Kwa furaha kubwa sana kipindi cha Uncle Magu niliipongeza serikali kwa kuanza kuleta ndege mpya za air Tanzania nikiamini ya kwamba ushindani dhidi ya fastjet utaongezeka nasi abiria tunufaike zaidi.
sikumbuki vizuri kilichotokea lakini fastjet waliondoka akabaki air Tanzania peke yake kama ndege kuu, hata hivyo sikufa moyo nilidhani tutaendelea kupanda air Tanzania kwa nauli kama za fastjet ama pungufu zaidi, kinyume na nilichofikiria mambo yakawa tofauti kabisa mpaka leo, kupanda air Tanzania ni ghali hata kwa watanzania middle class,
Fastjet tuliweza kupanda kwa elf 70 mpaka laki Dsm kwenda Kia (Moshi / Arusha), iliweza kupata sifa ya kuwa huduma ya kijamii, tuliweza kujionea hata safari za Dsm Mbeya zinajaa
Enzi hizo hata ushamba wa ndege watu wengi waliutoa, Nauli Mbeya hadi Dar kwa basi elf 40, fastjet elf 70 unaona heri uongeze miekundu mitatu upande mwewe
Air Taanzania wanaoweza ku afford ni matawi ya juu wale kina upper middle class na kuendelea, wengine wakipanda labda iwe emergency