Tunapendana sana na mchumba wangu. Tumedhamiria kuoana lakini familia yake hainitaki, inataka aende chuo

Tunapendana sana na mchumba wangu. Tumedhamiria kuoana lakini familia yake hainitaki, inataka aende chuo

ze jj

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2012
Posts
497
Reaction score
592
Habari za usiku JF.

Mimi nimekuwa kwenye mahusiano na binti miaka mitatu sasa. Tumeamua kwa dhati tuoane, wazazi wake hawataki. Wamefikia kunitishia maisha. Ukweli ni kuwa nampenda sana, nae ananipenda Sana.

Tumeamua kuishi kwa pamoja bila kujali. Maana kisheria tuko salama maana siyo mwanafunzi. Amemaliza kidato cha sita. niko tayari akasome chuo lakini Kama mke wangu,nina shuguli yenye kuingiza kipato cha million 40 kwa mwaka.
 
Akienda chuo huyo sio wako ni wa jamii, ila mna maamuzi ya ajabu yani form six tu mnataka oana au mnadhani ndoa ni kama jkt mujibu wa sheria ukimaliza six unaenda tu.
 
Kwa post yako hii nmejikuta nikijiuliza hv adui wa kwanza wa Taifa (ujinga) ataendelea kutunyanyasa mpaka lin?
 
Unatishiwa maisha nawe bado unakomaa, tena na wazazi wake Sasa si umuache akasome upambane na maisha huenda utakuwa zaidi ya hapo....na akienda chuo jipange kisaikolojia.
 
Back
Top Bottom