Tunapunguza vipi foleni jijini Dar es Salaam?

Tunapunguza vipi foleni jijini Dar es Salaam?

Mtoto wa Nyerere

Senior Member
Joined
May 21, 2021
Posts
129
Reaction score
689
Dar es Salaam ni Jiji lenye harakati nyingi sana ila foleni mjini imekuwa kero ukiunganisha na joto lilipo hapa.

Je, tunafanya nini ili kupunguza foleni katika jiji hili maana kupanua barabara pekee sioni kama ni suluhisho la moja kwa moja

Na tuna mkakati gani wa kuanza kuzuia majiji mengine ambayo yanakua kwa kasi yasiwe kama jiji la Dar es Salaam?

Jiji kama Mwanza, Mbeya na Arusha tayari foleni zimeshaanza?

Wadau wa sector hii njooni hapa tupange nini kifanyike.
 
Flyinterchange kila kona tu hakuna namna achana na izo za mfugale
 
Mabasi ya mwendo kasi yakiwekewa utaratibu wa level seat foleni dsm utakuwa historia. Hii inawezekana. Tatizo mabasi yamegeuzwa biashara ya mtu fulani. Hayana ustaarabu hata kidogo.

Abiria wanarundikana ndani kama magunia ya viazi na serikali inachekelea bila ya kuchukua hatua stahiki. Nasikia harufu ya rushwa kwa baadhi ya maofisa wa serikali (wizara ya fedha) wanaosimamua mradi huo. Wakiamua kuwajali wananchi foleni kwisha
 
Dar es Salaam ni Jiji lenye harakati nyingi sana ila foleni mjini imekuwa kero ukiunganisha na joto lilipo hapa.

Je, tunafanya nini ili kupunguza foleni katika jiji hili maana kupanua barabara pekee sioni kama ni suluhisho la moja kwa moja...
Uwezo wa Kufikiri wa VIONGOZI na CCM UMEFIKA MWISHO.

KATIBA MPYA ndio SULUHISHO itatupatia VIONGOZI wenye Uwezo wa Maarifa mapya
 
Njia za gharama na zisizo na gharama au zenye gharama hafifu katika kukabiliana na foleni Dar (na katika majiji mengineyo)

1.kuongeza/ kuzidisha ujenzi wa barabara za juu katika makutano (flyovers na interchange)

2.ujenzi wa miradi ya reli ambayo inaweza kusafirisha watu wengi kwa pamoja

3.upanuzi wa barabara zilizopo ili kurahisisha

4.kutanua (upatikanaji wa) huduma za jamii mfano kujenga masoko maeneo ya pembezoni mwa jiji/mji

5.kuwapo kwa miji midogo midogo yenye miundombinu yote ya msingi ili kuzuia au kupunguza watu wengi wasiende mjini (nadhani hii haina tofauti sana na namba 4)

6.ujenzi wa viwanja vya ndege na kuweka mazingira rafiki ya usafiri wa anga

7.kuimarisha bandari

Hata mimi
 
Back
Top Bottom