Shayu
Platinum Member
- May 24, 2011
- 608
- 1,655
Leo nilikuwa nasoma nikaamua kupitia kazi moja ya mwanafalsafa wa Ujerumani anayeitwa fredrich Hegel kwenye kazi yake ndefu inayoitwa PHILOSOPHY OF RIGHT. Ameongea mambo mengi ya kufikirisha kitabu hiki ni mkusanyiko wa tafakuri nyingi kuanzia siasa hadi mambo ya kijamii kama ndoa na familia, lakini pia METAPHYSICS.
Kitabu hiki ni miongoni mwa vitabu vigumu vya falsafa nilivyopata kuvisoma ili kukielewa inakubidi uwe na uwezo mkubwa IMAGINATION Ili kuelewa vizuri kiko very absract.
Sababu ya kutaja kitabu hiki na kujaribu kushare nanyi fikra zangu za siku nyingi kuhusu masuala ya familia na ndoa na uhusiano wake na jamii pamoja na taifa kwa ujumla katika ujenzi wa jamii iliyobora. Ingawaje familia inadhauraliwa ni kiungo bora na muhimu sana katika ujenzi wa taifa lolote lile imara na jamii yenye uhusiano mzuri.
Binadamu ni kiumbe anayeishi katika jamii afya yake ya kiakili na kimwili inategemea sana mahusiano yake na jamii lakini pia maendeleo yake kama mtu yanategemea uwepo wake katika jamii.
Kwahiyo Afya yetu ya kiakili na kimwili inategemea sana jinsi tunavyoishi pamoja. Kitu pekee ambacho kitafanya mahusiano yetu kama binadamu yaboreke na huu ndio msingi ni upendo.
Katika biblia kuna aya inayosema mpende bwana mungu wako kwa roho yako yote na kwa moyo wako wote na jirani yako kama umavyopenda nafsi yako:
Ukiangalia hii haya kwa umakini utagundua kitu kimoja kwa jamii yeyote ili iwe na harmony miongoni mwa unit zinazounda jamii na taifa huu umoja lazima uwepo na bila upendo umoja huu na muunganiko huu kamwe hauwezi kuwepo. Ni upendo pekee unaounganisha watu katika muunganiko ulio sawa bila upendo hakuna umoja. Na hii ni sheria katika jamii na katika ndoa.
Ndoa ni social contract kama alivyoita Hegel, ni mkataba wa kuungana kati ya mke na mume na mkataba huu unatambulika kwa watu wengine katika jamii ili kuunda social unit ambayo ni familia. Kwahiyo watu watatambua kwamba wale ni mke na mume wana haki zao kama mume na mke. Kwahiyo kutoka nje ya mkataba ni kosa au kuharibu ndoa ya mtu ni ukiukwaji ya sheria ya jamii na sheria asili . Wakati watu wanaoana si miili tu inaungana katika level ya juu akili na roho pia vinaungana ili kuunda mwili mmoja.
Ndio maana hakuna mtu anayeweza kuchekelea mke wake kuchukuliwa na mtu mwingine. Kwahiyo ni muhimu jamii kulinda ndoa ili kujenga jamii yenye afya inayotenda haki na yenye maadili.
Kwahiyo ndoa ni social contract na ni kiungo muhimu sana katika kujenga Taifa imara na lenye tija. Pale familia katika taifa lolote zikiwa zimesimama na zikiwa zenye umoja mara nyingi mataifa hayo huendelea kwasababu ya uwajibikaji na nidhamu ndani ya familia pamoja na mahusiano yao na majirani ambao pia familia zao ziko imara, hivyo kuunda jamii imara yenye mwelekeo mmoja wa kutengeneza jamii bora na Taifa imara.
Kwahiyo nidhamu ni muhimu sana ili kuunda familia imara ambayo itakuja kuunda mahusiano mazuri miongoni mwetu kama majirani na kama jamii kisha taifa. Kama tunataka kuunda harmonius society ni lazima tuangalie mambo haya ya msingi.
Siasa haijaundwa kuharibu social structure na social pattern ya jamii bali kuijenga . Kama siasa inaharibu mfumo mzima wa mahusiano yetu haifai na haina tija, ni muhimu kuishi kama watu wamoja ambao mwelekeo wao ni mmoja mengine ni uongo na ulaghai. Umoja wa watu wa Taifa hili ni jambo la msingi sana.
Leo hii tunashuhudia siasa za ubinafsi zimetawala taifa hili, mfumo wa kijamii ukiwa umeanguka kila mtu akijiangalia mwenyewe, ni wakati sasa wa kubadili aina za mawazo yetu na kuweka focus katika ujenzi wa taifa hili tukifanya hivyo tutakuwa na baadae nzuri na tutakuwa na dira kama Taifa katiba mpya haiwezi kujenga haya.
Taifa lolote lile hujengwa mioyoni na akilini mwa watu vile vile hubomolewa mioyoni na kwenye akili za watu. Kama hatupendani wenyewe kwa wenyewe hatutaweza kujenga taasisi zozote zitakazo wahudumia watu kwa ukamilifu na kwa upendo. Taasisi hizi hazitaweza ku deliver kwa watu kama hakutakuwepo na upendo. Huu ni wito wa mabadiliko ya mioyo na akili zetu kwasababu bila ya hivyo hatutakuwa na mwelekeo kama taifa. Tumeweka matumaini katika katiba lakini katiba haitaweza kutusaidia kama mioyo yetu ni ile ile na akili zetu ni zile zile ni lazima tutende haki, tupende raia wenzetu na tuwe tayari kutumikia. Kwa njia hii pekee tunaweza kunyanyua taifa hili tukijua ya kwamba kila mtu anayeunda Taifa hili ni mtu muhimu sana.
