Ndoto za mchana kweupe hizi.
Hakuna hasiyeyajuwa mabaya ya CCM, wala mabaya haya hayakuanza leo, wala wabwabwaji wa mabaya ya CCM hawakuanza leo.
CCM itaendelea kushinda chaguzi na kadhalika itaendelea kuvurunda uchumi wa nchi na maisha ya wananchi, hadi hapo tutakapokuwa na chama cha upinzani. Kuyasema mabaya ya CCM kila kukicha kamwe hakumwondoi mtanzania katika lindi la umaskini bila ya kuwa na chama madhubuti kitakachompa mwananchi alternative.
Tatizo sio CCM, tatizo ni watanzania. Hawana substitute ya CCM. CUF, chama ambacho kina nguvu kule visiwani kimegeuka mtaji wa wachache. Kiongozi wake mwenye dira ya ufalme ameapa maisha kugombea urais kwa gharama zozote. Kwake demokrasia lazima iwe baina ya vyama na si ndani ya chama chake. Kwake usafi wa kikombe sio ndani bali nje. CUF bara ni dhaifu mno kiasi cha kudhoofisha nguvu za kisiasa za mwenyekiti wake wa taifa, chanzo cha udhoofu huu hakitakiwi kujadiriwa na wala udhoofu huu hauchochei maswali juu ya mwelekeo wa CUF kwa ujumla.
Chadema, chama ambacho kingeleta matumaini nacho kimegeuka kichekesho kwa mwananchi wa kawaida. Ukabila umejikita vilivyo, viwango vya elimu cha viongozi wake wakitaifa ni mushkiri, viongozi wake badala ya kwenda vijijini kuanzisha matawi wanakesha JF 24/7 kana kwamba kura za JF zinatosha kukipa Chadema madaraka. Hotuba za bunge badala ya kuwafikia wapiga kura wa vijijini zinaletwa JF. Vijijini kwenye wapiga kura wengi, helkopta ya kiongozi inaonekana tu wakati wa kampeni.
Kwa maoni yangu wapinzani wametuangusha na wataendelea kutuangusha kwa kushindwa kwao kuwapa wananchi substitute ya CCM. Tz hatuhitaji wapinzani wa kuleta upinzani kwa CCM, bali upinzani wa kuing'oa CCM madarakani, that is what we need. Leo hii wapinzani wetu wameridhika kuwa kama mbwa anayebweka kila mwizi anapokuja hali akijuwa ni bosi wake tu ndiye anayeweza kumshika mwizi huyo. So at the end of the day mbwa ataendelea kubweka hata kama mwizi anayembwekea ni mtoto wa bosi wake. Upinzania lazima uwe wa kuing'oa CCM, upinzani wa kuorodhesha mafisadi wa CCM kila kukicha kamwe hautaleta maendeleo.
CCM inafungua matawi India, Chadema na CUF hazina tawi Tz kote. Leo hii wapinzani tunasema CCM kitanzini? Tunapata wapi nguvu hizi? Headlines za magazeti bongo yanayoongozwa na wapinzani zimejaa shutuma za CCM na serikali yake, kana kwamba wizi huu umeanza leo, hivi isingekuwa jambo la maana magazeti ya wapinzani yakawa yanaandika juu ya kuundwa kwa matawi ya vyama vya upinzani katika strongholds za CCM na mikakati ya ushindi 2010?
Tulichobakiwa wapinzani ni dua za bata (wala sio za kuku) na CCM wanajuwa hilo fika. Kama fisi wa mwituni tunakesha tukiomba mkono wa binadamu ung'oke tupate mlo, pasipo sisi kufanya jitihada zozote kuung'oa. Wapinzani tumewaangusha wananchi 100%, hatujawapa option.