Tunapoathiriwa na ujauzito wa wake zetu………..!

Mtambuzi

Platinum Member
Joined
Oct 29, 2008
Posts
8,809
Reaction score
15,421

Utafiti wa hivi karibuni uliofanywa katika kujaribu kuona kama ujauzito wa mke unaweza kumuathiri mume, umeonyesha kwamba, kuna uwezekano huo na imekuwa ikitokea kwa wanaume katika idadi ya kutosha. Imebainika kwamba, kuna homoni zipatazo tatu ambazo kiwango chake huwa kinapanda wakati mwanamke akiwa mjamzito na hasa anapokaribia kujifungua. Homoni hizi kwa mwanaume hupanda na kushuka wakati kama huo yaani mke anapokaribia kujifungua.

Hii ina maana kwamba homoni hizo ambazo huwa zinahusiana na hofu na matarajio ambapo kwa mwanamke huwa ziko juu anapokaribia kujifungua, kwa mwanaume hupanda na kushuka na hivyo kumpa tabia ambazo huwa hanazo wakati mwingine. Utafiti huu unadhihirisha kwamba, kuna ukweli wa kutosha kwamba, mwanamke anapokuwa mjamzito, mume naye anaweza kuwa na mabadiliko ya hali kutokana na mabadiliko ya homoni mwilini mwake. Ni vigumu hata hivyo kusema kama mabadiliko hayo yanaweza kumfanya mume naye akawa anatapika, kukasirika, au kula vitu vya kutia balaghamu ulimi kama ndimu, pilipili na udongo.

Wanaume kadhaa wamesharipoti kujikuta wakibadilika katika tabia na hali nyingine za kimwili kila wakati wake zao wanapokuwa na ujauzito. Kwa utafiti huu naweza kusema kwamba, madai haya yanaweza kuwa na ukweli. Lakini pia ukweli kwamba wanaume wengine huwa wanapata kiwewe cha furaha na (au) wasiwasi kila wake zao wawapo wajawazito ni jambo la kuzingatia.
 
Ni vigumu hata hivyo kusema kama mabadiliko hayo yanaweza kumfanya mume naye akawa anatapika, kukasirika, au kula vitu vya kutia balaghamu ulimi kama ndimu, pilipili na udongo.

Mutambuzi ugumu upi mwenzetu unaouona? Wanaumme hawatapiki au kula vitu vya kuuburidisha ulimi.............kukasirika kama wanakosa unyumba labda.................
 
Tatizo wanaume huhisi wivu wa kuja kukosa kukumbatiwa pindi mtoto azaliwapo ndo sababu ya wao kuwa na kisebusebu na kiroho papo.
 
nini mimba!mimi siku 3 au 4 kabla wife hajaona mwezi hutoka kipele kimoja usoni!amini usiamini utake usitake ndio hivyo kwangu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…