Tunaposikia ya Makamba na Zitto kutaka kubinafsisha TANESCO, tukumbuke yaliyofanyika TTCL

Wakati mwengine nenda kwenye web ya Tanesco View attachment 1948497
Boss, kama mkataba umesainia ni kwasababu JPM aliagiza hivyo baada ya issue ile ya nyanda za juu kusini kule nadhani. Hakuna uzalishaji wa umeme kutoka sekta binafsi zaidi ya SONGAS kwa sasa. Na kwa mkataba huo, unathibitisha nilichosema, HAKUNA KAMPUNI BINAFSI itakayoweza kuuza umeme, ila kuzalisha tu.

Narudia tena, tatizo sio uzalishaji wa umeme, Tanesco inahitaji angalau iweze kugharamia inachozalisha na kuuza ili iweze kusonga mbele, huwezi kuzalisha na kununua umeme kwa gharama ya juu kisha ukawa na uhakika wa kuuza kwa gharama ya chini takribani mara mbili ya uhalisia kisha ukasema tatizo ni UZALISHAJI hivyo tukiongeza uzalishaji, tunatatua yaliyopo.
 
Symbion nao ni serikali?
 
Mbona peramiho kuna mapadiri wanazalisha umeme na kuuza tanesco!?
Na wanapata faida, ni sawa na SONGAS tu mkuu, zamani walikuwepo IPTL, AGGREKO, SYMBION, Ngeleja alikuwa anawaleta KILWA ENERGY n.k pamoja na wote hao kuwepo, matatizo ya umeme wakati huo wote waliokuwepo yalikuwa ni zaidi ya wakati huu wasiokuwepo, unadhani ni kwanini?

Sipingi watu binafsi kuwa hawawezi kuzalisha na kuiuzia Tanesco, zaidi ninachosema, hiyo ndo niia pekee ya hao BINAFSI wanayoweza kuitumia kuipiga Tanesco, ila mpaka sasa hakuna juhudi zozote za kusema kuwe na kampuni binafsi inayosambaza umeme kwa wananchi ili kuleta ushindani kwa Tanesco kama yalivyo makampuni ya simu, unadhani shida ni nini? Sheria inaweza badilika tu kama jambo hilo lina tija, ila UNADHANI kwanini hilo halijawahi kuwa wazo kwa serikali ili kutatua shida iliyopo?
 
Symbion nao ni serikali?
Nijuze kama Symbion bado wanazalisha umeme hapa, taarifa nizijuazo, waliondoshwa pamoja na wengine wote akabaki SONGAS ambaye naye alikataliwa extension na JPM hivyo ilikuwa mkataba uishe 2024 na aondoke, abaki PANAFRICAN tu, sijui kama itaendelea kuwa hivyo baada ya jamaa kuondoka.
 
Naomba nifunge mdogo wangu!!..Jambo ulisolijua ni Sawa na Usiku wa Kiza!!..
 
Tunaongozwa na siasa sana!!... wakati mwengine watu wanapewa Tender kwasababu mtu flani anataka!!.. Tanesco ni zimwi, Watanzania wanapata umeme na umeshushwa bei!!.. Lakini hakuna vyanzo vipya vya Shirika kwenye uzalishaji?!!...
 
Naomba nifunge mdogo wangu!!..Jambo ulisolijua ni Sawa na Usiku wa Kiza!!..
Ningekuwa Muha, ningekwambia hujajibu swali hata moja kati ya mengi niliyokuuliza, uzuri umeamua kufata njia za kisiasa.

Ni sawa, niko gizani kuhusu hili, nilijaribu kuleta mazungumzo ya vijiwe vya kahawa kwenye forum ya Great thinkers😊
 
Umeongea point nzuri Sana mkuu.. Jinsi watanzania wanavyopitia magumu ya tozo na Kodi ili kujenga hii miradi mikubwa alionzisha Maguful, Leo hii watu wanataka shirika Muhimu kama Tanesco wapewe watu binafsi. Nini maana ya watanzania kukamuliwa kujenga bwawa ya Rufiji.. Bora bwawa likamilike kwanza lianze kuzalisha umeme tuone faida na hasara zake hapo ndo tuamue sasa kwamba tuwape watu binafsi... Lakini kwa Sasa tuache shirika libaki mikononi mwa Serikali.
 
Hawapewi bali wananunua hisa za hayo mashirika husika, hivyo si sahihi kuona kama linatolewa bure bure. Pili mpaka sasa sijaona mradi wa serikali ambao unaweza kujiendesha bila ruzuku kutoka serikalini, hivyo kuendelea kukaa nao ni kuzidi kutia hasara. Kama una mfano hata mmoja uweke hapa
 
Sasa hivi Ttcl Iko wapi
 
Tanesco ina madeni tu na bado haijaweza kulipa hata robo!!!...Acha propoganda

Wewe Acha kubisha bisha ongea facts Tanesco ina deni gani !?
Ikiwa JPM aliitoa kutoka kwenye mikataba ya kununua umeme wa Bei ya juu na kuuza kwa bei ya chini na nimekupa mfano wa IPTL ,
Sasa propaganda ipo wapi apo !?
Tanesco inazalisha umeme sasa hivi karibu Megawatts 2000 ambayo imezidi mahitaji ya ndani kwa sasa ya Megawatts 1500
Sasa kwako propaganda ni Ipi katika hizo hoja !?

