SoC03 Tunapigana na adui tunaemfuga wenyewe

SoC03 Tunapigana na adui tunaemfuga wenyewe

Stories of Change - 2023 Competition

Msigwa Victor

Member
Joined
Sep 24, 2019
Posts
5
Reaction score
9
Nchi yangu mwenyewe inanitesa mimi mwenyewe, kila mtu anapambana na Adui anaejifugia.

Watanzania wengi wenye kujitambua wanajitahidi Kupambania suala la malezi katika jamii lakini namna wanavyo pambana inaleta ukakasi sana. Tunapambana na jambo ambalo hatujui chimbuko lake.

Tunaona biashara ya ngono inavyozidi kuwa na fahari katika mitandao ya kijamii,Viongozi kwenye idara mbalimbali wanalia na Mmonyoko wa maadili lakini vyanzo vya mmomonyoko wamevikalia kimya Eti ni mfumo wa maisha.

Katika mfumo wa maisha kwenye jamii yetu ya sasa unapelekea mmomonyoko wa maadili kwa namna tunavyoishi, Mfano familia kuishi nyumba yenye wapangaji hasa maeneo ya mijini(Familia imepanga, huku kijana wa chuo kapanga na binti wa chuo wanaishi pamoja).

Katika nyumba hiyo hiyo mabachela wanaingiza wanawake mbali mbali humo, Ikumbukwe kuna familia imepanga humo wote ni wapangaji japokuwa wengine wanafamilia.

Watoto wanakuwa huku wakiendelea kupata elimu ya maisha kwenye huo mzunguko aliopo katika ukuaji wake.

Hapo utegemee kukuza mtoto mwenye maadili, Hivyo hicho ni moja ya chanzo kikuu katika jamii yetu ya sasa kumong'onyoa maadili japokuwa jamii imefumbia macho.

Vipindi kwenye vyombo vya habari zetu sisi wenyewe vinapelekea mmomonyoko wa maadili,Mzazi kutwa yupo kazini watoto wapo nyumbani wao na TV. Mzazi kurudi jioni hajui watoto wamelishwa nini akilini mwao baada ya kushinda kwenye TV. Hapa jibu unalo.

Utajiuliza Kwanini watoto wa zamani walikuwa wanaangalia TV wakiwa na wazazi tu, kwanza walikuwa hawajui kuwasha tukawa na kizazi bora zaidi ukilinganisha na sasa.

Watanzania tunaangalia zaidi kwenye kutafta pesa ila suala la malezi imekuwa ni ziada, Mtoto peleka nursery akashinde huko kurudi jioni, au ashinde na binti wa kazi aliyekimbia katika familia yake kuja kumlea mwana. Hapa tutatafta adui tunaemfuga wenyewe.

Wazazi wanakuwa makini na kutafta pesa na kuwaachia watu ambao sio wazazi kuvaa majukumu ya kuwa Mzazi, mwisho wa siku watoto wanatoka kwenye misingi ya tamaduni zetu.

Hata hivyo mabinti kulelea watoto kwa wazazi wao inachangia mmomonyoko wa maadili.Zamani binti kupatia mimba wakati akiwa katika mkono ya wazazi ilikuwa ni nadra sana, adhabu kali zilitolewa katika jamii yetu. Saizi Binti anazalia nyumbani watoto watatu baba tofauti lakini kuna huku taasisi mbalimbali zikiundwa kuwatetea wakati kitu kama hicho ilikuwa ni mmomonyoko Wa maadili, binti alikuwa akifukuzwa nyumbani kwenda kwa aliyempa ujauzito.

Vitu vidogo vidogo vya utamaduni wetu vinavyopuuziwa ndivyo vinavyosababisha mmomonyoko wa maadili, tunapiga vita mmomonyoko wa maadili lakini hatudhibiti vyanzo vinavyopelekea.


Picha na Danny (Sema Tanzania)

83799847.jpg
 
Upvote 2
Back
Top Bottom