Tunaomba watu wastaafu wakiwa 45 years (maisha ya nchi yetu ya Tanzania)

Extrovert24

Senior Member
Joined
Jun 23, 2022
Posts
144
Reaction score
211
Habarini wana Jf,

Katika Nchi yetu ya Tanzania population inazidi kuwa kubwa hasa na takribani miaka 100 ijayo Tanzania inaweza kuwa kwenye top ten ya Nchi zenye population kubwa duniani kulingana na Takwimu, hivo kutokana na ukuaji wa population wasomi wanazidi kuwa wengi, shule zinakuwa nyingi sana Lakini ajira hakuna ndiyo pale mwanafunzi anamaliza masomo yake ya elimu ya Juu Hana fani yoyote ya kujiajiri mwenyewe na anasubiria aajiriwe serikalini kitu ambacho ni kigumu sana na kuwapelekea vijana wengi kuanza kuwaza uhuni na mambo mengi ya ajabu ambayo hayatakiwi kufanyika katika Jamii.

Hivyo, lengo la kuyasema haya ni kwamba, kutokana na ongezeko kubwa la wasomi Serikali ifanye Marekebisho katika mtu kustaafu kufanya kazi serikalini (Iwekwe miaka 45 au mpaka 50 lakini 45 itapendeza zaidi). Naamini mtu akiajiriwa hali ya kuwa ana Umri wa miaka 25-28, mpaka kufikia 45 atakuwa tayari keshatengeneza msingi wa maisha na watoto wake na kwa hali kama hii watu watakuwa serious sana. Siyo mtu mpaka afikishe miaka 60 ndiyo astaafu wengine nao waliosoma miaka 17 mpaka 20 wawe wamepoteza tu muda? Kutakuwa na faida ya kupeleka watoto shule?..

Lakini pia suala la viongozi wa Serikali, kwanini mtu mmoja anakuwa uongozi wa wizara nyingi na mishahara yote anachukua? Kwanini wasipewe watu wengine ili nawao waishi vizuri na familia zao pamoja na ndugu zao? Kwanini awe mtu mmoja tu?

Kazi Mizinguo tuuuu, Fanyeni Amendment bhn , Nchi ina watu wengi sana na wengine waishi na familia zao.

Yaani kwanza Bora ingekuwa mtu akifikisha miaka 50 tu anakuwa hawezi hata kutoka ndani maana mnazingua saana.
 
Wazo zuri ila cha kuongezea ikiwa kustaafu ni miaka 45 mishahara pia iongezwe ili kunenepesha mifuko ya watumishi, na mafao yake PSSF ili mtu akimaliza utumishi awe na kimradi chake
 
ushauri wa ovyo hao unaowaita wasomi ni wa elimu ya kukariri kwenye makaratasi na vyeti.. wengi tunaosoma nchi hii ili kuajiriwa na huo ndio mfumo wa elimu yetu wa kukariri vitabu mm naona bora kubadili mfumo mzima wa elimu wa kusoma ili kuajiriwa uwe ni ule wa kutoa ujuzi na maarifa mtu unaweza kujiajiri!
 
Mimi nashauri mtu aajiriwe kwa miaka 15 tu. Mfano, mtu akipata ajira akiwa na 20, basi akifikisha 35 astaafu. Anayejiriwa akiwa na 25 basi akiwa na 40 aondoke.
 
mbona umri uliotaja wa kuajiriwa hiyo miaka 20-25 huyo si bado mwanafunzi wa form six au chuo tena hiyo miaka 20 wengine ndo wanamaliza form 4 sidhani kama serikalini wanaajiri wasio na walau cheti au diploma labda Uaskari tu ndo unaingia hata na division 4 ya mwisho
 
Wazo zuri ila bado utekelezaji wake utakuwa mgumu maana Tanzania hii watu wanaanza ajira na miaka kati ya 30-35. Yaani inasikitisha sana, ukitaka kujua fuatilia saili zinazoendelea kwa sasa nchini hizi za watu wa Afya na ualimu.
 
Tatizo mishahara ya bongo ni midogo sana. Wanaofaidi ni wanasiasa na watu wa taasisi kubwa na mashirika makubwa ambao wanapata pesa ya kutosha kwa mwezi hivyo vipato vyao vinaruhusu kufanya uwekezaji.

Maisha nje ya ajira rasmi ni magumu sana hasa wakati wa kujitafuta. Ukifanikiwa kujipata kupitia biashara hutotamani kuajiriwa kabisa.
 
mbona umri uliotaja wa kuajiriwa hiyo miaka 20-25 huyo si bado mwanafunzi wa form six au chuo tena hiyo miaka 20 wengine ndo wanamaliza form 4 sidhani kama serikalini wanaajiri wasio na walau cheti au diploma labda Uaskari tu ndo unaingia hata na division 4 ya mwisho
Siku hizi f4 ni miaka 16-18. Chuo shahada ya kwanza miaka 21. Maters 25.
 
Habarini wana Jf,

Katika Nchi yetu ya Tanzania population inazidi kuwa kubwa hasa na takribani miaka 100 ijayo Tanzania inaweza kuwa kwenye top ten ya Nchi zenye population kubwa duniani kulingana na Takwimu, hivo kutokana na ukuaji wa population wasomi wanazidi kuwa wengi, shule zinakuwa nyingi sana Lakini ajira hakuna ndiyo pale mwanafunzi anamaliza masomo yake ya elimu ya Juu Hana fani yoyote ya kujiajiri mwenyewe na anasubiria aajiriwe serikalini kitu ambacho ni kigumu sana na kuwapelekea vijana wengi kuanza kuwaza uhuni na mambo mengi ya ajabu ambayo hayatakiwi kufanyika katika Jamii.

Hivyo, lengo la kuyasema haya ni kwamba, kutokana na ongezeko kubwa la wasomi Serikali ifanye Marekebisho katika mtu kustaafu kufanya kazi serikalini (Iwekwe miaka 45 au mpaka 50 lakini 45 itapendeza zaidi). Naamini mtu akiajiriwa hali ya kuwa ana Umri wa miaka 25-28, mpaka kufikia 45 atakuwa tayari keshatengeneza msingi wa maisha na watoto wake na kwa hali kama hii watu watakuwa serious sana. Siyo mtu mpaka afikishe miaka 60 ndiyo astaafu wengine nao waliosoma miaka 17 mpaka 20 wawe wamepoteza tu muda? Kutakuwa na faida ya kupeleka watoto shule?..

Lakini pia suala la viongozi wa Serikali, kwanini mtu mmoja anakuwa uongozi wa wizara nyingi na mishahara yote anachukua? Kwanini wasipewe watu wengine ili nawao waishi vizuri na familia zao pamoja na ndugu zao? Kwanini awe mtu mmoja tu?

Kazi Mizinguo tuuuu, Fanyeni Amendment bhn , Nchi ina watu wengi sana na wengine waishi na familia zao.

Yaani kwanza Bora ingekuwa mtu akifikisha miaka 50 tu anakuwa hawezi hata kutoka ndani maana mnazingua saana.
Kwanini usipendekeza wanafunzi wafundishwe fani mbali mbali ili wakimaliza vyo wajiajiri?
 
Mkiambiwa chagueni viongozi wenye akili hamtaki mnata tustaaffu at age of 45!?? You must be crazy!! Hebu tuache bwana !! Wewe endelea kusikiliza bongo fleva na kushabikia ssc na Yanga!!
 
Back
Top Bottom