwamba hakuna kitu chenye gharama kubwa kama kupaki ndege bila kuitumia. Unapokuwa na ndege ni lazima itumike karibu kila wakati. Gharama za kuitunza ndege iliyopaki ni kubwa sana.

Tulikuwa na shamrashamra za kununua ndege ambapo tuliambiwa sasa ndege za ATCL zimefikia zaidi ya 10. Hatukutarajia kukumbwa na blaa la Corona lililozuia usafiri hasa wa kimataifa na kiasi wa ndani ya nchi.

Sasa kama wananchi wenye uchungu na kodi zetu, tungependa kufahamishwa gharama za kila mwezi tunazoingia kwa kupaki ndege za ATCL kutokana na ugonjwa wa Corona.

Na pia tungependa kujua tangu tatizo hili liikumbe dunia, ATCL imeingia gharama na hasara za kiasi gani kwa kupaki ndege zake.
 
Ndege zilipaki lini? Na ulichangia kiasi gani kununua?
 
Ndege zilipaki lini? Na ulichangia kiasi gani kununua?
Unajua kodi ninayolipa serikalini wewe? Au unafikiri hizi ndege zilinunuliwa toka hela ya mfukoni ya Raisi Magufuli? Na unafikiri gharama ya kuzindunza hela inatoka wapi? Kwa kuniuliza nilichangia kiasi gani unaonyesha wazi ulivyo mbumbumbu. Nenda shule. Domo kubwa masikio madogo.
 
Ndege hazijapaki zinapiga route acheni uwongo
Huo ni ufinyu wa akili. Kama tunajua ndege zinafanya kazi kwa nini tuulize gharama za kupaki? Labda wewe uliye mkweli utuambie zinapiga route kwenda wapi.
 
Hili halitakiwi, utaitwa mchochezi, Ni swali la maana lakini huwezi kupata majibu zaidi ya kufanyiwa dhihaka.
 
Achana na mashangingi hayo yana ufinyu wa uelewa

Back
Top Bottom