Mkuu just be honest to yourself...ni mara ngapi umewahi kutumia ofisi yako kupiga dili ukapata non taxable money(hizo ndiyo pesa chafu zenyewe).
Ikiwa kila mtu anawaza kupiga dili ili awe na RAV 4, Carina, CR-V, Demio etc ya kwendea ofisini ni nani atapambana na pesa chafu.
Waziri anapiga dili, naibu naye ni mtu wa madili, katibu mkuu(mf Jairo) ni madili kwa kwenda mbele, wakurugenzi hivyo hivyo, maofisa wadogo kadhalika, basi mwisho ni wananchi nao kupiga dili na watoto wetu tunawarithisha maisha ya madili.
Jiulize kama kesi zilizo wazi kama hizi za EPA, Meremeta zimetushinda ndiyo tutaweza kuwadhibiti wachawi kilingeni wakati tunashindwa kuwashughulikia wakiwa majumbani mwetu....MAWEEEE!!!!
Anti-Money Laundering inahitaji zaidi ya sheria...MAADILI kama taifa.
na MAADILI ni zaidi ya kusema tuache wizi, maisha ya watu yawe bora na mifumo iwepo kuhakikisha maisha ya watu ni bora wakati wote..ikiwa leo nipo kazini nanga zinapaa kesho nimestaafu itakuwaje, si ntakufa kwa kihoro na sononeko la moyo...ni kwa muktadha huo naamua kupiga dili ili niwe na uhakika wa maisha yangu baada ya kustaafu.
nikishapiga dili pesa zangu(dirty money) nazifanyaje??? inabidi nizisafishe kwa kuziingiza katika michakato halali(mf ntajenga jumba nikapangisha na kupata rental income etc) na hiyo ndiyo money laundering.....
Je, Mkuu unadhani ni vita nyepesi hiyo???