Tunapoambiwa kuwa Tanzania inakuwa 'Rebranded' ni vyema pia tukaambiwa nani 'aliichafua', lini na kwa manufaa gani

Wala hustahili kujitokeza kumsemea mhusika, ajitokeze yeye binafsi katika hili hakuna atakayekuunga mkono kwa kuwa wanajamvi na wananchi kwa ujumkla wana uelewa mkubwa tu.

Hilo eneo kuanzia chuo cha Mbegani, Zinga kwa Mtoro, Pande na Kiromo inasemekana watu wameanza kujisajili kulipwa fidia mara mbili. Wamasai na Wamang'ati wanaoishi kwenye pori hilo wanatishiwa kila siku kwamba wahame haraka vinginevyo watachomewa vijumba vya na mifugo-hofu imetanda.

Kuna kitu kimejificha kwenye mradi wa Bagamoyo sio bure mtathibisha hivi karibuni maana wako tayari kutumia nguvu kuuanzisha bila kuzingatia shuku ya dhuluma iliyokuwepo.
 
Hapo sikubaliani na wewe kabisa, juzi waziri mmoja wa uiengereza amejiuzulu nafasi hiyo baada ya kuenda kinyume na maelekezo ya udhibiti wa UVIKO sembuse makamu? Nyerere alijiuzulu uwaziri mkuu mwaka 1960 kwa kuona alikuwa kwenye nafasi kama kinyago tu.

Hana 'moral authority' ya kuwa 'critic' kwa mtangulizi wake la sivyo laana itamtafuna mpaka mifupa. Kwanini hajaitengua sheria iliyomwingiza makamu wa rais, waziri mkuu, jaji mkuu na spika wa bunge kutoshitakiwa kama kwenli ni mtenda haki?
 
Kwangu mimi Kassim ndio alitakiwa kuwa mtu wa kwanza kujiuzulu huyu ndio mtendaji mkuu wa serikali wa kila siku iweje asiwe anajua kweli? Makamu wa Rais bongo ni "cheo picha" tu

Naungana na wewe 100/100
Kassim Majaliwa angelinda heshma yake kwa kujiuzulu.
Ali fokea Umma.... kuwa Rais yupo busy kazi nyingi,ati tulitaka tumwome anatembea Kariakoo....n.k.
 
Hiyo bado sikuielewa ,

Yaani watanzania tumegeuka bidhaa??

Inawezekana lakini, maana ukute tushauzwa kitambo na hatufahamu Hilo.
 
Naungana na wewe 100/100
Kassim Majaliwa angelinda heshma yake kwa kujiuzulu.
Ali fokea Umma.... kuwa Rais yupo busy kazi nyingi,ati tulitaka tumwome anatembea Kariakoo....n.k.
Hata makamu naye ambaye kwa sasa ndiye mwenye kiti kikuu alifanya ziara Tanga ya siku sita wakati akijua bosi wake anaumwa tena akasema Rais anawasalimu na kwamba waendelee kuchapa kazi wakati akijua sio kweli.
 
Haya ndio maeneo nnayotamani kuona hiyo re-branding itayagusaje?

1. Elimu
2. Uongozi
3. Ulinzi na usalama
4. Afya
5. Ajira

Yapo mambo madogo madogo pia kama Nembo ya Taifa, Rangi za Taifa, vazi la Taifa, Maadili ya kijamii nk.

Kama wadaawa wengine walivyosema. Re-branding ni jambo pana sana na linahitaji watu wa kada mbalimbali kulifanikisha hilo

NAKUPENDA SANA TANZANIA
 
Unaumia sana yeye kuwa Rais baada ya JPM kufariki?.

Moral authority anayo na ndio inayomuwezesha kuongea na kufanya anayoyafanya.

Anakuwa critic kwa faida ya Tanzania sio ya mtu mmoja au wawili.

Swali la kwanini hakujiuzulu ni zito sana, hakuna aliyejua kuwa JPM angefariki march 2021 ni mipango ya Mungu.
 
Naona Dawa imekuingia eeeh? Safi sana
 
Acha kujipendekeza wewe, unaijua kesho kweli?

Nasisitiza tena hana hiyo 'moral authority' na tafadhali heshimu maoni ya mtu mwingine usilazimishe wengine kukubaliana na hoja yako butu kisa ni mnufaika wake.

Both internal and external resistance will cluster around the beef very soon until the landmark is resumed on track.
 
Samia na Magufuli ni kitu kimoja huo ndio ukweli. Wanatekeleza sera zile zile za Chama kile kile.

Ukinasa katika mtego wa personalities utawatenganisha wawili hao ukiutazama mustakabali mzima wa nchi hii hutazifikiria tofauti zao.

Better change your mindset as it is your downfall when it comes to realizing that the fate of our Tanzania is in the hands of this lady at Magogoni and Chamwino.
 
mimi sieliwi tuliambiwa Tanzania imepanda na kufika uchumi wa kati, leo tunaambiwa shuhuli zote zisubiri kwanza tujenge uchumi 🀣 🀣 🀣
 

Ninachojua rebranding ilianza wakati wa "bonge la kaka".
 
hata mama samia akimaliza mda wake ajiandae tu kwa maneno kama haya!
 
Msemakweli ni mpenzi wa Mungu. Au nasema uwongo ndugu zangu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…