Tunaotoka mkoa wa mkoa wa MARA njoo hapa

Tachu hano

JF-Expert Member
Joined
May 30, 2016
Posts
1,506
Reaction score
2,518
Tunaotoka mkoa wa MARA

Kwa neema za Mwenyezi MUNGU wanajamii forum wote mu wazima wa afya

Jamii forum ina watu tofauti tofauti kutoka sehemu mbalimbali hapa nchini

Leo naomba kwa wale wote tuliokaa ,tunaotoka au tunaoishi mkoa wa MARA tuambie ni changamoto gani unayokutana nayo kutoka kwa watu wa sehemu tofauti au uliyokutana nayo kwa sababu tu wewe ni kutoka mara (mkurya kama wengi wanavyodhani )

Au wewe ulipata changamoto gani kutoka kwa watu wa mara

......... Kuanza na mimi changamoto kubwa ni pale napojitambulisha kuwa ni mtu wa mara na mkurya watu kutamka hadharani kuwa Sisi wakurya ni KATILI na wanatuogopa huwa najisikia vibaya sana na sifa mbaya nyingne kama hizo

Karibu na wewe utwambie changamoto na ikiwezekana tuweze kubadirisha watu mitazamo yao kuhusu Sisi ::

Nb...si kila mtu kutoka mara ni mkurya
Ila mimi ni ndiyo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi nipo Mgango huku Musoma vijijini. Changamoto kubwa ninayoiona huku ni watu kuchukuliana wake. Unakuta mama mtu mzima ameacha familia kwake anatoka na kijana mdogo tu haooo hadi gesti. Sasa sijui huko wanafanya nini labda wanabadilishana mawazo ya kimaisha ila akili yangu inanituma kuhisi wanabambiana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siyo hivyo tu pia tunatambulika kama wezi na majangili!! Mfano nenda magerezani kama siyo robo basi ni theluthi ya watuhumiwa n Lakini pia tunajulikana kwa ujasiri wa kutokuogopa chochote zaidi ya haki .

Cairo's
 
Siyo hivyo tu pia tunatambulika kama wezi na majangili!! Mfano nenda magerezani kama siyo robo basi ni theluthi ya watuhumiwa n Lakini pia tunajulikana kwa ujasiri wa kutokuogopa chochote zaidi ya haki .

Cairo's
Ni kweli wengi ndivyo wanavyotuchukulia sisi watu kutoka mkoa wa mara
Asee yaani mtu anakwambia hivo alafu ukuumuuliza una uhakika yeye anakwambia eti anasikia watu wanaongea hivyo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…