Mkasome huko! Kafateni mikumbo na ushamba wenu mtaishia muhula wa kwanza... Wale hawanaga mchezo.
Tambua na uikumbuke hali ya nyumbani kwenu, uende ukaige wanaoazimwa magari na Kaka zao wenye makazi na mamishahara makubwa plus connection, mtaishia pabaya! Enzi sisi tunasoma Ngoma ilikuwa kwa kiasi kikubwa sana! Sijui siku hizi... Labda ARV imepunguza makali.
Wanaume huwaga ni wambea na wenye kufatiliana na kuchafuana (chuki binafsi) kuliko wanawake. Baadhi ya walimu wana utoto ndani yao wenye waliopata ajira kimazabe na connection, wakiku-mind hutakaa ufaulu... Soma usomavyo, utaishia kupata "C", ukipasua sana "B".... Mwisho wa siku GPA inasoma "2"
Ukiishi pale kama haupo, fata kilichokupeleka, fanya assignments zote na discussion shiriki, test na final utamaliza salama.
Epukana mikumbo, kutafuta umaarufu na kujulikana kusiko na sababu! Kutakuponza.
Kila la kheri!