Au Sababu unataka tu tukubaliane na Tanesco kuuzwa kwa hoja nyepesi!?
Vyovyote iwavyo kuna vyanzo vya uchumi ambavyo hutakiwi kuuza wala kubinafsisha kamwe ata vilete hasara kiasi gani
 
Nimeamua kukaa kimya!!..Kuna wanaoidai Tanesco tokea 1990 Hadi Leo na bado hawaja lipa hata nusu ya deni!!...sitaki kuongelea wengine hapa!!..
 
Wakati mwengine unaamua kukaa kimya kwasababu unaweza kutoa vitu humu watu mkaanza kuhoji imekuaje?!!...Hakuna shirika lina madeni kama Tanesco!!...Hi nasema 1990 lakini kuna madeni ya 1985 huko hadi sasa wanalipa kidogo kidogo na bado hayawezi kulipika!!..
 
Mnaleta siasa kwenye Tanesco oh oh JPM unajua kuna wanaoidai Tanesco tokea kipindi cha Mwalimu?!!..Hadi Leo ni miaka mingapi?!!.. Unadhani Tanesco inahitaji iingize fedha nyingi namna gani na huku bado inaongeza madeni?..Hivi kuna mtu uliwahi kusikia kaachana na mkataba na Tanesco bila kusikia wanaidai Tanesco na mahakama juu!!..
 
Tumekuja kwenye bei ya chini kwasababu wazalishaji umeme wamekua wengi!!.. Tanesco ikipewa Sekta binafsi tutalipwa madeni yetu ya miaka mingi na shirika litaendeshwa Kwa ufanisi mkubwa!!!... Kwenye hili tuache siasa kabisa!!.. Shirika linadaiwa zaidi ya miaka 10 hiyo interest inakuaje, Fikiria huyu ni mtu binafsi!!...
 
Nakubaliana na wewe ndio maana nikasema mikataba mikubwa yenye maslahi ya Taifa iwe wazi watu wasijifungie maofisini na kusign mikata ya namna hii.
 
Yule nshomile kaachiwa tutaona kila aina ya mauzauza
 
Ok wachumi wanasema ushindani ndio unaweka bei ya unafuu kwa mlaji. Sasa hayo mashirika au kampuni tatu zikishabinafsishwa si bado zinaendeleza ukiritimba kwenye maeneo yao ie production transmission na distribution? Kwenye production unaweza kua na ushindani ila kwenye usafirishaji na usambazaji umeme itawezekanaje ushindani bila dublication ya miundombinu. Kuna alisema eti kuna technology ya kusambaza umeme kwa mawimbi hewani. Sijawahi kusikia.
 
Sio kweli mzee ,wazalishaji walikua wengi kama IPTL ,Aggreko symbion nk na bado Bei zilikua juu Tanesco aliuziwa umeme kwa bei za kitaahira wakati yeye aliuuza kwa hasara,
Wote tuliona tulivokua tunalipia adi Capacity Charges kwenye kila unit ya umeme tunayonunua mzee usilete siasa kwenye hili ata kama akitajwa JPM unasikia kichefuchefu naona kwako ni kutajwa kwake Ndio tatizo,it’s okay hata sie tulitofautiana nae mitazamo kwenye baadhi ya mambo ikiwemo Korosho,ila alipopatia tutasema ata kama ni ukweli mchungu!
Mfano alitoa umeme Gas Unit inauzwa sio chini ya tsh 140 ,wa mafuta unauzwa hadi tsh 400,hivyo hivyo kwenye vyanzo vingine kama upepo,nuclear nk ukilinganisha na umeme wa maji ambapo unit inauzwa kuanzia tsh 50/60
Sasa kwanini usipongeze kwa vyanzo kama Bwawa la Nyerere ,(Stieglers Gorge) ?

Umekomaa tu Tanesco ina madeni ya Toka sijui mwaka 1990 kwa iyo iuzwe!
Kwa iyo Tuuze hadi nchi eti tu sababu ina madeni ya toka mwaka 1970 !?

Una sahau kuwa madeni mengi ya Tanesco na nchi yetu ya natokana tu mikataba mibovu isiyo na tija Na usimamizi mbovu wa rasilimali zetu !?
Kwako wewe solutions ni kuuza ????
Mzee we don’t buy hizo sounds zenu No Thank You !
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…