Tunaosubiri namba E tukutane hapa

General Mangi

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2013
Posts
15,303
Reaction score
23,064
Namba D zimekaa miaka mingi, tangu 2012 mpka leo, takribani miaka 9 na ushee...

Namba D ndo inaishia ukingoni, Jana Gari zilizosajiliwa zilikua DWV.




Sijui kwa herufi moja huneba magari mangapi mpk kuhamia herufi nyingine...
Nilisikia sijui ni magari 1000, yani ukitoka DW kwenda DX..

Jana tumesikia magari zaidi ya 3000 yameingia kwa mkupuo, ofcoz sio yote ni ya TZ, ila i bet 2000 yatakua ya hapa Tz...[emoji3]

Kwa idadi hiyo basi DZ inaingia mtaani mwezi huu na kudumu kwa miezi miwili...

Namba E rasmi October, D inakua yazamani [emoji23][emoji23][emoji23]

Kuna ambae anasubiri namba E kama mimi tuvute mkoko japani????

Update
22/08/2022
Leo ndio tarehe namba E imeingia mtaani,
Tangu mwaka jana mwezi kama huu uzi huu uanzee....

Bye bye namba D, madalali sasa tuingie kazini [emoji3][emoji3][emoji3]

Toa namba D mtaani, weka namba E, habari ya mjini [emoji28]
View attachment 2332963


Chaos
 
Duuh!.

Kwa hiyo namba E inakupunguzia kiasi cha matumizi ya mafuta? Au gari ndiyo itakuwa Classic?

Ninyi ndiyo wale mnashikishwa magari mabovu kwa sababu tu ya kununua namba badala ya gari.

Ninyi ndiyo wale ambao hamtaki kukubali kuwa uzee umefika, mnalazimisha kufanya mambo ya ujana ili kuendana na usasa. Utaangukia pua tu.

Bro, kuna gari namba B ni kali sana kuliko namba D.

Chukua mkoko, acha kusubiri namba.

Anyway, sikupangii matumizi ya fedha zako Mkuu.
 
Vumilia vumilia kaka, namba D zinaboa...

Madalali wamehiaribu hiyo namba [emoji23][emoji23][emoji23]
Hahahahah wakati huo wa namba E bora ufike ili zile IST za number D tuuziwe million 5/5 chap chap maana ni nyingi sana 😅!

Yani hali ilivyo sasa hata IST namba DC mtu anakomalia auze million 8 na inauzika fasta! Najiuliza ukija mbadala wa IST ghafla sijui wenye nayo sasa hali itakuwaje!
 
Zimekaa mda mrefu sababu ni waliondoa plan ya pikipiki kuchanganyika na magari! Ndio maana zile B na C hazikudumu muda mrefu. Kwa kumbukumbu C zilianza 2010 bila shaka mpaka kufikia 2014 zikakata zikaanza D!

A zilimezwa na conversion ya magari kutoka TZS 99999 format kwenda T111AAA!

B zilimezwa na usajili wa pikipiki humo humo nazo hazikudumu sana!

C ndio zilikaa almost 4 years zikaisha sababu ya hela ya Jakaya ilikuwepo bado kwenye account na mizunguko ya Watu!

D zilipoanza na mzee Jiwe akawa ameingia mitamboni kuanza kutingisha hali zetu😅 na ndio nahisi atakuwa amekufa nazo mwaka huu maana January lazma tuanze na E!
 

D zinakera sana mkuu...
nafikiri kila mwaka tuhamie namba mpyaa [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mkuu kumbukumbu zako haziko sawa.

Number C zilianza march 2012, zikaenda had sept 2014. C ndiyo iliyokaa muda mfupi zaidi, na ndiyo iliyomezwa na bodaboda

B ilianza 2009 had 2012 march.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…