Shayu
Platinum Member
- May 24, 2011
- 608
- 1,655
Ukweli ni kwamba kama unanipenda utaniheshimu. Huwezi kuniambia unanipenda wakati huniheshimu. Mapenzi huonekana katika heshima. Kama unampenda mke wako utamheshimu na kama una mpenda mume wako utamheshimu, na kama mnaheshimiana mtajenga nyumba yenye heshima.
Ukweli ni kwamba mtu yeyote anayekupenda atakuheshimu. Hawezi kufanya upuuzi. Je tunajenga mahusiano yetu katika misingi ya kuheshimiana?
Misingi ya kuheshimiana katika nyumba ikipungua hakuna familia itakayo simama imara. Ni lazima kuwe na mke msikivu na baba anayejiheshimu na kuangalia mwenendo wake kwa ukaribu.
Baba ambaye hafundishi watoto kwa maneno bali kwa matendo. Tunaambiwa baba ni kichwa katika nyumba hii ni kweli. Asipokuwa na misimamo akiwa legelege nyumba haitosimama. Baba yeyote lazima atafute busara juu ya yote. Utawezaje kujenga nyumba pasipo maarifa na busara? Misingi yake inawezaje kuwa imara?
Hakuna kitu kizuri kama familia yenye umoja na baba ambaye kauli yake inasikilizwa kwasababu ni yenye busara. Baba ambaye atawapeleka watoto katika mwelekeo unaofaa. Haitoshi kumpatia mtoto chakula, malazi na mavazi peke yake. Kisha tukasahau akili yake na roho yake. Tutampeleka shule lakini haitoshi, mtoto anahitaji muongozo kutoka kwa baba. Tabia yake ni muhimu sana katika maisha yake ya baadae.
Mwanamke na Mwanaume wanapoungana lengo kuu ni kutengeneza familia . Na fikra zote za watu walioungana lazima ziwe kwenye kujenga familia. Kwa mtu anayefahamu anachokifanya hawezi kuacha jukumu hilo na akili yake kugeuka sehemu nyingine, anaamini huko ni kutowajibika ipasavyo kama baba au kama mama. Anajua huo sio mfano bora kwa watoto. Mtu anayechepuka hana akili timamu hajui anachokifanya katika ndoa ni mtu mwenye akili mbili. Hampendi mke wake, hapendi watoto wake na wala hapendi familia yake. Familia haiwezi kuwa na umoja kama watu wanachepuka katika ndoa na kama watu hawaheshimiani.
Kuna suala lingine la ulevi kuna watu walevi hadi wanasahau majukumu yao katika familia zao. Wanatumia muda mwingi bar kuliko familia zao. Huu ni ujinga mwingine. Tunahitajika kukaa na familia zetu. Kuongea na watoto wetu na kuwapa muongozo juu ya maisha. Tunahitajika kuzipa familia zetu umuhimu wa pekee. Tunapotaka uwajibikaji katika serikali tuanze na familia zetu kwanza tuwajibike huko kisha tutakuwa na haki ya kuiambia serikali wajibika! Nchi ambayo ina strong famillies haiwezi kuwa na serikali ya kizembe. Hii namaanisha nini familia imara lazima zitaungana tu kwasababu zinajali kuhusu baadae ya watoto wao na taifa lao wataidai serikali yao iwajibike na sauti yao itasikika. Ili tujenge taifa hili lazima tuanze na msingi wa familia huu ndio mtazamo wangu. Hatutakuwa na taifa imara bila ya kuwa na familia imara. Kwahiyo watu walioa wajue nafasi yao katika taifa hili. Kwamba wao pia ni viongozi tena sio wadogo. Wana mamlaka makubwa dhidi ya familia zao na uwezo wa kujenga tabia za watoto kuwa raia bora.
Kuchepuka ni ufisadi dhidi ya familia yako unahamisha mshahara kutoka kwenye mfuko wa familia na kupeleka kwa hawara ukikosa uaminifu katika familia yako unaweza kuwa mwaminifu katika nchi? Mtu wa namna hii hapaswi kuiropokea serikali kuwa haiwajibiki au ya kifisadi. Tujiangalie na tujichunguze kwanza. Ni ujinga na kutokujua unachokifanya. Hatuwezi kuendelea kujiendekeza. Unawezaje kuwa kiongozi wa watu bila kuangalia mambo haya ya msingi. Kiongozi ni kuonyesha watu njia iliyosahihi na salama kupita. Ni lazima tukumbushane mambo haya muhimu. Bila kukumbushana mara kwa mara huwa tunapotea na kutoka katika njia iliyosahihi. Na Tujue kwamba heshima yetu ndani ya familia ni muhimu kuliko kitu kingine. inapovunjika ni ngumu kuirejesha. Naongea na nyinyi vijana; familia ni kitu muhimu sana katika maisha yako usiichezee. Fahamu ulichonacho ni chenye thamani sana. We must speak this with the strong tone of voice kama tunajali kuhusu taifa hili.
Familia zetu zikiwa na nidhamu natumaini tutakuja kuwa na serikali yenye nidhamu na inayowajibika kwakuwa tutakuwa na watoto waliolelewa vyema kwa maadili na nidhamu bora. Kwa mtu mwenye akili timamu kabisa atawajibika katika familia yake ipasavyo katika maadili yanayohitajika. Kwasababu maadili yetu na nidhamu zetu ndizo zitakazojenga nchi bora.
Maadili ya watoto yanaanzia katika familia na kuja jamii inayomzunguka. Kwahiyo kila mzazi anawajibika katika kujenga familia bora. Ili nchi ipate raia walioabora na wawajibikaji katika jamii zao na katika taifa lao. Hatuwezi kuzalisha chochote cha maana kama tutadharau misingi hii ya kimaadili katika familia. Nchi imara ni ile yenye familia imara ambazo zinajua wajibu wao kwa taifa. Ulinzi wa taifa letu ni kwa kuangalia maadili yetu pia taifa hili halitosimama kama hatuna maadili.
Tunapoanza kujenga taifa; tunaanza na msingi wa familia. Kwasababu huko ndipo tutakapo pata raia waliobora. Ukuaji na maadili ya familia ni muhimu katika ujenzi wa taifa imara.