Katika Taifa hili hakuna mtu ambaye si muhimu hata wale tunaowaangalia kwa macho ya pembeni. Wakati umefika sasa wa kujenga umoja katika taifa hili na kuleta mwelekeo. Wakati umefika sasa wa kuwa wa kweli wa nafsi na roho juu ya taifa hili. Ni lazima tufikiri sasa.
Jamii yeyote ambayo inahangaika kwenye kutafuta mali tu bila pia kujenga misingi ya mahusiano yao kamwe haitoweza kuwa na furaha. Kwasababu pesa itakuwa ndio msingi wa maisha yao. Uhusiano wao utakuwa duni na tunaweza kupima mwisho wa jamii hii kwa matendo yake na kuujua. Ni dhahiri sio mwisho mzuri.
Ni muhimu sana kujenga values katika Taifa letu kwasababu bila ya hizo hatutafika mbali kama jamii na kama Taifa. Tunapenda kuona kila mmoja wetu akipata heshima na akitambulika katika taifa lake mwenyewe. Tunahitaji kujenga uzalendo na kutumikia.
Kama Taifa kwasasa hatuna mwelekeo kila mtu anafuata njia yake kila mtu anajiangalia mwenyewe lakini hatuangalii kilicho kikubwa zaidi maendeleo ya Taifa letu. Ubinafsi wetu umepitiliza mipaka mpaka tunauziana madawa wenyewe kwa wenyewe na kuua tembo ni wakati sasa wa kuleta ORDER na mwelekeo katika taifa hili. Ni wakati sasa wa kujenga moyo wa uzalendo kwa watu wetu wote.
Nawaacha kwa quote kutoka kwa Aristotle na Hegel
EVERY STATE is a community of some kind, and every community is established with a view to some good; for mankind always act in order to obtain that which they think good.
Community si watu wanaoishi pamoja tu bali ni watu wenye malengo mamoja na wenye mashirikiano na wenye mwelekeo mmoja ni watu wanaopendana na wenye dira moja. Kwahiyo ni lazima tufanye matendo yatakayo tupeleka kwenye sehemu fulani nzuri. Kwenye maendeleo, kwenye upendo na kwenye umoja.
Aina hii ya Taifa ni lazima tulijenge, tofali baada ya tofali kwasababu inawezekana. Kwahiyo tunapojaribu kujenga uchumi tusisahau mahusiano yetu. Kwasababu maendeleo yetu yatategemea sana mahusiano yetu.
Mahusiano yetu yako mengi eg Walimu na Wanafunzi, watu katika familia, jirani na jirani, vyama vya siasa, Mashirika na wananchi na wote tuhamasishane kujenga Tanzania iliyo bora yenye upendo na umoja, yenye watu wenye kutimiza wajibu wao na wenye jitihada katika kujenga Taifa lao lakini pia Tanzania ya watu wanaoheshimiana . Ni MUHIMU kutimiza wajibu wetu wa kijamii na wa kitaifa hili linawezekana kama tutakuwe wenye nidhamu kwasababu bila nidhamu hatutaweza kulinda taifa hili na jamii zetu dhidi ya uharibifu.
'' If the state is confused with civil society, and if its specific end is laid down as the security and protection of property and personal freedom, then the interest of the individuals as such becomes the ultimate end of their association, and it follows that membership of the state is something optional. But the state's relation to the individual is quite different from this. Since the state is mind objectified, it is only as one of its members that the individual himself has objectivity, genuine individuality, and an ethical life. Unification pure and simple is the true content and aim of the individual, and the individual's destiny is the living of a universal life. His further particular satisfaction, activity and mode of conduct have this substantive and universally valid life as their starting point and their result.'' - Fredrick Hegel
Kwahiyo hapa Hegel ametofautisha kati ya ''State'' na ''civil society'' kama nilivyowahi kuandika katika andiko langu moja humu ndani ya kwamba hatujawa taifa bado ni kundi la watu tu tunaoishi pamoja kila mtu akitafuta chake ila tuwe taifa ni lazima tuwe na dira moja na mwelekeo mmoja na huu Utaifa unaweza kufanyika katika kiwango cha juu mno mpaka baadae tukashindwa kutenganisha watu wetu na ardhi yao kwakuwa watakuwa wameunganishwa nayo. Kwa hali tuliyo nayo sasa bado hatujawa taifa ni ''civil society'' kama mantiki ya Hegel ukiangalia kwa undani unaliona hili kwasababu tumekuwa jamii ya makundi na ya watu wanaotafuta interest binafsi na ile coherence imepotea ambayo ni muhimu katika uundaji wa Taifa lolote. Tunaona watu wakidai uraia wa nchi mbili hii ni hali halisi ya watu kuishi katika civil society na sio state kama nadharia ya Hegel.
Kwahiyo hii universal life anayozungumzia Hegel haipo. Katika mazingira haya ya kila kutafuta cha kwake bila kuangalia interest za pamoja maisha ya kimaadili hupungua sana.Uongozi unakuwa wa kununua na viongozi watakuwa wakitafuta faida binafsi na sio ya taifa kwa ujumla wake. Kwahiyo ni wakati sasa wa kujiangalia upya kama jamii kwasababu kuishi kama civil society na sio state ni hatari.
Mambo haya yote yanaonekana dhahiri machoni mwetu ni muhimu sana kuchukua hatua sasa ili kuokoa elimu yetu na jamii yetu na kujenga umoja wa nchi na mwelekeo.