Tunaomba wakurugenzi waliopokea vibali vya uhamisho kwa wenza tangu mwishoni mwa December 2024 wawaachie na wao wapate fursa ya kuungana na familia

Tunaomba wakurugenzi waliopokea vibali vya uhamisho kwa wenza tangu mwishoni mwa December 2024 wawaachie na wao wapate fursa ya kuungana na familia

Black Walker

Senior Member
Joined
Oct 8, 2018
Posts
119
Reaction score
254
Tunaomba wakurugenzi waliopokea vibali vya uhamisho kwa wenza tangu mwishoni mwa December 2024 na mwanzoni mwa January 2025 wawaachie na wao wapate fursa ya kuungana na familia zao.

Inasikitisha sana kuona kwamba tuna viongozi ambao hawana huruma na watanzania wenzao.

Suala la uhamisho kwa sasa limekuwa na usumbufu mwingi kuliko kawaida kila hatua fikiria mtumishi anapambania uhamisho wake kwa muda mrefu wengine kwa mwaka mzima na zaidi, inatokea mtu wa watu anabahatika kupata kibali kwa Katibu mkuu TAMISEMI au UTUMISHI. Changamoto nyingine inajitokeza kwa hawa wanaoitwa wakurugenzi wanakalia barua kwa muda mrefu sijui huwa wana maana gani.

Ni dhahiri kabisa kwamba haya ni mateso ya wazi kwa hawa watumishi. Wakurugenzi badilikeni.
 
Dah poleni i feel you,hata mimi nilihangaika sana mwisho Mungu alinisaidia kwa kupata mtu wa kubadilishana kwenye mfumo.
 
Back
Top Bottom