Tunapolalama badala ya kuwakomalia wezi wetu

Tunapolalama badala ya kuwakomalia wezi wetu

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Hili lilikuwa letu. Hili halikuwa la Samia, Majaliwa wala Kadogosa.

Wenye nchi tulikuwa sisi. Tena si wa wakulalama. Bali kuwafurusha wote na kuwataka kurejesha vilivyo vyetu na viboko juu.

FsZVMM0WAAIYKQz.jpeg


Haya yametokea Rais yupo? Waziri mkuu yupo? Kadogosa yupo? Kumbe walikuwa na kazi gani?

Maajabu ya Mussa Sasa tupo tunalalama. Kwamba vipi wangali ofisini? Watatoka vipi? Kwa ridhaa yao?

Dua la kuku tangu lini likampata mwewe?

Kwani aliyetambua utofauti wa masikio ya kenge na masikio mengine hakuwa kafanya utafiti?

Kwamba nyomi tunazo ila kwa shughuli muhimu kama hizi hatuna? Tunapaswa kujihoji sana chini hadi juu. Nchi ni yetu wenye maamuzi ni sisi.

JamiiForums298906090_512x311.jpg


Ni uzwazwa uliopitiliza kubakia kulia lia wakati majizi yetu yanajulikana na kazi yao ya wizi ikiendelea.

Kwamba tunalia lia, mbona hata wao wanatushangaa?
 
Back
Top Bottom